Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim
Seif Sharif Hamad, amepongeza hatua ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali yakuweka
mikakati imara ya kukabiliana na matatizo yanayoikabili sekta ya elimu nchini.
Maalim Seif ametoa pongezi hizo katika hafla ya
uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la madarasa nane la skuli ya msingi
Tumbe, ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi
kikubwa kukabiliana na matatizo ya sekta hiyo yakiwemo ya upungufu wa vikalio
na vitabu vya kusomea.
aidha maalim seif amewapongeza wananchi wa
Tumbe na Micheweni kwa moyo wao wa kujitolea, na mwamko walionao katika
kuchangia huduma za elimu.
Amesema kuwa kwa kipindi kirefu Wilaya ya
Micheweni ilikuwa nyuma katika sekta sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo
elimu, na kwamba mwamko unaoonyeshwa na wananchi hao umesababisha watoto wengi
zaidi kupata fursa ya elimu.
Amewahimiza kushirikiana na walimu katika
malezi ya watoto ili kutunza maadili ambayo yanaonekana kuporomoka katika
maeneo mbali mbali nchini, sambamba na
kuwalinda dhidi ya marafiki waovu wanaoweza kuwaingiza katika vitendo viovu
vikiwemo utumiaji wa madawa ya kulevya.
Mapemba akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa
elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna, amesema kuwa miongoni mwa mikakati
yao ya kutatua kero za elimu ni pamoja kuanzisha miradi ya vitabu vya kusomea
ambapo wanafunzi wote hadi darasa la nne watapatiwa vitabu vitano kila mmoja
kuanzia mwezi Januari, 2014.
No comments:
Post a Comment