WANAFUNZI 151 wamelazimika kukatishiwa masomo yao elimu ya lazima, baada ya kuozwa waume hapa Zanzibar, kuanzia mwaka 2011 hadi mwezi septemba mwaka huu.
Taarifa zilizopatikana kutoka Wizara ya elimu pekee, zinaeleza kuwa idadi hiyo ni wale walioripotiwa, mara baada ya kuolewa wengi wao wakiwa chini ya mumri wa miaka 18.
Kwa mujibu wa idadi hiyo, wanafunzi wamekuwa wakipuingua kila mwaka kuolewa, maana mwaka 2011 kuliripotiwa wanafunzi 53, wakati mwaka 2012 kulipungua wanafunzi watatu na kuwepo 53.
Idadi hiyo imripotiwa kupungua tena, mwaka 2013 kufikia watoto 29 na kuripotiwa wanafunzi 21 pekee kwa Unguja na Pemba, huku mwaka uliofuata wakijitokeza 18 na mwaka huu watoto tisa.
Wilaya ya Micheweni ilikuwa kiboko kwa kuwa na idadi ya wnafunzi 62, ikifutiwa wilaya za Wete Pemba na Kati kwa unguja ambazo ziliripoti wanafunzi 19, chini ya wilaya Magharibi iliokuwa na watoto 17, huku wilaya za Chake chake na Mkoani zikiwa na wanafunzi 14 kila wilaya.
Aidha kwa kipindi hicho mwaka 2011 hadi mwaka jana, wilaya zilizoripoti idadi ni ndogo ni pamoja na Kaskazini ‘B’ saba, Kusini watano, huku Kaskazini ‘A’ na Magharibi zikiripoti kesi tatu tatu kila wilaya.
Mrajisi wa elimu Zanzibar Siajabu Makame Pandu, hivi karibuni akiwasilisha ripoti hiyo kwa waandishi wa habari, alisema hata idadi hiyo wizara bado inasikitishwa.
Amesema ndoa za utotoni zimekuwa zikiathiri sana maendeleo ya watoto wa kike kielimu, jambo ambalo huwavunjia mipango na mikakati yao ya baadae katika maisha.
“Lazima jamii iendelee kushirikiana na wizara ya elimu, katika kumaliza tatizo, na moja ni kiziripoti kesi hizo wanapogundua wazazi wamewaoza waume watoto wao’’,alisema
Afisa elimu na mafunzo ya amali wilaya ya Micheweni Mbwana Shaame, amesema huwenda kama malezi ya pamoja yakirudi na mtoto kulelewa na jamii, hali hiyo itapungua.
Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Pemba Omar Khamis Othuman, amesema lazima jamii ifikirie mara mbili, umuhimu wa kumsomesha mtoto wa kike, bada ya kuunga mkono kwenye kumuozesha.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Chake chake Hanuna Ibrahim Massoud, amesema lazima sheria zifanye kazi vyema iwapo wazazi wataendelea kuwakatisha watoto wa elimu.
Mchungaji wa Kanisa Katoliki la Kiluthere Tanzania KKKT Usharika wa Vitongoji Chake chake Pemba, Benjamen Kissanga, amesema hata kanisa haliridhii mtoto kukoseshwa haki yake ya elimu kwa kuolewa.
Sheikh Mohamed Hassan wa Chake chake, amesema inawezekana jamii haitambui kuwa elimu ni jambo la lazima, wakati ndoa kwa waumini wa kiislamu ni sunna.
“Inaonekana jamii inakimbilia ndoa ambayo ni sunna, kuacha elimu ambayo tulitakiwa tuitafute hadi china, ambayo ni faradhi’’,alifafanua.
Sheha wa shehia ya Mchanga mdogo Asaa Hamad Makame, alisema jamii inahitaji elimu kila siku, ili kueleweshwa umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike.
Mratibu wa FAWE Zanzibar, amesema moja ya sababu ya wazazi kuwaoza watoto wao, umaskini na hasa wa kumuendeleza mtoto bado ni changamoto.
Mzazi Khadija Omar Mudathiri wa Machomane Chake chake, yeye amesema, lazima serikali ibuni mifuko maalumu ya kuwasaidia watoto hasa wa kike wanaposhindwa uwezo wa kusonga mbele kielimu.
Mratibu wa mradi wa Kukuza Usawa wa kijinsia na Kuwawezesha Wanawake ‘GEWE’ kutoka Chama cha waandishi wa habari Tanzania TAMWA ofisi ya Zanzibar, Asha Abdi Makame, amesema mashine ya DNA pia ikiwepo inaweza kupunguza ubakaji kwa watoto.
Mtoto (17) wa shehia ya Mchanga mdogo ambae alikosa kufanya mitihani wake wa taifa wa darasa la kumi na mbili mwaka 2011, kwa kuolewa alisema lazima wazazi wawe makini.
“Wazazi wakiwa makini kwamba mtoto hata wa kike anaweza kusoma na kuibadilisha familia yake, basi ndoa za ovyo ovyo zitapungua’’,alisema.
Mratibu wa wanawake na watoto shehia ya Kangagani Aweza Salim Kombo, alisema kama vyombo vya sheria vitatekeleza wajibu wake vyema, basi ndoa, mimba na ubakaji utapungua.
Afisa Ustawi wa jamii wilaya ya Wete Haroub Suleiman Hemed, amese lazika kila chombo kikifanya wajibu wake, hakuna tatizo litakalodumu ndani ya jamii.
Hata hivyo taarifa za wizara ya elimu kisiwani Pemba, zinanyesha kuanzia mwaka 2012 hadi mwezi septemba mwaka huu, kulisharipotiwa wanafunzi 63 waliokatishwa masomo kwa kuolewa, akiwemo wa darasa la tatu skuli ya Uwondwe mwaka jana.
CHANZO ZANZINEWS
No comments:
Post a Comment