tangazo

tangazo

Monday, December 23, 2013

PEMBA. Wananchi wa Mkoani Kisiwani Pemba, wametakiwa kuitunza miundombinu ya Maji safi na Salama

PEMBA. Wananchi wa Mkoani Kisiwani Pemba, wametakiwa kuitunza miundombinu ya Maji safi na Salama ,ikiwemo na Tangi la kusambazia maji liliopo Uweleni, ili liweze kukidhi mahitaji yaliokusudiwa .

Ushauri huo ulitolewa na Naibu Waziri wa Kilimo na Mali asili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mtumwa Kheri Mbarouk, huko Uweleni Mkoani Pemba, wakati alipokuwa akiweka Jiwe la Msingi la Tangi hilo ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema kuwa Maji ndio uhai kwa Binaadamu hivyo ni wajibu wa Wananchi kuyaenzi ili yaweze kuwasaidia wao na Vizazi Vijavyo , na kuthamini matunda ya Mapinduzi ya mwaka 1964 ambapo baada ya Mapinduzi hayo Muasisi wa Nchi hii alitangaza huduma hiyo kuwa bure kwa Wananchi wote.

Waziri huyo,aliwasihi Wananchi hao kulipia huduma hiyo ya Maji kwa wakati ili kuiwezesha Mamlaka ya Maji (ZAWA) kutowa huduma kwa urahisi kutokana na Mamlaka hiyo kuwa na mambo mengi ya kuwapatia huduma hizo Wananchi wa Zanzibar.

Aliwataka Wananchi kuacha tabia ya kumwaga maji ovyo kwani kufanya hivyo ni kuongeza gharama kwa Mamlaka na Serikali kwa ujumla .

Hata hivyo aliiomba Mamlaka hiyo, kupunguza mgao wa Maji sambamba na kupunguza mkato huo ili Wananchi waondokane na kero na usumbufu wa Maji .

Ujenzi wa Tangi hilo unafanywa na Kampuni ya Serengeti kutoka Tanzania na Mshauri Mwelekezi ni Kampuni ya C.LOTTI Kutoka Italy.

No comments:

Post a Comment