.
waziri wa biashara
viwanda na masoko ndugu nassor ahmed marui amesema kuwa ukuaji wa
biashara ni moja ya hatua muhimu katika
kukuza nakuendeleza uchumi wa nchi.
akizungumza na waandishi wa khabari katika ukumbi wa chuo
cha utalii marugubi amesema kuwa kuanzishwa
kwa tamasha la biashara
kutasaidia kuinua kiwango cha
ajira nakuitangaza nchi kiuchumi.
aidha waziri mazrui amefahamisha kuwa moja ya nyezo
muhimu yakuendeleza biashara nikuanzishwa kwa tamasha la biashara kwa ajili ya
uuzaji wa bidhaa mbali mbali
zinazozalishwa viwandani.
hata hivyo waziri huyo amefafanua kuwa lengo la tamasha
hilo mikuitangaza zanzibar kuwa kituo cha biashara sambamba nakuendeleza masoko
ya bidhaa hizo.
jumla ya makampuni 100 kutoka nchi mbali mbali zikiwemo
uturuki,indonesia,tanzania bara na wenyeji zanzibar yanatarajiwa kushiriki
katika tamasha hilo la biashara la siku sita.
No comments:
Post a Comment