“TUSIHARIBU TIMU ZOTE , TUSAIDIENI SISI SAND HEROES”
Na: Abubakar Kisandu, Zanzibar.
Timu ya taifa ya Zanzibar ya soka la ufukweni ( Zanzibar Sand Heroes ) ipo kwenye mazoezi makali ya kujiandaa kwenye mashindano beach soccer yanayotarajiwa kufanyika katikakati ya mwezi ujao nchini Kenya.
Timu hiyo inajifua kwenye fukwe za Bububu bamboo yenye jumla ya wachezaji 13 ambao 7 walikuwemo kwenye timu ya taifa ya Tanzania ya beach soccer.
tumefanikiwa kuzungumza na kocha msaidizi wa timu hiyo ambae ni Fahad Khamis na hapa akizungumzia mazoezi yanavokwenda napia akiamini watafanya vizuri kwenye mashindano yaliopo mbele yao ambapo akiwataka wadau wa michezo wajitokeze kuisaidia timu hiyo.
“ Mazoezi yanaendelea vizuri hapa Bamboo, tulianza mazoezi magumu na kwasasa tunafanya madogo madogo tu, timu yangu nzuri mana najivunia ninawachezaji 7 wanaocheza timu ya taifa, nawaomba wadau wa michezo watusaidie kwa hali na mali ili tukawakilishe vyema huko Kenya”. Alisema kocha msaidizi wa Sand Heroes.
Zanzibar sand Heroes ilipata mualiko kwenda nchini Kenya kwenye mashindano yanayofanyika kila mwaka , ambapo mwaka huu yanatarajiwa kufanyika 16-20 mwezi Disemba kwenye Fukwe za Buntwani, kata ya Kilifi, mji wa Malindi nchini humo.
No comments:
Post a Comment