tangazo

tangazo

Monday, December 23, 2013

MALIPO YA WATENDA WEMA

TUKUMBUSHANE || MAISHA NI KUSAIDIANA
Kijana mmoja maskini aitwaye Comfrey aliamua
kuuza bidhaa akipita nyumba kwa nyumba ili
aweze kujikimu kimaisha na kupata fedha za
kulipia ada ya chuo. Siku moja baada ya...
kuzunguka kutwa nzima akiuza bidhaa zake
alichoka huku njaa ikiwa inamuuma hivyo
akamua kwenda nyumba ya jirani ili aombe
chakula.
SOMA HII TAFADHALI!!
Baada ya kuugonga ule mlango alifungua binti
mmoja mzuri wa sura na umbo, kijana akaona
aibu na kuomba maji ya kunywa badala ya
chakula. Binti akagundua kuwa yule kijana ana
njaa pia hivyo akaingia ndani na kumletea glasi
ya maziwa, baada ya yule kijana kunywa
akamuuliza yule binti, " Dada ni bei gani
unanidai kwa maziwa haya?" Binti akamjibu, "
Sikudai chochote, Mama alitufundisha tusidai
malipo baada ya kutoa fadhila au msaada"
Comfrey akamjibu, "Nakushukuru sana kutoka
moyoni mwangu.... Asante dada" na kisha
kuondoka zake.
Wakati Comfrey anaiacha ile nyumba hakujisikia
kushiba tu ila pia moyo wake ulijawa na fura na
kumshuru Mungu na kuamini kuwa bado kuna
binadamu wenye upendo na wenye kujitolea
kwa wenzao. Akajisemesha kuwa amepata funzo
kubwa maishani mwake kupitia kwa yule dada
mrembo.
Miaka michache baadae yule dada akapatwa na
ugonjwa, madkatari wa hospitali alikolazwa yule
binti pale kijijini waliushangaa ule ugonjwa na
kuomba ahamishiwe katika hospitali kubwa
yenye madaktari waliobobea ili waweze
kumchunguza na kumpa matibabu sahihi.Baada
ya mgonjwa kuwasili pale hospitalini, Dokta
Comfrey akaitwa ili kumhudumia mgonjwa.
Alipolisikia jina la kijiji alikotokea yule
mgonjwa, akakikumbuka kile kijiji akasimmama
haraka na kwenda wodini akiwa amevalia
mavazi ya kidaktari na kakua tofauti na miaka
kadhaa iliyopita akaingia kumhudumia
mgonjwa.
Akaikumbuka ile sura ya yule binti mara moja.
Akarudi ofisini kwake na kuongea peke yake
kuwa lazima ahakikishe yule dada anapona kwa
kutumia uwezo wake wote wa kitaalamu
akishirikiana na wenzake.Kuanziasiku ile alimpa
matibabu kwa umakini chini ya uangalizi wa
ukaribu.
Baada ya jitihada za muda mrefu hatimaye
dokta Comfrey akaishinda vita kwa kushirikiana
na wenzake na binti akapona kabisa na dokta
Comfrey akaomba mhasibu wa hospitali ile
ampitishie bill kabla ya kwenda kwa mgonjwa.
Akaiangalia ile bill kisha akaandika kitu chini ya
ile bill na ikapelekwa kwa yule binti wodini
kwake. Yule binti akaichukua ile bill na kuogopa
kuifungua kwani alifahamu fika kwa jinsi
hospital ile ilivyona gharama kubwa,
ingemgharimu maisha yake yote kuilipa ile bill.
Hatimaye akaichukua ile bahasha ya bill na
kuifungua bili ikamtisha sana kabla ya kuona
kitu kimeandikwa mwisho wa ile bill na kusoma
yale maandishi yakiwa yameandikwa......., ” Bili
yote imelipwa kwa glasi moja ya
maziwa.” (Imesainiwa) Dkt. Comfrey.
Machozi ya furaha yakaufunika uso wake na
kisha akasali: “Asante Mungu,Upendo wako
umesambaa dunia nzima kupitia Mwanadamu
na mikono yake ........Amen.”
Kama umeipenda

No comments:

Post a Comment