Mpaka sasa wachezaji ambao hawajafika mazoezini ni wanne (4)
ambao ni Khamis Ali “Chichi” (KMKM), Nassor Masoud “Cholo” (Stand United, na
wawili wa Yanga Matteo Anton Simon na Said Makapu.
Wachezaji watatu wengine waliokuwa hawajafika mazoezini
Zanzibar Heroes ambao wanajulikanwa walipo ni Nadir Haroub “Canavaro” (Yanga),
Mwinyi Haji (Yanga) na Mudathir Yahya (Azam) wote wapo kwenye timu ya taifa ya
Tanzania (Taifa Stars).
Katika mazoezi ya leo tumebahatika kuzungumza na wachezaji
wawili walipomaliza mazoezi ambao ni Agrrey Morris na Ame Ali wote wakimsifia
kocha wao Malale Hamsini kwa dozi anayowapa.
Aggrey aliulizwa na mtandao huu kwanini amechelewa kufika
mazoezi ambao wenzake tangu jumatatu wameanza yeye kafika leo.
“ Mimi niliomba ruhusa kwa mwalimu kuwa nina dharura ndo mana
nimefika leo, na kwa upande wa mazoezi ni mazuri sana mana kocha anajua
kufundisha, naamini tutafanya vizuri kwenye mashindano”. Alisema Aggrey Morris.
Na kwa upande wake Ame Ali “Zungu” amesema mazoezi matamu
kweli kweli.
“ Mazoezi matamu, nimekuja leo tu lakini nimerizika, nakujibu
swali lako Kisandu kwanini sijaja mazoezi siku zote hizo, mimi Kisandu
nimeajiriwa kwenye timu ya Azam na siwezi kuja tu kama sijapokea taarifa kwa
mabosi wangu, nilipoambiwa Azam ndo leo umeniona”. Alisema Ame Zungu.
No comments:
Post a Comment