Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein AMEWATAKA VIJANA kuzingatia mafunzo ya msingi
ya mwenendo wa waasisi wa Mapinduzi YA
JANUARY MWAKA 1964.
Dk. Shein AMETOA WITO HUO alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa
matembezi ya Umoja wa Vijana wa CCM kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya mwaka
1964 huko Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Dk. Shein amebainisha kuwa Mapinduzi ya mwaka 1964 ambao
yaliwakomboa wananchi wa Zanzibar yaliwezekana tu kutokana na ujasiri,
mshikamano, moyo wa kujitolea na uzalendo WA WAASISI WAKE.
aMEsisitiza kuwa Mapinduzi ya mwaka 1964 yalikuwa halali
KUTOKANA NAKUwapa wananchi wote wa Zanzibar haki ya kujitawala na kuwaondoshea
ubaguzi.
AIDHA DR SHEIN ameutaka
Umoja wa Vijana wa CCM kuendelea kuyalinda Mapinduzi na Muungano AMBAVYO ndio
nguzo mbili kuu za msingi wa uhuru, amani na maendeleo yaliyopatikana katika
miaka 50 ya Mapinduzi na Muungano ifikapo Aprili, 2014.
Akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana
wa CCM Sadifa Juma Khamis aMEeleza kuwa madhumuni ya matembezi hayo ni kupeleka
ujumbe wa Mapinduzi kwa jamii ili kuleta hamasa kukumbuka mchango wa vijana
katika Mapinduzi hayo ambayo hayawezi kufutika katika historia ya ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment