Na Ally Saleh
Wananchi wa Zanzibar waliamka asubuhi ya Oktoba 25 kwenda kufanya maamuzi ambayo yamo ndani ya katiba lakini pia ni sehemu ya maadili ya kidemokrasia.
Maadili hayo yalianza kurudishwa 1995 kwa maana ya wananchi kuamua viongozi wawatakao kila baada ya miaka mitano na hilo kwa hakika limefanywa mara nne bila ya kukosa.
Na katika mara nne zote CCM wameshinda na ikiwa na maana Wapinzani hawajashinda hata.moja na kwa hivyo CCM wakawa wanashika dola na kuwa mwendelezo ulioanzia 1964 chini ya chama cha Afro Shirazi.
Kitendo hiki cha kushika dola kwa hakika kimekuwa kikiipa CCM imani, kiburi na jeuri kuwa ndicho chenye uwezo peke yake wa kuiongoza Zanzibar.
Mbaya zaidi wakaanza kujenga hoja majigambo na misingi kuwa wao ndio wenye haki na pekee waliopigwa muhuri kuiongoza Zanzibar.
Kauli zimekuwa zikitoka wazi wazi kwa jeuri na kedi kuwa nchi haitolewi kwa karatasi na kuwa Ikulu hataingia mtu mwengine zaidi ya CCM na hazikuwahi kukanushwa, kupingwa wala kukemewa.
Kwa hivyo ndani ya mioyo ya CCM imekuwa kwamba.uchaguzi ni njia tu ya kuiambia jumuia ya kimataifa kuwa tumo kwenye njia.ya demokrasia na pengine utawala bora ili kujenga taswira ya kupata msaada.
Ila pia kuna fikra na sumu ya ajabu sana ilopandikizwa dhidi ya Maalim Seif kwamba haiwezekani na haistahiki kabisa yeye kuingia ikulu na husemwa ni kama haramu na najisi.
Kwa dhana hizo CUF ikadai kuibiwa uchaguzi wa 1995 na.jawabu ikawa hawakuibiwa kitu ila kura zao hazikutosha kwa sababu ndio kwanza wameingia siasani ingawa matokeo yalikiwa karibu 50 kwa 50.
Uchaguzi uliofuata 2000 CUF wakasema tena wameibiwa na zamu hio hawakukubali bali walojaribu kudai haki yao iliyopokwa na watu 31 waliuawa na maelfu kwenda ukimbizini Kenya na wengine Somalia.
Tena cuf wakaambiwa hawajaibiwa kitu ila ni madai ya uongo na uchu wa madaraka wa kiongozi wao Maalim Seif ambae aliwekwa jela miaka mitatu kupigania mabadiliko.
Yayo hayo yakatokea tena mwaka 2005 na kisha pia tena 2010 kwa kila njama kufanywa na kila.hila.kutekelwzwa ili Maalim Seif na CUF wasiingie Ikulu.
Hapo kati miafaka miwili ikafanywa na kutarajiwa muda wote Maalim Seif awe ndio mpole na.akubali madhila dhidi yake na yale.ya chama chake huku ni dhahiri akiwa na wafuasi nusu moja nzima ya Zanzibar.
Bila shaka wengi tunajua jeuri hii ambayo imekuwa ukifanywa imekuwa ikiridhiwa na CCM Dar esalam na Serikali ya.Jamhuri ya Muungano.
Pia ni wazi kuna.mkono wa.vikosi vya Muungano ambavyo kila msimu wa uchaguzi huigeuza Zanzibar kama.eneo la vita bila kuona matumizi kama hayo ya vifaa kuonekana Daresalam bila ya shaka maana yake ni kuwatisha Wazanzibari.
Lakini tukio la Oktoba 27 ndio lilopiga muhuru uingiliaji wa jeshi na vikosi katika taratibu za.uchaguzi pale alipochuliwa kwa nguvu Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji abdul hakim Ameir.
Jeshi letu halikutaka kujihusisha kabisa palipokuwa na malalamiko.na mpaka sasa yapo kuwa kuna vikundi vinabeba silaha vikifanya matendo ysiyo ya kimaadili kwa kuwaonea na kudhulumu wananchi labda kwa kuwa walolengwa ni Wapinzani.
Kwa kila hali CCM ilikuwa imeshashindwa katika uchaguzi wa.Oktoba 25 na ilikuwa imeishiwa njia kabla.kunusurka kwa tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jecha Salum Jecha.
Ila ni wazi kilchotokea ni mapinduzi baridi na kitu kisichokubalika kidemokrasia ambapo Tanzania inajitia mstari wa mbele kusimamia.
CCM kwa kuamini ndio pekee yenye haki ya kutawala imekuwa nyuma kifikra, imeganda kimawazo na imeozakiitakadi na ni chama kinachokimbiwa.
Kwa kuwa,ni chama kinachoongoza serikali ungetaraji umma ungevutika na kile kinachoitwa asilimia 90 ya utekelezaji wa ilani ya 2010… lakini wapi.
Ungetarajia kwa uwezo wake wa kiuchumi kwa..mtandao wake, kwa wingi wa makada.wangeshawishi umma… uwachague…lakini wapi.
Ilipooona kwenye viti vya uwakilishi wanapteza, CUF wanapata majimbo mapya Unguja na urais unakwenda na maji CCM ikapiga.mikambe ya kinyangumi tena maji haba.
Kitendo kinachoendelea kutokea cha Dk Shein kutafutiwa kipengele mpenyo ili aendelee kuwa kitini ni hasara kubwa kwa na pigo kwa CCM lakini ni aibu kwa Tanzanua.
Siamin kwamba nchi yangu Tanzania itakuwa na uso mbele ya jumuia ya kimataifa ambayoina imani na Tanzania kwa misimamo yake ya haki huko nyuma.
Umma wa Zanzibar utavunjika moyo kuwa kumbe Zanzibar kuna demokrasia baguzi na kumbe haina haja kushiriki uchaguzi wakati mshindi tayari ana chapa na kumbe zaidi kuna haja gani ya kuwa nz siasa za ushindani wa vyama.
Zanzibar, iwapo uamuzi huo wa kuwa na rais mwendeleaji utasimama, itarudi nyuma miaka hamsini na zaidi na baya zaidi wananchi watakuwa hawana tena imani na serikali hii na yoyote itayokuja maana ukitafunwa na nyoka kamba utaiogopa, na tumetafunwa mara ngapi hadi sasa?
No comments:
Post a Comment