nyuma ya soko la mwanakwerekwe licha ya uchafu uliokithiri jaama aonekana akijisaidia haja ndogo
ndani ya soko la mombasa maaruufu soko la shimoni
sehemu ya machinjio ya kuku soko la mwanakwerekwe
katika baadhi ya maeneo ya ndani katika soko la shimoni
HALI YA MASOKO YETU YA ZANZIBAR KIPINDI HICHI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.
Ugomjwa wa kipindupindu mpaka mwanzoni mwa wiki hii, ulikuwa umeua watu 106 kote nchini na maelfu kuugua maradhi hayo.
Moja ya sababu kubwa inayochangia ugonjwa huu kuendelea kusambaa kwa kasi, ni uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji kutotunzwa ipasavyo.
Kwa msingi huo, ili kuudhibiti, hapana budi wananchi kufuata kanuni za usafi katika maeneo wanayoishi, fanyia kazi na maeneo ya biashara kama masoko, hoteli, baa, mama ntilie nakadhalika.
Suala la usafi kwa ujumla, ni tabia ambayo kila mwananchi anapaswa kuiheshimu.
Tunawashauri Watanzania wabadilike kwani ugonjwa huu ni wa hatari sana.
Kwa hakika kama hatutakuwa makini, ugonjwa huu utaleta maafa makubwa hasa katika kipindi hiki ambazo mvua zimeanza kunyesha katika maeneo mengi ya nchi.
Ni muhimu kuzingatia kwa dhati kabisa kanuni za usafi ambazo mbali ya usafi wa mazingira, pia kuhakikisha kwamba maji ya kunywa yanachemshwa, kunawa mikono baada ya kutoka msalani, kuosha matunda kabla ya kula na usafi wa vyombo vyote vinavyotumiwa kwa chakula ama kinywaji.
Ni matumaini yetu kwamba Watanzania watazingatia haya pamoja na maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na wataalam wa afya ili kuepusha maafa zaidi ya gonjwa hili.
No comments:
Post a Comment