RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA KUZINDULIWA KWA MITAMBO MIPYA NA YA KISASA YA
KIWANDA CHA UCHAPAJI NI UTEKELEZAJII WA DHAMIRA YA SERIKALI YA KULETA
MABADILIKO MAKUBWA KATIKA UCHAPISHAJI WA NYARAKA ZA SERIKALI NCHINI.
KWA HIYO AMEUTAKA UONGOZI NA WATUMISHI WA IDARA YA
UPIGAJI CHAPA NA MPIGACHAPA MKUU WA SERIKALI KUIFAHAMU VYEMA DHAMIRA HIYO YA
SERIKALI ILI UTENDAJI WAO UZINGATIE UTEKELEZAJI WA DHAMIRA HIYO
.
DK. SHEIN AMESEMA HAYO JANA WAKATI AKIZINDUA RASMI
JENGO JIPYA LA IDARA YA MPIGACHAPA MKUU WA SERIKALI PAMOJA NA MITAMBO MIPYA YA
KIWANDA CHA UCHAPAJI HUKO MARUHUBI MJINI UNGUJA IKIWA NI SEHEMU YA SHAMRASHAMRA
ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.
“TUMEFANYA HIVI KWA LENGO LA KUFANYA MABADILIKO
MAKUBWA KATIKA UCHAPISHAJI WA NYARAKA ZA SERIKALI NA TULIPOONA MSAADA
UNACHELEWA TULIAMUA KUTUMIA FEDHA ZETU WENYEWE”DK. SHEIN ALIELEZA.
AMEITAKA IDARA YA MPIGACHAPA MKUU WA SERIKALI
KUHAKIKISHA KUWA INATEKELEZA IPASAVYO MALENGO YA SERIKALI KATIKA NYANJA HIYO YA
UCHAPISHAJI HUKU IKIZINGATIA MAZINGIRA YA BIASHARA YALIYOPO SASA.
“LAZIMA MUWE TAYARI KUBADILIKA NA KUZINGATIA MAZINGIRA
YA KIBIASHARA YALIYOPO SASA KWA KUBADILI TABIA, MWELEKEO NA MTAZAMO WENU KATIKA
KUTENDA KAZI ZENU” DK. SHEIN ALIWAELEZA WATUMISHI WA IDARA HIYO.
ALIWAKUMBUSHA WATUMISHI HAO KUWA KAZI YAO YA KUCHAPA
NYARAKA ZA SERIKALI NA HATA ZA WATEJA WENGINE NI JUKUMU LINALOHITAJI UMAKINI,
UTULIVU NA USIRI MKUBWA HIVYO NI WAJIBU WAO KUZINGATIA MAZINGIRA HAYO YA KAZI.
“NYARAKA ZOTE ZA SERIKALI NI SIRI HADI PALE
ZITAKAPOTANGAZWA NA MAMLAKA HUSIKA HIVYO KAZI ZENU ZOTE NI SIRI HIVYO
ZINAHITAJI UMAKINI MKUBWA NA UTULIVU” ALISEMA DK. SHEIN.
ALILIELEZA TUKIO HILO LA UZINDUZI WA JENGO NA MITAMBO
HIYO MIPYA KUWA NI KIELELEZO CHA AZMA YA SERIKALI KUIREJESHA TENA HISTORIA YA
IDARA YA UCHAPAJI NCHINI.
KWA HIYO ALIUAGIZA UONGOZI WA IDARA HIYO KUUTANGAZIA
UMMA HUDUMA AMBAZO ZINAWEZA KUPATIKANA ILI KUVUTIA WATEJA IKIWA NI UTEKELEZAJI
WA LENGO LA SERIKALI LA KUIFANYA IDARA HIYO KUJIENDESHA KIBIASHARA HUKU
AKISISITIZA UONGOZI KUHAKIKISHA KUWA WATEJA WOTE WANALIPIA HUDUMA WANAZOPEWA
KWA WAKATI HATA KAMA NI WIZARA AU IDARA ZA SERIKALI.
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
ALITUMIA FURSA HIYO KUISHUKURU TIMU YA MAKATIBU WAKUU WAKIONGOZWA NA KATIBU
MKUU KIONGOZI KWA KUAFIKI RAI YAKE YA KUTAKA ENEO HILO LA MARUHUBI KUENDELEA
KUTUMIA KWA SHUGHULI ZA SERIKALI BADALA YA KUPEWA SEKTA BINAFSI.
KUFUATIA UAMUZI HUO ENEO HILO HIVI SASA LINATUMIKA
KAMA OFISI ZA IDARA YA MPIGACHAPA MKUU WA SERIKALI, BOHARI KUU YA MADAWA, OFISI
ZA MKEMIA MKUU WA SERIKALI NA MAABARA YA TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR –ZBS.
AKIZUNGUMZA KABLA YA KUMKARIBISHA MGENI RASMI WAZIRI
WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA MOHAMED ABOUD MOHAMED ALIELEZA KUWA BAADA YA
KUKAMILISHA AWAMU YA KWANZA TARATIBU ZINAFAYIKA KUANZA UTEKELEZAJI WA AWAMU YA
PILI YA MRADI HUO AMBAO ALIBAINISHA KUWA AWAMU HIYO ITAKAPOKAMILIKA KIWANDA
KITAKUWA NA UWEZO WA KUFANYA KAZI NYINGI ZAIDI.
ALISEMA KIWANDA HICHO KINA UWEZO WA KUKIDHI MAHITAJI
YOTE YA UCHAPISHAJI KWA SERIKALI NA AWAMU YA PILI ITAKAPOKAMILIKA MAGAZETI YA
SERIKALI YATAKUWA YAKICHAPISHWA KIWANDANI HAPO.
ALISISITIZA KUWA AZMA YA KUKIFANYA KIWANDA HICHO
KIJIENDESHE KIBIASHARA INAFANYIWA KAZI NA UONGOZI UTAFANYA KILA JITIHADA
KUHAKIKISHA MITAMBO HIYO INATUNZWA VIZURI NA KUDUMU KWA MIAKA MINGI IJAYO.
AKIELEZA HISTORIA YA KIWANDA CHA UCHAPAJI ZANZIBAR
WAZIRI HUYO ALISEMA KIWANDA KILIANZA WAKATI WA UTAWALA WA KIKOLONI MWAKA 1875
HUKO KATIKA JENGO LA BEIT EL AJAIB FORODHANI NA BAADAE KUHAMISHIWA KATIKA JENGO
JINGINE NYUMA YA MAKUBUSHO YA MFALME FORODHANI HADI MWAKA 1956 KILIPOHAMISHIWA
SAATENI AMBAKO KILIDUMU HADI MWAKA 2013 KILIPOHAMIA MARUHUBI.
HAFLA YA UZINDUZI WA JENGO HILO LA UCHAPAJI NA MITAMBO
MIPYA AMBAYO IMEGHARIMU KWA PAMOJA KARIBU SHILINGI BILIONI 4.2 ILIHUDHURIWA NA
VIONGOZI MBALIMBALI AKIWEMO MAKAMU WA PILI RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI.
No comments:
Post a Comment