Maafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar wakifungua moja ya Boxi lenye Vipozi vyenye Kemikali ambavyo vimepigwa marufuku kutumika duniani baada ya kuvikama Bandarini vikitokea Marekani na Italy.
Baadhi ya Vipozi vyenye Kemikali ambavyo vimepigwa marufuku kutumika duniani vikiwa vimetolewa katika Maboxi ambayo yalitumika kuviihifadhi. Vipodizi hivyo Vinasubiri kuteteketezwa na Maafisa wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Na Miza Kona Maelezo Zanzibar 25/11/2015
Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi imekamata vipodozi haramu katika Bandari Kuu ya Malindi Zanzibar ambavyo vimepigwa marufuku kuingizwa nchini.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko Ofini Mombasa Mkaguzi wa Bodi hiyo Nassir Buheti amesema vipodozi hivyo haramu vimepigwa marufuku kuingizwa nchini kutokana na kuwa Viambata vyenye kemikali vinavyoweza kuleta madhara Mtumiaji ikiwemo Kansa, Ulemavu pamoja na uharibifu wa ngozi.
Amevitaja vipodozi hivyo kuwa ni pamoja na Movet Crèame kutoka Itali na Medical Fade Crème kutoka Marekani vyenye uzito wa tani tatu na kuhifadhiwa katika Makontena yaliyochanganyishwa na vitu vingine bandarini hapo.
Aidha amefahamisha kuwa vipodozi vya aina Movet Cream hutumika kwa matibabu ya ngozi lakini inahitajika kupata ushauri wa daktari kabla ya kutumia ili kuepukana na madhara.
Mkaguzi huyo ameeleza mawakala wa vipodozi hivyo wamedai kuwa havikukusudiwa kuingizwa nchini jambo ambalo vipodozi vya aina hiyo vimepigwa marufuku dunia nzima.
Amesema Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi inafanya juhudi ya kutaka kudhibiti kuingiza bidhaa haramu nchini hivyo inaomba mashiriano makubwa kwa jamii ili iweze kufikia lengo lililokusudiwa.
Aidha Mkaguzi Buheti amesema Sheria inasema si ruhusa kuingiza, kuuza, kusambaza vipodozi haramu na kuwataka wafanyabiasha wa vipodozi, dawa pamoja na Chakula kutofanya udanganyifu wa bidhaa wanazoingiza ili kuepuka madhara yasiongezeke nchini.
No comments:
Post a Comment