tangazo

tangazo

Wednesday, November 18, 2015

ZANZIBAR HEROES KUKABIDHIWA BENDERA JANA HII HUKU AGREY MORIS KUKOSA CHALENJ MWAKA HUU

ZANZIBAR HEROES KUKABIDHIWA BENDERA JANA HII HUKU AGREY MORIS KUKOSA CHALENJ MWAKA HUU

Na: Abubakar Kisandu, Zanzibar.

Wachezaji wa  timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes)  wametakiwa kuwa na umoja, ushirikiano na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote mashindano ya challenge cup yanatarajiwa kuanza  tarehe 21 ya mwezi huu Adis Ababa nchini Ethiopia.

Ushauri huo umetolewa na DR Mwinyi Haji Makame ambae alikuwa mgeni rasmi katika shughuli nzima ya kuwaanga wachezaji hao pamoja na kuwakabidhi bendera na wimbo wa taifa la Zanzibar katika ukumbi wa VIP Amaan Unguja.

“ Ushirikiano, umoja, kupendana pamoja na nidhamu ndio silaha yenu ya kufanya vizuri , lazima viongozi wenu muwasikilize na musilaumiane, mukifanya hivyo mutafanikiwa kufanya vizuri huko Ethiopia”. Alisema Mwinyi Haji.

Wakati huo huo Dr MWINYI HAJI MAKAME alimkabidhi Bendera na CD ya Wimbo wa taifa la Zanzibar Nahodha wa timu hiyo  Awadh Juma huku akimsisitiza kuwa wanawakilisha Wanzanzibar wote kwenye mashindano hayo ndio mana wakakabidhiwa Bendera na CD .

“ Nakukabidhi Bendera hii na CD Captain wetu kwa heshma kubwa ya nchi yetu ili mukawatuwakilishe vizuri kwani wanzanzibar watakuangalieni kwenye mashindano hayo kupitia TV”.

Kwa upande wake captain wa timu hiyo Awadhi Juma amewaahidi Wanazanzibar kwamba watarudi na kombe bila ya hofu yoyote kwani wao wanaenda kushindana na si kushiriki.

Aliseme Awadh, “ Sisi tunaenda kupambana  na si kushiriki , kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutarudi na ubingwa kwani tunajua umuhimu wa mashindano , hivyo siku tutakayorudi mashabiki waje kutupokea kwa wingi uwanja wa Ndege”.

Kwa upande mwengine Mlinzi wa Kati Agrey Moris hatokwenda Ethiopia kutokana na majeruhi aliyokuwa nayo kufuatia mchezo wa juzi wa kirafiki kati ya Zanzibar Heroes na Kombain ya Makocha kuumia na kushindwa kumaliza mchezo huo kwenye Uwanja wa Amaan ambapo Heroes ilishinda 1-0 kwa bao la Khamis Mcha.

Daktari wa timu ya Zanzibar Heroes Mohd Said Mwinyi amethibitisha kuumia Agrey na kusema kuwa atakaa nje ya uwanja zaidi ya Wiki mbili na nafasi yake kocha Malale Hamsini amemchukua Shaffii Hassan mlinzi wa timu ya Zimamoto.

Tumemtafuta mlinzi huyo Shaffi aliechaguliwa kuchukua nafasi ya Agrey na kusema kuwa anafuraha sana.

“ Nimefurahi kocha kuniona mimi nafaa na kunichagua, naamini ntafanya vizuri kwani mimi pia ni mzowefu katika mashindano hayo maana nshacheza”. Alisema Shaffii.

kikosi hicho kinaundwa na MAKIPA MWADINI ALI AZAM, MOHD ABRAHAM JKU.
 MABEKI PEMBENI
MWINYI HAJI YANGA, NASSOR MASOUD STAND UNITED, ADAYMU SALEH COASTAL UNION NA ISMAIL KHAMIS JKU.

 WALINZI WA KATI
NADIR HARUB YANGA, SHAFII HASSAN ZIMAMOTO, SAID MUSSA MAFUNZO,  ISSA HAIDARY JKU.

 VIUNGO
AWADHI JUMA SIMBA,  MUDATHIR YAHYA AZAM,  SAIDI MAKAPU YANGA,  MOHD ABDULIRAHMANI MBAMBI MAFUNZO,  HAMIS MCHA AZAM, SULEIMAN KASSIM STAND UNITED NA  OMARI JUMA HARD ROCK.

 WASHAMBULIAJI IBRAHIMU HILIKA ZIMAMOTO, MATEO ANTONY YANGA NA AME ALI AZAM.

Kikosi cha Zanzibar Heroes kinatarajia kuondoka kesho majira ya saa 9 alaasiri kwenye uwanja wa Ndege wa Abeid Aman  Karume na kitafikia  Dar es salam na wataondoka kwenye uwanja ndege wa huko Dar kisha wataondoka na watatumia ndege ya Ethiopia  na kwenda huko moja kwa moja ,lakini pia mbali na hayo  Muamuzi wa Zanzibar mwenye beji ya FIFA Mfaume Ali Nassor ambae pia kachaguliwa kwenda kuchezesha mashindano hayo tayari ameondoka visiwani leo hii akifatana pamoja na mjumbe wa kamati tendaji ya CECAFA Mzee Zam Ali kwenda kwenye mashindano hayo.

 Zanzibar wapo kundi B pamoja na Burundi, Kenya na Uganda  na mchezo wao wa mwanzo watacheza na Burundi November 21

No comments:

Post a Comment