Timu ya Mtende Renger yenye maskani yake kusini mwa kisiwa cha Unguja ambayo
inashiriki ligi kuu soka Zanzibar kwasasa takribani misimu 4 mfululizo
imewaachia nafasi hiyo ya ligi kuu msimu huu wa mwaka 2015-2016 maswahiba zao
wapya Kilimani City Cooperative Society
ambao wanayo timu inashiriki ligi daraja la pili wilaya ya Mjini.
Akizungumza nasi katibu wa Kilimani City Football Club
Ramadhan Juma amesema wamepata ofa kutoka kwa Mtende Renger watapewa daraja na
watachanganya uongozi kwa pamoja na kwenye ligi kuu msimu huu watatumia
wachezaji wale wale wa Mtende wa msimu ulopita.
“ Mtende Renger wametupa daraja, na uongozi tutashirikiana”.
Kwa upande wake katibu wa Mtende Renger Salum Sina amekiri
kuwa timu yake Mtende wamewapa daraja kilimani City huku akisisitiza kuwa yeye
atabakia kuwa katibu kama kawaida.
“Kweli Kilimani City tumewapa timu yetu lakini katibu
nitabaki kuwa mimi kama kawaida"
Viongozi wa timu Mtende Renger wameshindwa kuongoza timu hiyo
kutokana na ukata wa fedha, baada ya aliekuwa kiongozi wao mkuu anaehudumu timu
kifedha kuachana nayo timu hiyo.
No comments:
Post a Comment