PEMBA.
SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEWATAKA
WANANCHI kujivunia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika sekta ya elimu
nchini.
WITO HUO UMETOLEWA NA RAIS WA
ZANZIBAR Dk. ALI MOHD Shein WAKATI AKIZUNGUMZA katika sherehe za
ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Chasasa na Skuli ya Sekondari ya Wanawake ya
Utaani huko Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya mwaka 1964.
Amesema KUWA miaka 50 ya Mapinduzi
imeshuhudia mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu nchini ikiwa ni
utekelezaji wa moja ya lengo la Mapinduzi hayo ya kutoa elimu kwa kila
mwananchi bila malipo Na ubaguzi.
AIDHA DR SHEIN AMEBAINISHA kuwa azma
ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tOKEA wakati huo ni kuwapatia elimu watoto
wote hadi kikomo cha uwezo wao.
aMEwaeleza wananchi hao kuwa
anajivunia mradi huo mkubwa wa elimu uliojumuisha skuli 19 ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM kukamilika kabla ya muda uliopangwa wa
miaka mitano.
Katika mnasaba huo aMEsisitiza kuwa
ndio maana Serikali imekuwa ikiimarisha mazingira ya utoaji elimu nchini
ikiwemo uimarishaji wa maslahi ya walimu kama ilivyo kwa watumishi wengine wa
Serikali.
No comments:
Post a Comment