WASOMI NCHINI
WAMETAKIWA KUUTATHMINI NA KUUCHAMBUA MFUMO WA ELIMU PAMOJA NA SERA YA ELIMU YA
MWAKA 2006, ILI KUONA IWAPO INAKIDHI MATARAJIO YA SEKTA YA ELIMU ZANZIBAR.
WITO HUO
UMETOLEWA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF
HAMAD, WAKATI AKIFUNGUA KONGAMANO LA ELIMU KUHUSU MFUMO WA ELIMU ZANZIBAR
KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA MAPINDUZI.
KATIKA KONGAMANO
HILO LILILOANDALIWA NA CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA CHWAKA, MHE. MAALIM
SEIFAMESEMA LICHA NA MAFANIKIO YA KUPIGIWA MFANO KATIKA SEKTA YA ELIMU, BADO
YAPO MATATIZO YANAYOHITAJI KUFANYIWA TATHMINI KWA LENGO LA KUYATAFUTIA UFUMBUZI.
AMETAJA BAADHI YA
MATATIZO HAYO KUWA NI PAMOJA NA UPUNGUFU WA VIFAA VYA KUFUNDISHIA, UKOSEFU WA
WALIMU WENYE SIFA, PAMOJA NA UPUNGUFU WA VITABU VYA KUSOMEA.
SAMBAMBA NA HILO,
MAALIM SEIF AMESEMA MFUMO WA ELIMU ULIOPO SASA UNAHITAJI KUFANYIWA MAPITIO, ILI
KUWAWEZESHA VIJANA KUJIAJIRI NA KUAJIRIA WAPOMALIZA MASOMO.
AMEWASISITIZA WASOMI
HAO KUENDELEA KUFANYA TAFITI NA KUTOA MATOKEO YAKE AMBAYO YATASAIDIA KUTATUA
MATATIZO YANAYOIKABILI SEKTA YA ELIMU.
KAIMU MKUU WA CHUO
HICHO IDDI HAJI MAKAME AMESEMA TAYARI CHUO HICHO KIMEANZA KUTOA SHAHADA ZA AINA
NNE IKIWEMO YA USIMAMIZI WA FEDHA.
SHAHADA NYENGINE
WANAZOTOA NI ICT NA UHASIBU, MANUNUZI NA USAMBAZAJI, PAMOJA NA HUDUMA ZA BENKI.
AMESEMA KATIKA
KUHAKIKISHA MAENDELEO YA CHUO HICHO WAMEAMUA KUWAFUNDISHA WALIMU WAO KATIKA
NGAZI YA UDAKTARI “PHD”, ILI WAWEZE KUTIMIZA LENGO LAO LA KUANZISHA SHAHADA WA
UZAMILI KATIKA KIPINDI KIFUPI KIJACHO.
No comments:
Post a Comment