Baada ya kuchezea kipigo cha mabao 4-0 kwa timu ya taifa ya Zanzibar walipopigwa Uganda kwenye mashindano ya CECAFA CHALENJI CUP huko Ethiopia , Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Salum Bausi amesikitika kwa kipigo hicho huku akiwabebesha lawama kamati inayosimamia soka pamoja na Benchi la Ufundi kwa kusema kuwa timu imekosa nidhamu na ndio maana ikapata aibu hiyo.
“ Timu imekosa nidhamu wachezahji wanacheza tu ndo maana tunafungwa kama hivi, hatujawahi kufungwa mabao 4-0 kwa miaka ya hivi karibuni, Uganda inatufunga?, wakati sisi mara nyingi tunawafunga. Alisema Bausi.
Aidha Bausi alisikitishwa sana kwa kuachwa kocha wa makipa Zanzibar ambae ni Saleh Machupa na timu kwenda huko Ethiopia bila ya kocha wa Makipa.
“Imeniuma sana kocha wa makipa kaachwa hapa Zanzibar , timu haina kocha wa makipa!, ni aibu sana wamejazana makocha watatu tu huko wakati kocha wa makipa wamemuacha, ni muhimu angeenda mana leo kashapewa kadi nyekundu Mwadini, sijui itakuaje mchezo wa mwisho na sijui nani atakaa na makipa kuwajenga kisaikologia!, yani viuongozi wapo kama washamba washamba tu mana wao lazima wasafiri , yani inauma sana”.
Hata hivyo kocha huyo amesema kina Moroco na Canavaro walikuwa wapumzike tu na wamejitia aibu kwenda huko Ethiopia.
“ Kocha Hemed Morocco alikuwa atulie tu na kupumzika, mwenzake Mkwasa yupo nyumbani katulia, tumefungwa 7-0, siku ya 2 wamekuja Zanzibar na kuungana na wenzao kwenda Ethiopia, hawezi kumudu timu maana hajawahi kuifundisha hata siku moja mazoezi, yani hii Zanzibar majanga tu, na hata Nadir alikuwa nae apumzike tu bora lakini ndo mambo ya Zanzibar haya”. Alisema kocha Bausi.
Kocha Salum Bausi aliinoa Zanzibar Heroes kwenye mashindano hayo mwaka 2012 nchini Uganda na kufanikiwa kunyakua ushindi wa tatu , lakini pia aliifundisha tena mwaka 2013 mashindano yaliofanyika nchini Kenya ambapo Heroes ilitolewa kwenye makundi na pia mwaka huo Bausi aliwaacha nyota 3 muhimu Zanzibar na Tanzania ambao ni Nadir Haroub, Agrey Moris na Abdi Kassim “Babi” na kuwachukua walinzi walichipukia kwa wakati huo Mohd Fakih (Sosha) ambae kwasasa anacheza Simba pamoja na Mlinzi Shaffi Hassan.
Timu ya taifa ya Zanzibar imesafiri na makocha watatu, akiwemo kocha mkuu Hemed Suleiman (Morroco), na makocha wasaidizi wawili Malale Hamsini Keya na pamoja na Hafidhi Muhidin, wakati kocha wa makipa aliedima siku zote za mazoezi aliachwa na hakwenda Ethipia ambae ni Saleh Machupa pia walinda mlango walikwenda huko ni wawili tu ambao ni Mwadin Ali pamoja na Mohammed Abrahman wakati kipa Mohd Ali wa Tanzania Prisons aliachwa, sasa mchezo wa mwisho kati ya Zanzibar heroes na Kenya hakuna kipa wa akiba baada ya leo kupigwa kadi nyekundu kipa nambari moja Mwadin.
Swali linakuja nani atakuwa kipa mbadala wa Mohammed Abrahman kwenye mchezo wa mwisho maana kipa waloenda 2 tu na Mwadin ana kadi nyekundu?. Lazima mchezaji wa ndani awe mbadala wa kipa Mohammed Wawesha.
No comments:
Post a Comment