tangazo

tangazo

Thursday, January 16, 2014

Maimamu Nchini Wametakiwa Kuwa Mfano Bora

Maimamu Nchini Wametakiwa Kuwa Mfano Bora Na Kiigizo Mbele Ya Jamii Kwa Kuendeleza Tabia Njema  Nakuepuka Maovu.
Wito Huo Umetolewa Leo Na Mkuu Wa Kitengo Cha Fat-Wa Katika Afisi Ya Mufti Wa Zanzibar Samahatu Sheikh Thabit Nouman Jongo Wakati Akifunga Semina Ya Siku Tatu Ya Maimamu Na Makhatibu Zaidi Ya 150 Wa Wilaya 6 Za Unguja Iliyofanyika Katika Ukumbi Wa Shirika La Utangazaji Zanzibar  Zbc Rahaleo Mjini Zanzibar.
Mada Mbali Mbali Zinazohusiana Na Mchango Wa Maimamu Na Makhatib Katika Kurekebisha Jamii Zimetolewa Katika Semina Hiyo.
Aidha Sheikh Thabit Amewasisitiza Maimamu Na Makhatibu Hao Kuwa Mfano Mzuri  Katika Jamii Yetu.

Semina Hiyo Iliyotayarishwa Na Afisi Ya Mufti Zanzibar Kwa Kushirikiana Na Shirika La World Islamic Coll Society La Libya.

No comments:

Post a Comment