tangazo
Friday, November 20, 2015
ZANZIBAR HEROES YAONDOKA NA WACHEZAJI WAO WOTE KASORO AGREY MORIS AMBAYE NI MAJERUHI
Na: Hafidh Hussein, Zanzibar.
Jumla ya wachezaji 20 wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) wameondoka usiku wa jana (Magharibi) kwenye uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume na kuelekea Adis Ababa kwenye mashindano ya CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP 2015 yatakayofanyika nchini Ethiopia Novemba 21.
Kocha Malale Hamsini Keya amewaahidi Wanzazibar Ubingwa bila ya wasi wasi wowote.
“ Mimi kama mwalimu nawaahidi Wazanzibar ushindi lazima, kila game ni ushindi tu”. Alisema Malale.
Kwa upande wake Awadh Juma captain wa Heroes nae pia amewaambia Wa Zenj wajitayarishe kuja kuwapokea wakati watakaporudi na kombe.
Aliseme Awadh, “Kwa kweli nawaambia Wazanzibar watuombee dua tufike salama na sisi tutaenda kupambana na tutarudi na kombe na wajitayarishe kuja kutupokea wakati tutakaporudi”.
Kama tunavofahamu Mlinzi wa Kati Agrey Moris hatokwenda Ethiopia kutokana na majeruhi aliyokuwa nayo kufuatia mchezo wa juzi wa kirafiki kati ya Zanzibar Heroes na Kombain ya Makocha kuumia na kushindwa kumaliza mchezo huo kwenye Uwanja wa Amaan ambapo Heroes ilishinda 1-0 kwa bao la Khamis Mcha.
Daktari wa timu ya Zanzibar Heroes Mohd Said Mwinyi alithibitisha kuumia Agrey na kusema kuwa atakaa nje ya uwanja zaidi ya Wiki mbili na nafasi yake kocha Malale Hamsini amemchukua Shaffii Hassan mlinzi wa timu ya Zimamoto.
Pia tumezungumza na mlinzi wa kushoto wa timu ya taifa ya Tanzania Mwinyi Haji Mngwali ambapo anazungumzia kuwa miongoni mwa wachezaji wa Heroes walondoka ambapo juzi alirudi Algeria .
“ Hii ndio mara yangu ya kwanza kucheza Heroes, nimefurahi sana na si kama ninauwezo mkubwa, a a bali kujituma na bahati pia imechangia, wazanzibar wasubiri makubwa kutoka kwetu”.
Lakini pia nilitaka kujua kwa MWINYI agusie kidogo mchezo wa juzi wa Tanzania walipofungwa mabao 7-0 dhidi ya Algeria ambapo na yeye pia alikuwemo miongoni mwa wachezaji waliofungwa mabao hayo.
“ Kipigo kile sitokisahau katika maisha yangu kwani ndio kipigo kikubwa kwangu nimejisikia unyonge sana, lakini watanzania wanaojua mpira hawatotulaumu sana mana ndio soka”. Alisema Mngwali.
Kikosi kilichosafiri leo kinaundwa na;
Makipa: Mwadini Ali (Azam), Mohamed Abraham (JKU).
Mabeki wa pembeni: Mwinyi Haji (Yanga), Nassor Masoud (Stand United), Adaymu Saleh (Coastal Union) na Ismail Khamis (JKU).
Walinzi wa kati: Nadir Harub (Yanga), Shafii Hassan (Zimamoto), Said Mussa (Mafunzo), Issa Haidary (JKU).
Viungo: Awadhi Juma (Simba), Mudathir Yahya (Azam), Saidi Makapu (Yanga), Mohamed Abdulirahmani Mbambi (Mafunzo), Hamis Mcha (Azam), Suleiman Kassim (Stand United) na Omari Juma (Hard Rock).
Washambuliaji: Ibrahimu Hilika (Zimamoto), Mateo Antony (Yanga) na Ame Ali (Azam).
Zanzibar wapo kundi B pamoja na Burundi, Kenya na Uganda na siku ya November 21 watacheza mchezo wao wa kwanza na Burundi.
lakini pia mbali na hayo Muamuzi wa Zanzibar mwenye beji ya FIFA Mfaume Ali Nassor ambae pia kachaguliwa kwenda kuchezesha mashindano hayo tayari amefika salama nchini Ethiopia ambapo aliondoka visiwani jana akifatana pamoja na mjumbe wa kamati tendaji ya CECAFA Mzee Zam Ali wote kwenda kwenye mashindano hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment