tangazo

tangazo

Sunday, November 29, 2015

ZANZIBAR KUWA MWENYEJI KUANDAA MASHINDANO YA KAGAME 2016




Na: Abubakar Kisandu, Zanzibar.

Chama cha soka visiwani Zanzibar  (ZFA) kimethibitisha kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya vilabu kwa ukanda wa afrika mashariki na kati ya KAGAME CUP, ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi wa 7 mwakani.

Mkurugenzi wa ufundi wa ZFA Massoud Attai amethibitisha kuwa Zanzibar watakuwa wenyeji kuandaa mashindano hayo ambapo walipelekea maombi yao kwa CECAFA kwa kutaka kuwa wenyeji na CECAFA wakawakubalia kuandaa wao mwakani (2016) na kwasasa maandalizi yameshaanza maana Baraza la Michezo tayari wameshapokea barua ya kuwa Zanzibar ni wenyeji mwakani .


“Nikweli Zanzibar tumepeleka maombi yetu kwa CECAFA kuwa mwenyeji na tayari wameshatukubalia, kwaiyo yatafanyika mwakani bila ya wasi wasi wowote”. Alisema Attai.

Katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika ndani ya visiwa vya zanziabar ambapo timu ya Mafunzo na JKU ambao ndio bingwa na makamo bingwa wa ligi kuu ya Zanzibar msimu wa 2014-2015 ndio watakaowakilisha zanzibar, lakini pia hii si mara ya kwanza kwa Zanzibar kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ambapo waliwahi kuwa wenyeji miaka mingi sana kama mwaka 1985 na 1990 na mashindano yakachezwa kwa utulivu wa hali ya juu na mashindano yakanoga.

No comments:

Post a Comment