ZANZIBAR
IMELEZWA
KUWA TAIFA LOLOTE DUNIANI HALIWEZI
KUPIGA HATUA YA MAENDELEO ENDELEVU BILA YA RAIA WAKE KUWA NA UZALENDO.
HAYO
YAMEELEZWA NA MKURUGENZI WA MIPANGO NA
UENDESHAJI SERA WA CHAMA CHA WAKULIMA TANZANIA AFP NDUGU RASHIDI YUSSUF MCHENGA
KATIKA TAARIFA YAKE KWA VYOMBO VYA HABARI.
AMESEMA
UZALENDO NI KITU MUHIMU KWA TAIFA,JAMII NA HATA MTU MMOJA MMOJA NA ILI KUFIKIA
MAENDELEO NI LAZIMA KWA KILA MTU KUFUATA
UTARATIBU WA KANUNNI ZA NCHI NA HAKI ZA BINADAMU KWA MUJIBU WA SHERIA.
HATA HIVYO
AMESEMA NCHI NYINGI ZILIZOPIGA HATUA DUNIANI WATU WAKE WALIKUWA NA MOYO WA
KIZALENDO NA KUPELEKEA MKUBWA KUMUHESHIMU MDOGO NA MDOGO KUMUHESHIMU MKUBWA.
VILEVILE
AMETOLEA MFANO KWA NCHI KAMA SYRIA,MISRI,LIBYA NA SUDANI KUSINI WANANCHI NA
VIONGOZI WAO WALIKOSA UZALENDO NA KUAMUA KUVUNJA SHERIA NA KATIBA ZAO NA
KUPELEKEA KUZIHARIBU NCHI ZAO KIUCHUMI NA KIMAENDELEO KWA KUHARIBU MIUNDOMBINU
MBALI MBALI SAMBAMBA NA MALI ZA UMMA.
SAMBAMBA NA
HAYO AMESEMA KUNA HAJA YA KUTOLEWA ELIMU YA URAIA KWA WANANCHI WA TANZINIA
KUANZIA NGAZI YA SHEHIA,VITONGOJI,KATA NA HATA NGAZI YA TAIFA SAMBAMBA NA
KUPELEKA ELIMU HIYO MASHULENI ILI RAIA WAKE WAWE WAZALENDO.
No comments:
Post a Comment