tangazo

tangazo

Tuesday, December 31, 2013

mahakamani


wilaya ya wete.

Mahakama ya Wilaya ya Wete kisiwani pemba imemhukumu kwenda kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kijana Ahmad Albeto John  mkazi wa Chasasa Wete , baada ya kupatikana na kosa la wizi wa karafuu nusu pishi zenye thamani ya shilingi 3500 mali ya  ndugu Juma Hamad Juma .

 

Mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Rashid Machano Magendo , mwendesha mashtaka wa Polisi  Fakih ameiambia  mahakama kuwa kijana huyo alifanya kosa hilo disemba 26 majira ya saa 7.45 mchana ambapo mara baada ya kusomewa shitaka lake amekiri kufanya kosa  hilo.

 

Kwa mara ya kwanza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani disemba 27 na kukubali kosa lake na hivyo kupelekwa rumande na baada ya kurejeshwa na kukumbushwa  kosa linalomkabili alikubali kuiba karafuu hizo .

 

Awali mwendesha mashitaka mkaguzi wa polisi Fakih  aliiomba mahakama kutoea adhabu kali kwa mtuhumiwa  kutokana na vitendovya wizi kuongezeka katika mashamba ya wakulima wa karafuu .

No comments:

Post a Comment