MATTEO ANZA
LEO MAZOEZI NA KUTUPIA MOJA KWENYE MECHI
Zanzibar Heroes waanza vyema mchezo wa kirafiki
uliosukumwa jioni ya jana kwenye uwanja wa Amaan walipoifunga kombain ya Wilaya
ya Mjini bao 3-1.
Mabao ya
Zanzibar heroes yamefungwa na Aggrey
Morres dk 42,Rashid Abdallah dk 76 na Matheo Simon dk 84 na bao pekee la kufuta
machozi la Combine ya wilaya ya mjini limefungwa na Abdillah Rajab dk 74.
Mbali na
mchezo huo Katika Mazoezi yao asubuhi mahudhurio kwa wachezaji yamekuwa
na idadi kubwa baada ya kuongezeka Nassor Massoud Cholo, Said Juma Makapu
pamoja na Matteo Anton Simon na kukifanya kikosi hicho kuwa na jumla ya
wachezaji 25 kasoro watatu waliokuwepo taifa stars Nadir Haroub, Mwinyi Haji na
Mudathir Yahya , wakati Khamis Chichi pia ndie mchezaji pekee aliekuwa
hajajiunga na wenzake mpaka sasa ambapo kocha Malale Hamsini akisema ndo basi
kwa mchezaji huyo kucheza Heroes kwa mwaka huu.
Timu hiyo
(Zanzibar Heroes) leo hii mazoezi yake yamefikia siku ya 5 kwenye uwanja
wa Amaan ambapo wanafanya kila siku asubuhi.
Kocha Malale
Hamsini kafurahishwa sana kuona idadi wachezaji wengi kufika mazoezi.
“Nimefurahi
sana kaja Cholo, Matteo na Makapu, lakini Chichi pekee hajaja kwaiyo
nshamuondosha kwenye kikosi changu” . Alisema Malale.
Kwa upande
wa mechi za kujipima nguvu kwa michezo ya kimataifa kocha Malale amesema anayo
nia hiyo ya kucheza na taifa jengine.
“Ripoti
yangu nimewaandikia viongozi ndani yake pia nahitaji mechi ya Kubwa ya Kitaifa
ukiachia ya leo ya Wilaya ya Mjini”.
Mbali na
kocha pia tumezungumza na wachezaji
Nassor Massoud Cholo, Matteo Anton na Said Makapu ambao wote kwa mara ya kwanza
wamefika leo mazoezini.
Kwa upande
wa Nassor Massoud amesema alikuwa hana taarifa ndo mana akawa hajafika mazoezini
na pia alikuwa ana matatizo ya kifamilia.
“Nilikuwa na
matatizo ya kifamilia na pia sijapigiwa simu ya kuitwa ila naipenda timu yangu
ya Zanzibar na ndio maana leo nipo hapa mazoezini”. Alisema Cholo.
Kwa upande
wake Said Juma Makapu kiungo mkabaji wa Yanga amesema walikuwa hawana ruhusa ya
kuja kwenye timu hiyo kwasababu klabu yake ndio yenye dhamana.
“Sababu
ilionifanya nichelewe kufika mazoezini ni ruhusa, kwasababu bila ya ruhusa ya
katibu wangu wa Yanga siwezi kuja lakini jana nimepewa ruhusa na leo nimekuja
hapa Amaan”. Makapu alisema.
Nae Matteo
Anton Simon aliekuja mazoezi kwa mara ya kwanza leo hii na kwenye mechi katupia
moja wavuni jioni ya leo walipoitwanga wilaya ya Mjini 3-1 amesema mazoezi mazuri
tu leo alikuja na alichelewa kwasababu ya ruhusa.
“ Ukweli
sisi tupo kwenye timu lazima tupewe taarifa kwenye timu yetu licha ya kuwa
nimesikia taarifa ya kikosi kwenye Clouds Fm
lakini lazima nifate utaratibu si unajua tena klabu yetu ni kubwa”. Matteo
alisema.
Zanzibar
Heroes ipo kundi B pamoja na Burundi, Kenya na Uganda kwenye mashindano ya
CECAFA Chalenj Cup yanayotarajiwa kufanyika tarehe 21 ya mwezi huu ambapo siku
hiyo pia Zanzibar Heroes wakiwa kundi B
watacheza (21/11/2015) mchezo wao wa
Kwanza
Burundi vs Zanzibar, 24/11/2015 Uganda
vs Zanzibar na wa mwisho kwenye kundi
lao tarehe 27/11/2015 Kenya vs Zanzibar
.
No comments:
Post a Comment