RAIS WA ZANZIBAR NA
MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEUTAKA UONGOZI WA
CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR –SUZA KUHAKIKISHA KUWA UPANUZI WA MITAALA,
UFUNDISHAJI NA TAFITI ZINAZOFANYWA NA CHUO HICHO ZINAELEKEZWA KATIKA KUTOA
MICHANGO NA RAI ZITAKAZOCHANGIA NA KURAHISISHA UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA
MAENDELEO YA NCHI.
AKIZUNGUMZA WAKATI WA MAHAFALI YA TISA YA CHUO KIKUU
HICHO YALIYOFANYIKA LEO HUKO TUNGUU, MARA BAADA YA KUWATUNUKU VYETI, STASHAHADA
NA SHAHADA WAHITIMU 763 DK. SHEIN AMESEMA NI JUKUMU LA VYUO VIKUU HASA VYA
SERIKALI KUTOA TAALUMA INAYOLENGA KURAHISISHA UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA
MAENDELEO TAIFA NA JAMII KWA UJUMLA.
KWA HIYO AMEBAINISHA KUWA ZITIHADA ZINAZOFANYWA NA
CHUO ZA KUKUZA ELIMU ZITAKUWA NA MANUFAA ZAIDI ENDAPO ELIMU ITAKAYOTOLEWA
ITALIONGOZA TAIFA NA ITATUMIKA KURAHISISHA MAISHA NA KUIMARISHA MAENDELEO KWA
KUSAIDIA UTEKELEZAJI WA DIRA YA MAENDELEO 2020, MKUZA II, MALENGO YA MILENIA NA
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM.
DK. SHEIN ALIWAELEZA WAHITIMU, JUMUIYA YA WANACHUO NA
WAGENI WALIOHUDHURIA MAHAFALI HAYO KUWA SERIKALI INAZIUNGA MKONO JITIHADA
ZINAZOFANYWA NA CHUO HICHO ZA KUONGEZA MAFUNZO YA NYANJA MBALIMBALI KWA KUWA
INAAMINI KUWA MAENDELEO YA NCHI YANATEGEMEA NGUVUKAZI YENYE ELIMU YA KUTOSHA.
KWA HIYO ALISISITIZA KUWA SERIKALI INA KILA SABABU YA
KUIMARISHA MASLAHI YA WATUMISHI WA SUZA KILA HALI YA UCHUMI ITAKAPORUHUSU NA
KUONGEZA KUWA AZMA NI KUHAKIKISHA KUWA MASLAHI YANAKUWA MAZURI HADI KUWAVUTIA
WALE WALIOKO NJE KURUDI CHUONI HAPO.
HATA HIVYO MHESHIMIWA RAIS ALIHIMIZA WATUMISHI WA CHUO
KUFANYAKAZI KWA BIDII NA KUJITUMA BILA KUSUBIRI KUHIMIZWA KWANI KUENDELEA NA
MTINDO WA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA HAKULISAIDII TAIFA WALA WATUMISHI WENYEWE KWA
KUWA NCHI INAZIDI KUBAKI NYUMA HIVYO KUSHINDWA KUBORESHA HATA MASLAHI YAO
MWENYEWE.
DK. SHEIN ALIELEZA KUWA AMERIDHIKA NA JITIHADA ZA CHUO
HICHO ZA KUZIDI KUONGEZA NYANJA ZA MASOMO AMBAPO KATIKA KIPINDI KIFUPI CHUO
HICHO KIMEWEZA KUONGEZA PROGRAMU MPYA TISA ZIKIWEMO MBILI ZA SHAHADA ZA
UZAMILI, FANI TANO ZA KIWANGO CHA SHAHADA NA MBILI ZA KIWANGO CHA STASHAHADA.
ALIKIPONGEZA CHUO KWA KUANZISHA MAFUNZO YA SHUGHULI ZA
UJASIRIAMALI NA UBUNIFU HATUA AMBAYO ALIIELEZA KUWA ITASAIDIA SANA JITIHADA ZA SERIKALI
ZA KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI.
KWA HIYO AMEWATAKA WAHITIMU WA VYUO VIKUU NCHINI
KUBEBA DHANA YA UJASIRIAMALI KAMA WANAVYOFANYA VIJANA WENZAO WASOMI WA NCHI
NYINGINE ULIMWENGUNI ZIKIWEMO CHINA NA MAREKANI NA KUACHANA NA DHANA YA KUONA
SHUGHUILI ZA UJASIRIAMALI NI KAZI ZA MIKONO TU NA NI KWA AJILI YA WATU
WALIOKOSA ELIMU YA JUU.
AKIZUNGUMZA KATIKA MAHAFALI HAYO MWENYEKITI WA BARAZA
LA CHUO MHESHIMIWA SAID BAKARI JECHA ALIISHUKURU SERIKALI KWA KUKIUNGA MKONO
CHUO HICHO KWA HALI NA MALI KATIKA JITIHADA ZAKE ZA KUKIKIIMARISHA IKIWEMO
KUANZISHA SKULI MBALIMBALI CHUONI HAPO.
MWENYEKITI HUYO HATA HIVYO ALIIOMBA SERIKALI KUANGALIA
UPYA MASLAHI YA WATUMISHI WA CHUO HICHO AMBAYO ALIYAELEZA KUWA NI MADOGO
YAKILINGANISHWA NA MASLAHI KATIKA VYUO VIKUU VINGINE HALI AMBAYO INAKIFANYA
CHUO HICHO KISIWEZE KUSHINDANA KATIKA SOKO LA AJIRA.
WAKATI HUO HUO
MAKAMU MKUU WA SUZA PROFESA IDRIS AHMADA RAI AMESEMA KUWA KATIKA KUIMARISHA
UWEZO, CHUO KIMEWEZA KUFANIKIWA KUPATA RASILIMALI MBALIMBALI KUPITIA UTARATIBU
WA USHINDANI KWA WANATAALUMA WA CHUO HICHO KUPELEKA MIRADI NA TAFITI ZAO.
AKIZUNGUMZA KATIKA MAHAFALI HAYO PROFESA RAI
ALIBAINISHA KUWA CHUO KIMEWEZA KUSHINDA MIRADI MIWILI INAFADHILIWA NA SERIKLAI
YA NORWAY YENYE THAMANI SHILINGI BILIONI 3.3, DENMARK INAFADHILI MRADI MMOJA
WENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2.2, COSTECH MRADI MMOJA WENYE YA SHILINGI
MILIONI 90, SHIRIKA LA UMOJA MAENDELEO LA UMOJA WA MATAIFA- UNDP MRADI MMOJA
WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 44.3 NA UTURUKI INAFADHILI MRADI WA SHILINGI
MILIONI 80.
PROFESA RAIS ALIELEZA PIA KUWA CHUO HICHO KIMEFANYA
MABADILIKO YA MUUNDO WAKE, DIRA NA DHAMIRA PAMOJA NA MAMBO MENGINE.
KWA HIYO ALIBAINISHA MABADILIKO HAYO KUWA NI KUWEKA
MAADLILI MAKUU YA CHUO AMBAYO YATAONGOZA UTENDAJI WA CHUO KWA LENGO LA KUFIKIA
DIRA NA DHAMIRA ZA CHUO.
ALIYATAJA MAADILI MAKUU HAYO KUWA NI PAMOJA NA
KUKUBALI MABADILIKO NA KUYAPELEKA MBELE, KUFANYAKAZI KWA VITENDO, KUFANYAKAZI
KWA PAMOJA, UWAZI NA UKWELI, UHURU WA FIKRA/MAWAZO NA KUJIELEZA, KUZINGATIA
WAKATI NA UBORA, NIA NJEMA NA UZALENDO.
MAHAFALI HAYO YALIHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI
WALIKWEMO MAWAZIRI NA MAKATIBU WA WAKUU. MIONGONI MWA MAWAZIRI WAKUOHUDHURIA NI
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI MHESHIMIWA ALI JUMA SHAMUHUNA
No comments:
Post a Comment