Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia
Makosa yaliyokuwa yakimkabili ni mawili ambayo ni kushawishi watu kutenda kosa, pamoja na kutoa matamshi yanayoumiza imani ya dini nyingine.
Hakimu wa kesi hiyo Mary Moyo amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haukujitosheleza hivyo mahakama hiyo imemwachia huru na rufaa iko wazi endapo upande wa mashitaka hautaridhika na hukumu hiyo.
Shehe Ponda alikuwa anakabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kushawishi wa imani wa dini ya Kiislam nchini kutenda makosa,ambayo anadaiwa kutenda Ogost 2013,
Upande wa wa Serikali katika kesi hiyo uliwakilishwa na wakili wandamizi wa Serikali Berdard Kongola,Sunday Hrela na George Mbalasa wakati wa upande wa Mshtakiwa unawakilishwa Wakili Juma Nasoro ,Abubakal Salim na Bartholomeo Tarimo.
Awali kesi hiyo ilipangwa kutolewa hukumu 19 ya mwezi wa kumi ambapo shauri hilo lilihairishwa hadi Novemba 18 na kuhairishwa tena mpaka kutolewa hukumu hiyo jana,
tangazo
Monday, November 30, 2015
CCM YAKANUSHA TAARIFA ZA MITANDAONI KWAMBA IMEKUBALI KUMKABIDHI MAALIM SEIF IKULU
Na Maelezo Zanzibar 30/11/2015
Chama cha Mapinduzi CCM kimekanusha Taarifa iliyozagaa katika Mitandao ya Kijamii kwamba Chama hicho kimeridhia aliyekuwa Mgombea wa Urais wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akabidhiwe nchi kuiongoza kwa miaka mitano.
Akikanusha Taarifa hiyo mbele ya Waandishi wa Habari Afisini kwake Kisiwandui Naibu Katibu Mkuu wa CCM Vuai Ali Vuai amesema taarifa hiyo ni uzushi uliotungwa ili kuwatia taharuki WanaCCM na Wananchi kwa Ujumla.
Amesema toka kusambaa kwa Taarifa hiyo Jana amekuwa akipigiwa simu na Watu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kujua ukweli wa Taarifa hiyo hasa ikizingatiwa kuwa ilidaiwa kusainiwa na Naibu huyo.
“Huu ni Uzushi Mkubwa na kwamba unafaa kupuuzwa maana hauna lengo jingine zaidi ya kuwagawa WanaCCM” Alismema Vuai.
Amesema kilichopo nikwamba CCM inajiandaa kwa ajili ya uchaguzi wa Marejeo kama ambavyo Tume ya Uchaguzi ilitangaza kuufuta Uchaguzi na hivyo kurudiwa upya.
Aidha Vuai amesema kuwa tayari wamewasiliana na Wanasheria wao pamoja na wataalamu mbalimbali ili kuwabaini waliohusika kusambaza Taarifa hizo na kuwapeleka katika Vyombo vya Sheria.
“Tumeshafanya mawasiliano na Wataalam wetu na tukiwabaini Sheria ya Makosa ya mtandao itachukua nafasi yake” Alisema Vuai.
Katika taarifa hiyo iliyosambaa na kudai kusainiwa na Vuai Ali Vuai ilisema kuwa Chama cha mapinduzi kimeridhia na kukubali kumpa nchi Maalim Seif Sharif kupitia chama chake cha Cuf kuwa ndio rais wa uchaguzi ulopita,na yeye ndio atakayeongoza serikali ya umoja wa kitaifa.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa CCM imekubali kushirikiana na maalim Seif katika kuongoza nchi chini ya serikali ya umoja wa kitaifa na kukubali kutoa makamo wa kwanza wa rais na nusu ya mawaziri.
Vuai amerejea kauli yake kuwa mazungumzo yanayofanywa na Viongozi wa Kitaifa kwa kushirikiana na Viongozi Rais Wastaafu wa Zanzibar hayawezi kubatilisha maamuzi ya Tume ya kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliopita.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

Sunday, November 29, 2015
ZANZIBAR KUWA MWENYEJI KUANDAA MASHINDANO YA KAGAME 2016
Na: Abubakar Kisandu, Zanzibar.
Chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) kimethibitisha kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya vilabu kwa ukanda wa afrika mashariki na kati ya KAGAME CUP, ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi wa 7 mwakani.
Mkurugenzi wa ufundi wa ZFA Massoud Attai amethibitisha kuwa Zanzibar watakuwa wenyeji kuandaa mashindano hayo ambapo walipelekea maombi yao kwa CECAFA kwa kutaka kuwa wenyeji na CECAFA wakawakubalia kuandaa wao mwakani (2016) na kwasasa maandalizi yameshaanza maana Baraza la Michezo tayari wameshapokea barua ya kuwa Zanzibar ni wenyeji mwakani .
“Nikweli Zanzibar tumepeleka maombi yetu kwa CECAFA kuwa mwenyeji na tayari wameshatukubalia, kwaiyo yatafanyika mwakani bila ya wasi wasi wowote”. Alisema Attai.
Katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika ndani ya visiwa vya zanziabar ambapo timu ya Mafunzo na JKU ambao ndio bingwa na makamo bingwa wa ligi kuu ya Zanzibar msimu wa 2014-2015 ndio watakaowakilisha zanzibar, lakini pia hii si mara ya kwanza kwa Zanzibar kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ambapo waliwahi kuwa wenyeji miaka mingi sana kama mwaka 1985 na 1990 na mashindano yakachezwa kwa utulivu wa hali ya juu na mashindano yakanoga.
Thursday, November 26, 2015
Jaji Mkuu awafunda waandishi habari za mahakama.
Waandishi wa habari za mahakama wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kushindwa kuelewa baadhi ya maneno ya kitaalamu yanayotumiwa na majaji, mahakimu na wanasheria wakati wa kuendesha kesi na hukumu.
Akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari za mahakama jijini Dar es Salaam jana, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande, alisema mahakama kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari imeandaa mafunzo hayo ili kuwasaidia kuelewa maana ya maneno muhimu ili kuondoa upotoshaji wakati wa kuripoti habari za mahakama.
Alisema wakati wa mafunzo hayo, waandishi wa habari wataelimishwa juu ya maneno ya kisheria yanayotumika mara kwa mara mahakamani pamoja na taratibu ili kuboresha habari na taarifa za vyombo vya habari nchini kuhusiana na mashauri mbalimbali yaliyopo mahakamani.
“Habari zilizotolewa na vyombo vya habari juu ya matukio ya mahakama na kesi unalazimu niongelee juu ya uandishi wa habari taswira au unaolenga kuhukumu kwa macho ya jamii (trial by media)," alisema.
Jaji Chande alisema habari kama hizo zina muhukumu mshitakiwa kabla hajatiwa hatiani kihalali kwani atakuwa ameshahukumiwa mbele ya mahakama ya maoni ya jamii na kwamba kwa kufanya hivyo waandishi watakuwa wamejivika majoho ya jaji au hakimu jambo ambalo si sawa.
Alitoa mfano wa vichwa vya habari habari zinavyowatia hatiani watuhumiwa ni kama; ‘Tanesco wakamata mwizi wa umeme, mahakama ya rufani yamwachia jambazi sugu’.
“Habari zinazohukumu na jamii itamtazama hivyo mhutumiwa hata kama jamhuri au serikali imeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha au kuthibitisha kesi bila shaka yoyote ambayo kisheria ni jukumu lao na si la mshtakiwa.
Aidha, Jaji Chade alisema kumekuwa na habari za mahakamani ambazo huandikwa zikiishia hewani bila kufanya mwendelezo wake jambo ambalo huwafanya wananchi wasielewe kinachoendelea au hatma ya kesi husika.
"Wasomaji wamekuwa wakisubiri kuona mwendelezo wa habari za mahakamani lakini waandishi wengi wamekuwa wakitoa taarifa nusunusu au kutomaliza kabisa," alisema.
CHANZO: NIPASHE

Wednesday, November 25, 2015
“TUSIHARIBU TIMU ZOTE , TUSAIDIENI SISI SAND HEROES”
“TUSIHARIBU TIMU ZOTE , TUSAIDIENI SISI SAND HEROES”
Na: Abubakar Kisandu, Zanzibar.
Timu ya taifa ya Zanzibar ya soka la ufukweni ( Zanzibar Sand Heroes ) ipo kwenye mazoezi makali ya kujiandaa kwenye mashindano beach soccer yanayotarajiwa kufanyika katikakati ya mwezi ujao nchini Kenya.
Timu hiyo inajifua kwenye fukwe za Bububu bamboo yenye jumla ya wachezaji 13 ambao 7 walikuwemo kwenye timu ya taifa ya Tanzania ya beach soccer.
tumefanikiwa kuzungumza na kocha msaidizi wa timu hiyo ambae ni Fahad Khamis na hapa akizungumzia mazoezi yanavokwenda napia akiamini watafanya vizuri kwenye mashindano yaliopo mbele yao ambapo akiwataka wadau wa michezo wajitokeze kuisaidia timu hiyo.
“ Mazoezi yanaendelea vizuri hapa Bamboo, tulianza mazoezi magumu na kwasasa tunafanya madogo madogo tu, timu yangu nzuri mana najivunia ninawachezaji 7 wanaocheza timu ya taifa, nawaomba wadau wa michezo watusaidie kwa hali na mali ili tukawakilishe vyema huko Kenya”. Alisema kocha msaidizi wa Sand Heroes.
Zanzibar sand Heroes ilipata mualiko kwenda nchini Kenya kwenye mashindano yanayofanyika kila mwaka , ambapo mwaka huu yanatarajiwa kufanyika 16-20 mwezi Disemba kwenye Fukwe za Buntwani, kata ya Kilifi, mji wa Malindi nchini humo.

BAUSI ASEMA ZANZIBAR HEROES HAINA UMOJA NDO MAANA TUMEPIGWA ALIZOPIGWA REAL MADRID
Baada ya kuchezea kipigo cha mabao 4-0 kwa timu ya taifa ya Zanzibar walipopigwa Uganda kwenye mashindano ya CECAFA CHALENJI CUP huko Ethiopia , Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Salum Bausi amesikitika kwa kipigo hicho huku akiwabebesha lawama kamati inayosimamia soka pamoja na Benchi la Ufundi kwa kusema kuwa timu imekosa nidhamu na ndio maana ikapata aibu hiyo.
“ Timu imekosa nidhamu wachezahji wanacheza tu ndo maana tunafungwa kama hivi, hatujawahi kufungwa mabao 4-0 kwa miaka ya hivi karibuni, Uganda inatufunga?, wakati sisi mara nyingi tunawafunga. Alisema Bausi.
Aidha Bausi alisikitishwa sana kwa kuachwa kocha wa makipa Zanzibar ambae ni Saleh Machupa na timu kwenda huko Ethiopia bila ya kocha wa Makipa.
“Imeniuma sana kocha wa makipa kaachwa hapa Zanzibar , timu haina kocha wa makipa!, ni aibu sana wamejazana makocha watatu tu huko wakati kocha wa makipa wamemuacha, ni muhimu angeenda mana leo kashapewa kadi nyekundu Mwadini, sijui itakuaje mchezo wa mwisho na sijui nani atakaa na makipa kuwajenga kisaikologia!, yani viuongozi wapo kama washamba washamba tu mana wao lazima wasafiri , yani inauma sana”.
Hata hivyo kocha huyo amesema kina Moroco na Canavaro walikuwa wapumzike tu na wamejitia aibu kwenda huko Ethiopia.
“ Kocha Hemed Morocco alikuwa atulie tu na kupumzika, mwenzake Mkwasa yupo nyumbani katulia, tumefungwa 7-0, siku ya 2 wamekuja Zanzibar na kuungana na wenzao kwenda Ethiopia, hawezi kumudu timu maana hajawahi kuifundisha hata siku moja mazoezi, yani hii Zanzibar majanga tu, na hata Nadir alikuwa nae apumzike tu bora lakini ndo mambo ya Zanzibar haya”. Alisema kocha Bausi.
Kocha Salum Bausi aliinoa Zanzibar Heroes kwenye mashindano hayo mwaka 2012 nchini Uganda na kufanikiwa kunyakua ushindi wa tatu , lakini pia aliifundisha tena mwaka 2013 mashindano yaliofanyika nchini Kenya ambapo Heroes ilitolewa kwenye makundi na pia mwaka huo Bausi aliwaacha nyota 3 muhimu Zanzibar na Tanzania ambao ni Nadir Haroub, Agrey Moris na Abdi Kassim “Babi” na kuwachukua walinzi walichipukia kwa wakati huo Mohd Fakih (Sosha) ambae kwasasa anacheza Simba pamoja na Mlinzi Shaffi Hassan.
Timu ya taifa ya Zanzibar imesafiri na makocha watatu, akiwemo kocha mkuu Hemed Suleiman (Morroco), na makocha wasaidizi wawili Malale Hamsini Keya na pamoja na Hafidhi Muhidin, wakati kocha wa makipa aliedima siku zote za mazoezi aliachwa na hakwenda Ethipia ambae ni Saleh Machupa pia walinda mlango walikwenda huko ni wawili tu ambao ni Mwadin Ali pamoja na Mohammed Abrahman wakati kipa Mohd Ali wa Tanzania Prisons aliachwa, sasa mchezo wa mwisho kati ya Zanzibar heroes na Kenya hakuna kipa wa akiba baada ya leo kupigwa kadi nyekundu kipa nambari moja Mwadin.
Swali linakuja nani atakuwa kipa mbadala wa Mohammed Abrahman kwenye mchezo wa mwisho maana kipa waloenda 2 tu na Mwadin ana kadi nyekundu?. Lazima mchezaji wa ndani awe mbadala wa kipa Mohammed Wawesha.
VIPODOZI FEKI VYAKAMATWA BANDARINI ZANZIBAR.
Maafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakifungua moja ya Boxi lenye Vipozi vyenye Kemikali ambavyo vimepigwa marufuku kutumika duniani baada ya kuvikama Bandarini vikitokea Marekani na Italy.
Baadhi ya Vipozi vyenye Kemikali ambavyo vimepigwa marufuku kutumika duniani vikiwa vimetolewa katika Maboxi ambayo yalitumika kuviihifadhi. Vipodizi hivyo Vinasubiri kuteteketezwa na Maafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Na Miza Kona Maelezo Zanzibar 25/11/2015
Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi imekamata vipodozi haramu katika Bandari Kuu ya Malindi Zanzibar ambavyo vimepigwa marufuku kuingizwa nchini.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko Ofini Mombasa Mkaguzi wa Bodi hiyo Nassir Buheti amesema vipodozi hivyo haramu vimepigwa marufuku kuingizwa nchini kutokana na kuwa Viambata vyenye kemikali vinavyoweza kuleta madhara Mtumiaji ikiwemo Kansa, Ulemavu pamoja na uharibifu wa ngozi.
Amevitaja vipodozi hivyo kuwa ni pamoja na Movet Crèame kutoka Itali na Medical Fade Crème kutoka Marekani vyenye uzito wa tani tatu na kuhifadhiwa katika Makontena yaliyochanganyishwa na vitu vingine bandarini hapo.
Aidha amefahamisha kuwa vipodozi vya aina Movet Cream hutumika kwa matibabu ya ngozi lakini inahitajika kupata ushauri wa daktari kabla ya kutumia ili kuepukana na madhara.
Mkaguzi huyo ameeleza mawakala wa vipodozi hivyo wamedai kuwa havikukusudiwa kuingizwa nchini jambo ambalo vipodozi vya aina hiyo vimepigwa marufuku dunia nzima.
Amesema Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi inafanya juhudi ya kutaka kudhibiti kuingiza bidhaa haramu nchini hivyo inaomba mashiriano makubwa kwa jamii ili iweze kufikia lengo lililokusudiwa.
Aidha Mkaguzi Buheti amesema Sheria inasema si ruhusa kuingiza, kuuza, kusambaza vipodozi haramu na kuwataka wafanyabiasha wa vipodozi, dawa pamoja na Chakula kutofanya udanganyifu wa bidhaa wanazoingiza ili kuepuka madhara yasiongezeke nchini.

Tuesday, November 24, 2015
WARAKA WA ZATU JUU YA HOJA YA KUANZISHWA KWA KODI YA ELIMU “EDUCATION LEVY” KISHERIA ZANZIBAR
1.0
UTANGULIZI
Moja kati ya mambo makubwa na adhimu
ya kujivunia Wazanzibari, ni uwamuzi uliochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, tarehe 23
Septemba 1964, wa kutoa elimu kwa wananchi wake wote bila ya malipo, SERA YA
ELIMU BURE KWA WOTE. Sera hii ilikuwa ni mfano kwa wengine hapa Afrika, ambapo
baadhi ya mataifa yaliiga. Mfano wa mataifa hayo ni Mauritius. Pamoja na
kuyumba kwa uchumi wa taifa letu, lakini Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
wakati wote imekuwa ikiisisitiza na kuin’gan’gania sera ya elimu bure kwa wote.
Bila shaka imekuwa ikifanya hivi kwa kuamini kuwa, elimu sio tu ni haki ya
msingi kwa kila raia, bali pia ndio msingi mkuu wa maendeleo ya jamii yetu.
Chama cha Walimu Zanzibar kwa dhati, kinaipongeza sana serikali yetu kwa hatua
hii ya kimaendeleo na kimapinduzi.
Lakini pamoja na nia njema na nzuri
ya serikali yetu, mabadiliko ya kiuchumi
na kijamii, yamepelekea nia njema hii, kuwa na changamoto kubwa na nyingi,
kiasi cha kuathiri matokeo ya jumla ya nia yenyewe. Sio siri hata chembe, kuwa
ubora wa elimu yetu umeshuka, tena umeshuka sana. Hali hii ya kushuka kwa ubora
wa elimu, imetokea wakati taifa likiwa linapiga hatua kubwa, ya mafanikio ya
kusambaza huduma ya elimu katika nchi yetu. Kwa sasa hakuna mwanafunzi
anaepaswa kutembea, masafa marefu ya zaidi ya kilomita tatu kufuata skuli. Kwa
maneno mengine inawezekana kusema kuwa taifa limefanikiwa kuongeza idadi ya
skuli, na wanafunzi wanaosoma, lakini ongezeko hilo haliendani sambamba na
ongezeko la ubora wa elimu yenyewe.
Inakubalika kuwa katika elimu
kinachohitajika, sio wingi wa idadi bali ni ubora, hivyo haitoshi kabisa
kuridhika na wingi pasina kuangalia ubora wa elimu itolewayo.
Sababu kubwa ya kushuka kwa kiwango
cha elimu nchini, ni gharama kubwa za elimu ambazo zimekuwa zikipanda siku hadi
siku, hivyo ni wakati sasa wa kubuni njia na mbinu mpya za namna ya kuigharamia
elimu yetu.
Waraka huu unakusudia kuwasilisha
hoja ya Chama cha Walimu Zanzibar ZATU juu ya kuanzishwa rasmi kwa kodi ya
elimu “Education levy” ili jaza pengo la gharama zinazohitajika za elimu nchini
mwetu.
2.0
USULI WA TATIZO
Elimu katika nchi yoyote ni mali ya
umma, hivyo ni wajibu wa umma kuigharamia. Taifa kwa ujumla wake, ni lazima
libebe dhima ya kuhakikisha kuwa, gharama za elimu nchini hazikwamishi
upatikanaji wake. Elimu lazima ipatikane kwa wote, na kwa ubora wa hali ya juu.
Kigezo sahihi cha ubora wa elimu katika nchi, kiwe ni ubora wa elimu katika
skuli za umma, ambazo kila mmoja ana uwezo wa kusoma. Hata pale zinapokuwepo
skuli binafsi, jambo ambalo kwa sasa haliwezi kuepukika, kusijengeke mazingira
ya kuwa, mwananchi akitaka elimu bora kwa mtoto wake, iwe ni lazima ampeleke
katika skuli ya binafsi. Skuli binafsi ziwe ni kwa utashi wa mambo ya ziada tu
na sio ubora wa elimu.
Katika makubaliano ya Dakkar ya
Mkutano wa Dunia juu ya elimu, ilikubalika kuwa nchi maskini zisaidiwe kuona
kuwa kila taifa linafikia lengo la elimu kwa wote kwa mataifa yenye uwezo
kuwatoa fedha za kutosha kwa shughuli za elimu. Pia ilielekezwa kuwa, nchi
zenyewe maskini zitenge asilimia 4-6 ya pato lote la taifa au asilimia 15 – 20
za bajeti zake kwa ajili ya masuala ya elimu, kulingana na ipi kati ya hiyo ni
bora zaidi.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
kipindi cha miaka mitano iliyopita imekuwa ikiweka elimu kuwa moja ya
vipaumbele na kuwa bajeti ya elimu imekuwa ni wastani wa asilimia 20 ya bajeti
yote ya serikali inayopangwa, japokuwa kiwango kitolewacho na hazina huwa
pungufu ya hiyo asilimia 20.
3.0
UCHANGANUZI WA TATIZO
Kama ilivyoelezwa hapo juu kuwa
pamoja na nia ya serikali yakuwapa elimu watu wake bila ya malipo kumekuwa na
changamoto nyingi zinazokwaza azma hiyo. Hoja za hapa chini ni miongoni mwa
hoja za kuonyesha changamoto hizo.
3.1 Hoja
ya ufinyu wa Bajeti vis as vis mahitaji:
Japokuwa serikali hutenga asilimia
ishirini (20%) ya bajeti yake ya matumizi kila mwaka kwa ajili ya elimu nchini,
lakini kiwango hiki kinaonekana kuwa ni kidogo sana kukidhi mahitaji ya elimu
yetu. Asilimia kubwa ya bajeti ya elimu inayotengwa na serikali huwa ni kwa
ajili ya matumizi ya kawaida na mishahara ya walimu ambao bado wanalipwa
mishahara duni na isiokidhi mahitaji yao. Ithibati ya hayo ni hii inayoonyeshwa
na jedwali hapa chini
S/N
|
MWAKA
|
BAJETI YA SHUGHULI ZA KAWAIDA
|
BAJETI YA MAENDELEO
|
1.
|
2012/13
|
7I,050,000,000/-
|
5,100,000,000/-
|
2.
|
2013/14
|
80,200,000,000/-
|
5,350,000,000/-
|
3.
|
2014/15
|
86,201,500,000/
|
3,300,000,000/-
|
CHANZO; HOTUBA ZA
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI......
(2012-2015)
Sote
tunajua kuwa elimu ni uwekezaji na ndio uwekezaji wa msingi katika taifa. Kwa
hivyo ni dhahiri kuwa kwa uwekezaji huu tuko mbali na kufika huko tunakostahili
kufika. Kwa ufupi ni kuwa pamoja na kuwa serikali hutenga asilimia ishirini ya
bajeti yake kwa mwaka kwa ajili ya elimu nchini kiwango hicho ni kidogo sana,
kwani sehemu kubwa ya fedha hizo huwa ni kwa matumizi ya kawaida na ni chache
sana zinazowekezwa katika maendeleo ya elimu.
3.2 Uchache wa fedha
halisi zinazopatikana kutoka hazina
Hoja ya pili ni uchache wa fedha
zinazotolewa na hazina kwa wizara pamoja na kuwa Baraza hili limepitisha Bajeti
yake. Wizara ya elimu imekuwa ni moja ya wizara zinazopokea fedha pungufu za
bajeti yake kutoka hazina. Hali hii inapelekea kwa kazi nyingi zinazopangwa
katika sekta ya elimu kukwama. Jedwali hapa chini linatoa taswira ya hali
halisi;
S/N
|
MWAKA
|
TAASISI AU IDARA
|
ASILIMIA YA FEDHA ZA MAENDELEO
ZILIZOPATIKANA
|
ASILIMIA YA FEDHA ZA MATUMIZI YA KAWAIDA
ZILIZOPATIKA
|
1.
|
2012/13
|
WIZARA
ELIMU
|
80.3%
|
-
|
2.
|
2012/13
|
“
|
59.2%
|
95.3%
|
3.
|
2013/14
|
“
|
31.0%
|
83.7%
|
CHANZO; HOTUBA ZA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI...... (2012-2015)
Kuna baadhi ya maeneo ya wizara
ambayo hukosa fedha kwa kati ya zaidi ya themanini asilimia 80% hadi asilimia
mia moja (100%). Mifano halisi ni hotuba ya bajeti ya 2014/15, ambayo
ilionyesha upatikanaji wa fedha kutoka hazina kwa miradi mbalimbali. Ifuatayo
ni miradi ikiwa na asilimia ya bajeti iliyopatikana kutoka hazina kwenye
mabano;
4
Mradi wa uimarishaji wa Chuo kikuu cha Taifa SUZA (43%)
5
Mradi wa uimarishaji elimu ya msingi (18.0%)
6
Mradi wa ujenzi wa Chuo cha Kiislamu ( 0%)
7
Mradi wa uimarishaji wa Elimu mbadala na amali (15%)
8
Mradi wa uimarishaji wa elimu ya lazima (35%)
9
Mradi wa uimarishaji wa elimu ya maandalizi (13%)
CHANZO; HOTUBA YA WAZIRI WA ELIMUNA MAFUNZO YA AMALI ....(2014/15)
3.3 Utegemezi na
upatikanaji usio muafaka wa fedha za wafadhili
Zanzibar kama zilivyo chini nyengine
zinazoendelea zimepewa ahadi ya uhakika wa misaada ya fedha kutoka nchi
zilizoendelea na mashirika ya kimataifa kwa ajili ya kuendeleza elimu na
kufikia malengo ya maendeleo ya melenia, na hasa lengo la elimu kwa wote.
Lakini kuna ushahidi kuwa matarajio ya serikali ya kupata fedha hizo huwa
hayafikiwi. Katika hotuba za bajeti kwa karibu miaka mitatu iliyopita
imeonyesha kuwa kile kiwango kinachopangwa na kutarajiwa kutoka kwa wafadhili
hupatikana chini ya makisio
S/N
|
MWAKA
|
ENEO LILILOLENGWA MSAADA
|
MSHIRIKA WA MAENDELEO
|
FEDHA ZA MAENDELEO ZILIZOTARAJIWA
|
FEDHA ZILIZOPATIKA
|
1.
|
2012/13
|
i)
Mpango
wa maendeleo ya elimu
ii)
Uimarishaji
elimu ya maandalizi
iii)
Uimarishaji
wa elimu ya msingi
|
AfDB, BADEA, WB SIDA ,
UNESCO na UNICEF
UNICEF
SIDA na
UNICEF
|
419,200,000/-
4,969,938,000/-
|
21,585,548,444/-
(45%)
51,264,700/- (11%)
359,576,800/- (08%)
|
2.
|
2012/13
|
i)
Uimarishaji
SUZA
ii)
Uimarishaji
elimu mbadala na amali
iii)
Uimarishaji
elimu ya maandalizi
|
BADEA
AfDB
UNICEF
|
4,332,959,000/-
1,994,098,000/-
491,200,000/-
|
594,833,392/- (13.7%)
1,230,070,040/- (61.7%)
23,357,300/- (22.9%)
|
3.
|
2013/14
|
iv)
Mpango
wa maendeleo ya elimu
v)
Uimarishaji
wa elimu ya msingi
vi)
Uimarishaji
elimu mbadala na amali
|
AfDB, BADEA na WB
Sida ,UNICEF UNESCO GPE na
USAID
AfDB
|
0
7,212,032,000/-
1,529,906,000/-
|
6,223,274,932/- (20.6%)
2,881,271,948/- (40.0%)
93,321,600/- (15%)
|
CHANZO; HOTUBA ZA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI...... (2012-2015)
3.4 Uwepo
wa kodi mbalimbali ambazo zimekosa uratibu mzuri wa matumizi yake
Kwa sasa kuna kodi na michango
mbalimbali rasmi na isiyo rasmi kwa ajili ya kuendesha elimu nchini. Hali hiyo
ya kuwa na michango iliyo rasmi na ile ambayo haipo rasmi na wala mahesabu yake
hayako wazi, inaweza kupelekea upotevu wa rasilimali za umma na kuwaruhusu wale
wasio waaminifu kujinufaisha kwa fedha hizo.
Kwa upande wa michango rasmi ni
pamoja na kodi zifuatazo:
i)
Kodi ya maendeleo ya ujuzi “skill development levy” ambayo
huwa inakusanywa kutoka kwa waajiri wote wakubwa na wadogo wa sekta ya umma na
sekta binafisi
ii)
Mchango wa madawati kwa wasafiri wanaosafiri kupitia bandari
za Zanzibar.
Kwa upande wa michango isiyo rasmi ni
pamoja na michango ifuatayo:
i)
Michango ya wazazi maskulini ambayo pamoja na kuwepo kwa
muongozo juu ya michango hii kila skuli imekuwa na kiwango chake ambacho kamati
ya wazazi huwa wanakubaliana
ii)
Michango ya walimu wenyewe wanayoitoa kwa hiyari kwa ajili ya
shughuli mbalimbali za kiskuli.
iii)
Michango inayochangishwa na baadhi ya taasisi za elimu nchini
mfano michango ya wanafunzi inayokusanya na Taasisi ya Sayansi na teknolojia ya
Karume na Chuo cha Kiislamu
3.5 Umuhimu wa kuwa na
fedha za kutosha kwa ajili ya mahitaji na maendeleo ya elimu
Hoja nyengine ya kuwa na kodi ya
elimu, ni haja na umuhimu wa kuwa na fedha za kutosha, kwa
ajili ya maendeleo na mahitaji ya elimu nchini. Kutokana na fedha kidogo isiokidhi
mahitaji, walimu wamekuwa ndio waajiriwa wa umma wanaodai fedha nyingi
serikalini kuliko waajiriwa wengine wowote. Mfano halisi ni kuwa Walimu wanadai
kutoka kwa mwajiri wao malimbikizo ya posho ya likizo, huku wengine wakifika
kusubiri fedha hizo kwa miaka mitatu, muda ambao mzunguko wao wa kupewa tena
fedha hizo unakuwa umefika.
Zaidi ya fedha za likizo walimu pia
wanadai fedha za stahiki mbalimbali kutoka kwa mwajiri zikiwemo stahiki za
safari za kikazi, malimbilikizo ya madeni ya mishahara baada ya kurudi
masomoni. Madai ya stahiki baada ya kushinda kesi mbalimbali na kadhalika.
3.6 Utekelezaji wa
sera ya elimu
Hoja nyengine ya kusisitiza kuwepo
kwa kodi ya elimu nchini ni utekeleza wa sera ya elimu ya mwaka 2006. Katika
sera ya elimu iliyotajwa hapo juu, imeelekezwa kuwa kutaanzishwa kwa kodi ya elimu nchini. Sura
ya 9, Kifungu nambari 921 kinaeleza “Mfuko wa elimu utaanzishwa kisheria”
3.7 Nia ya serikali ya
kutoa elimu bila malipo kwa wananchi wake ili kuwapa fursa sawa
Hoja
nyengine ni nia ya serikali kuendelea kutoa elimu iliyo bora kwa wananchi wake
4.0
MAPENDEKEZO
Kutokana na hali ya hapo juu, Chama
cha Walimu Zanzibar Kinapendekeza yafuatayo:
i)
Serikali kufanya tathmini ya kina, juu ya mahitaji halisi ya
gharama za utoaji wa elimu nchini, ili kujua kiasi halisi cha fedha
kinachohitajika, badala ya hali ya sasa ambapo inaonekana kuwa serikali
inatumia kulingana na kinachopatikana na sio kinahitajika.
ii)
Kufanya tathmini ya kina juu ya michango mbalimbali iliyopo
sasa kama vile michango ya madawati, kodi ya maendeleo ya ujuzi, pia michango
inayokusanywa na vyuo, ili kujua ni kwa kiasi gani michango hii imekuwa
ikigharamia elimu.
iii)
Kuandaa muswaada wa sheria utakaolenga kuikusanya kodi na
michango yote chini ya mfuko mmoja utakaokuwa na wigo mpana zaidi na nguvu
zaidi ili kukidhi mahitaji ya kifedha zinazohitajika katika elimu.
iv)
Kuanzisha kodi ya elimu kisheria ambayo itakuwa na udhibiti
wa Ofisi ya Rais kodi ambayo italenga kubeba gharama za elimu nchini.
Naomba
kuwasilisha
Monday, November 23, 2015
MSAADA WA DHARURA UNAHITAJIKA KATIKA MUYO WA KIZALENDO
ndugu mtanzania mwenzangu popote ulipo duniani tunaomba mssada wako kwa Mzee Mohamed Paschal mkazi wa fuoni mambo sasa Unguja ambaye amekimbiwa na familia yake na hapo hana msaada wowote tatizo lake lilianza kipele hadi kuwa donda anaishi na mwanawe ambaye naye kimaisha hayuko vyema mara baada ya tatizo hilo mke wake aliamua kurudi kwao, msaada wako unahitajika kwa ajili ya kuweza kupata gharama za matibabu ya mguu unaomsumbua kwa muda wa miaka tisa sasa hali ambayo inapelekea kushindwa kufanya shughuli zake za kujipatia kipato kama umeguswa na swala hili waweza wasiliana nami kwa namba zangu za simu ya mkononi0774151617 au kupitia email yangu husseinhafidh@gmail.com
Subscribe to:
Posts (Atom)