tangazo

tangazo

Thursday, December 31, 2015

Karafuu Kiungo kwa Vyakula na Tiba ya Magonjwa mengi


Na Zuhura Omar na Pili Khatib -MUM
Karafuu ni zao linalotokana na mkarafuu, ingawa karafuu hazimo katika kundi la vyakula wala vinywaji lakini ni kiungo na dawa muhimu sana kwa maisha ya binadamu.
Mikarafuu ilianza kupandwa kwenye visiwa vya Shelisheli, Mauritius na sehemu nyinginezo katika karne ya 19. Miche ya mikarafuu ililetwa Zanzibar kutoka Indonesia, mashariki ya mbali mwaka 1818.
Mikarafuu inastawi zaidi Visiwani vya Unguja na Pemba ambapo katika miaka 30 iliyopiata Zanzibar ilikuwa inazalisha asilimia 80 ya karafuu zote zinazohitajika duniani ambapo uchumi wake ulitegemea sana zao la karafuu.
Karafuu zina matumizi mengi, ambapo hutumika kama kiungo katika vyakula na vinywaji, dawa kwa maradhi ya tumbo, meno na misuli vile vile hutumika katika kuleta harufu nzuri ya kinywa, mwili na mazingira ya nyumbani.
Pia karafuu zinatumika katika uzalishaji wa bizaa nyengine ikiwemo sigara, mafuta ya karafuu ambayo hutumika kwa kuchulia misuli inayouma, kutengezea dawa za meno na perfume kwa ajili ya manukato.
 Karafuu zinatumika sana kwenye mapishi ya vyakula mbali mbali ikiwemo nyama, biriani, pilau, mchuzi wa masalo na vyakula vikavu kama vile vileja, beskuti na donas na kwa ubande wa vinywaji karafuu hutumika katika chai na maziwa .
Kama vilivyo viungo vyengine karafuu nazo zina utamu, ladha na harufu nzuri ya kuvutia na kupendeza katika vyakula hivyo ambapo watu wengi hasa katika bara la Asia, Mashariki ya kati na ulaya hupenda sana kiugo cha karafuu katika vyakula vyao.
Karafuu inasaidia usagaji mzuri wa chakula tumboni na ni nzuri  kwa matibabu ya maumivu ya tumbo, tumbo kujaa gesi na kiungulia. Hivyo karafuu ni miongoni mwa kiungo muhimu katika vyakula kutokana na vinasaba vya aina ya eugnol vilivyomo ndani ya karafuu.
Aidha karafuu hutumika katika utengenezaji wa mafuta (Mafuta ya karafuu) ambapo mafuta hayo husafisha damu, tafiti zinaonyesha kuwa visanaba vilivyomo katika karafauu vinapunguza sumu katika damu. Vinasaba aina ya eugnol vilivyomo ndani ya karafuu vinasaidia mzunguko mzuri wa damu.
Kutokana na ukuaji wa viwanda duniani kumekuwa na mahitaji makubwa ya karafuu pamoja na kuongezeka kwa nchi zinazozalisha ambapo karafuu hutumika sana kwa utengenezeji wa sigara katika nchi za Ulaya, Asia na Marekani.
Sigara zinazotengenezewa karafuu kutoka Zanzibar zina thamani na ubora zaidi duniani kuliko sigara zinazotengezewa karafuu kutoka nchi nyengine kutokana na ubora wa karafuu za Zanzibar.
Pia karafuu hutumika katika viwanda kwa ajili ya kutengezea dawa za meno kwa ajili ya kutunza meno na kuondosha maumivu ya meno na ufidhi, kung’arisha meno na kuleta harufu nzuri ya kinywa, harufu iliyomo katika karafuu inasaidia kuondosha harufu mbaya mdomoni.
Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa mwaka 2011katika Jarida la Asia Plant Science and Research toleo namba 1 (2) karafuu husadia kutibu vidonda vya mdomo na kuimarisha Afya ya fizi pamoja na kuzuia meno kuoza.
Aidha Mafuta ya karafuu yamekusanya vinasaba vya eugnol ambavyo vimekuwa vikitumiwa na Madaktari wa meno kwa miaka mingi kutibu matatizo ya meno na ufizi.
Karafuu inatumika katika urembo ambapo hutumika kusugulia mwili (scrub) kwa kuchanganya unga wa karafuu kavu iliyosagwa na mafuta ya nazi na liwa ambapo husuguliwaa mwili mzima kuondoa uchafu.
Mbali na hayo pia karafuu hutengenezewa sabuni ambazo ni nzuri kwa kuondosha maradhi ya ngozi kama vile harara, vipele na chunusi na kuifanya ngozi iwe nyororo na yenye kuvutia. Sio hayo tu lakini pia karafuu hutumika kutengenezea mafuta mazuri kwa sababu karafuu ina harufuu ya kipekee inayovutia.
Hivyo karafuu na mafuta ya karafuu ni mazuri kwa ajili ya kutunza ngozi hasa kwa ngozi yenye mabaranga, mba na kuchakaa ambapo huifanya ngozi kuwa nzuri na yenye kung’ara.
Matumizi ya karafuu na mafuta ya karafuu kwa kawaida humfanya mtu kuwa mchangamfu kwa kuondoa uchofu kwa vile karafuu inaiweka akili katika hali nzuri na kufanya ubongo ufanye kazi vizuri. Pia husadia kuondoa matatizo ya kusinzia, kupoteza kumbukumbu na wasiwasi.
Mafuta ya karafuu husaidia kuondosha maumivu ya kichwa kwa kuchanganganywa na chumvi na kupakaa kwenye paji la uso hupoza maumivu. Pia huondosha matatizo katika mfumo wa upumuaji na kusafisha koo na hutibu kikohozi, mafua na pumu.
Mchanganyiko wa mafuta ya karafuu na mafuta ya ufuta (sesame oil) ni mazuri kwa kuondsha maumivu ya sikio.

Wednesday, December 30, 2015

ZFA WILAYA YA MJINI WALIA NA KOMBE LA MAPINDUZI



Na: Abubakar Khatib (Kisandu), Zanzibar.

Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa Miguu Wilaya ya Mjini Hassan Haji “Chura” amesikitishwa kwa kutojumuishwa hata mjumbe mmoja kutoka chama chao kuwemo kwenye kamati inayosimamia kombe la Mapinduzi ambapo chama chao ndio waanzilishi wa Kombe hilo.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa Mwenyekiti huyo kwa kusema kuwa wao ndio walioanzisha kombe hilo lakini wamesahauliwa sasa.

“Nasikitika sana kuona katika wajumbe wote wa kamati ya kombe la Mapinduzi hata mjumbe mmoja kwetu hajatoka wakati sisi ndo waasisi wa kombe hili!”.

Aidha mwenyekiti huyo alizidi kufafanua juu ya kutoshirikishwa.

“ Ligi zipo nyingi lakini mbona watu wanakuwa vinganganizi kwenye kombe la Mapinduzi!, basi waiboreshe ligi kuu!, kwanini huko hawajenda?, kwasababu kombe la Mapinduzi ni biashara na linawanufaisha watu wengi”.Alisema Hassan.


Huu utakuwa ni mwaka wa tano kwa kombe hilo tangu liondoshwe ZFA Wilaya ya Mjini na kupelekwa Wizarani ambapo ZFA Wilaya ya Mjini walilianzisha mwaka 2007.

MAFUNZO BINGWA KOMBE LA MAPINDUZI – AME MSIMU  


Na: Abubakar Khatib (Kisandu), Zanzibar.

Timu ya Mafunzo ya mpira wa Wavu yapania kuchukuwa ubingwa wa Mapinduzi yatakayoanza tarehe 6/1/2016 katika uwanja wa Mafunzo Mjini Unguja.

Kauli hiyo ameitoa kocha wao Mkuu ambae ni Ame Msimu alipozungumza nasi leo hii asubuhi baada ya kumaliza mazoezi.

“ Maandalizi mazuri na vijana wanapokea vizuri mazoezi na ndio maana naamini ntachukua Ubingwa wa Mapinduzi kama nilivyochukuwa ubingwa wa ligi kuu”. Alisema Ame.

Mapinduzi Zanzibar huwa yanaenda sambamba na michezo mbali mbali kila ifikapo mwezi Januari ambapo vyama vya michezo tofauti huandaa mashindano yao kwa mchezo husika kwa kwenda sambamba na kuazimisha sherehe hizo.

DOKTA SHEIN AZINDUA MIRADI YA MAENDELEO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo ametembelea miradi ya Maendeleo ukiwemo mradi wa gati mpya pamoja na mradi wa maji safi na salama huko Wilaya ndogo Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja na kueleza kuwa ahadi zake zina lengo la kuwasaidia wananchi na kuwaletea maendeleo endelevu.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kutembelea miradi hiyo Dk. Shein alisema kuwa amefurahishwa kwa kiasi kikubwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuwaletea maendeleo sambamba na kuimarisha huduma za kijamii.

Dk. Shein alisema kuwa  ujenzi wa gati mpya   umejengwa kwa kitaalamu zaidi kwani gati hiyo itahilimi vishindo vya vyombo vyote kwani juhudi hizo zote ni kwa ajili ya usafiri wa uhakika wa wananchi wa kisiwa cha Tumbatu pamoja na bidhaa zao hasa ikizingatiwa kuwa wananchi hao wa Tumbatu wao wenyewe ndio waliokuwa mafundi chini ya usimamizi wa Shirika la Bandari.

Katika maelezo yake  Dk. Shein alisema kuwa ujenzi huo wa gati ni miongoni mwa maendeleo makubwa yaliokusudiwa kwa ajili ya wananachi wa Tumbatu ambapo kabla ya kuwepo kwa gati hiyo wananchi hao walikuwa wakipata usumbufu mkubwa.

Akieleza kuhusu mradi mpya wa maji safi  na salama, Dk. Shein alisema kuwa kutokana na kuwa maji ni uhai na hakuna maisha ya mwanaadamu bila ya kuwepo kwa huduma ya maji ndipo Serikali ikaona haja ya kuwaongeza huduma hiyo wananchi wa Tumbatu kwa kuanzisha mradi huo mpya wa maji.

Dk. Shein alisema kuwa lengo na madhumuni ya mradi huo ni kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wa Tumbatu hivyo aliwataka wananchi hao kuutunza mradi huo ili uwasaidie zaidi wao na vizazi vyao vijavyo.

Aidha, Dk. Shein aliwaahidi wananchi wa Tumbatu kuwa matangi kwa ajili ya maji yatajengwa  kisiwani humo na Serikali kwani uwezo huo inayo.

Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwataka wananchi wa Tumbatu kuwapuuza wale wote watakaobeza miradi hiyo kwani hulka hizo ni miongoni mwa hulka za baadhi ya wanaadamu na kusisitiza kuwa mwanaadamu yeyote anaepata neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni vizuri akashukuru.

Dk. Shein pia, alitumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi wa Tumbatu kwa kushiriki vyema katika ujenzi wa miradi hiyo na kuwaadi kuwa Serikali yao itaendelea kuwaunga mkono katika kuwapelekea miradi ya maendeleo.

Akitoa shukurani kwa wazee wa Tumbatu, Dk. Shein alipokea ombi lao la kutaka kuimarishiwa zaidi kituo chao cha Polisi kwa lengo la kuongezewa ulinzi wanachi hao pamoja na mali zao huku akiwaahidi kuwa juhudi zitachukuliwa na Serikali katika kukiimarisha zaidi kisiwa cha Tumbatu kwa kujenga barabara pamoja na taa maalum za muangaza wa jua kwa mashirikiano ya pamoja Serikali na uongozi wa Jimbo hilo.

Nae Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu Mhe. Haji Omar Kheir alitoa pongezi kwa Dk. Shein kwa juhudi zake za makusudi za kuhakikisha wananchi wa Tumbatu wanapata huduma bora maendeleo zikiwemo huduma za afya, maji safi na salama,umeme, elimu ujenzi wa gati na huduma nyenginezo.

Aidha, Mwakilishi huyo wa Tumbatu ambaye pia, ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ alitoa pongezi kwa Wizara ya  Miundombinu na Mawasiliano pamoja na Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kwa kutekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM.

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Abdalla Juma alimueleza Dk. Shein kuwa ujenzi wa gati hiyo mpya ni kutekeleza agizo la Serikali na kusema kuwa kwa upande wa Tumbatu umekamilika na kilichobaki ni mambo madogo madogo huku akieleza kuwa kwa upande wa gati ya Mkokotoni ujenzi wake unatarajiwa kuanza mapema mwaka ujao.

Mkurugenzi Juma alisema kuwa ujenzi wa gati hiyo mpya kwa upande wa Tumbatu ambayo tayari imeshaanza kutumika hadi kumaliza kwake utagharimu Shilingi 374 ambapo kwa upande wa gati ya Mkokotoni ambayo tayari michoro yake ipo, itagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni moja na wakati wowote tenda yake itatangazwa.

Alisema kuwa kwa upande wa gati ya Tumbatu ni kwa ajili ya vyombo yote vidogo vidogo vikiwemo vile vya kienyeji ambapo pia, limejengwa eneo maalum kwa ajili ya mizigo na kwa upande wa Mkokotoni bandari hiyo mpya itatumiwa na hata boti kubwa.

Nae Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk. Mustafa Ali Garu kwa upande wake alisema kuwa mradi huo mpya wa maji safi na salama kisiwani unaotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar umeshaanza kutoa huduma huku akieleza kuwa mchango mkubwa umetolewa na wananchi wa Tumbatu, Mwakilishi wa pamoja na Washirika wa Maendeleo wakiwemo Ubalozi wa Marekani na Iran.

Garu alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kuwa na visima vitatu ambapo tayari hivi sasa kisima kimoja kimeshaanza kazi kilichochimbwa huko Donge Kipange na vyengine vinaendelea na kueleza kuwa kukamilika kwa visima hivyo na kuunganishwa kwake kutaondosha kabisa upatikanaji wa maji kwa mgao kama ilivyo hivi sasa na badala yake yatapatikana kwa muda wote wa masaa 24.

Garu alisema kuwa Mradi huo unatekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia ZAWA ikiwa ni pamoja na kulaza mabomba baharini na  uchimbaji visima na kueleza kuwa gharama za Mradi huo ni T. Shilingi Bilioni moja na nusu na kwa hivi sasa tayari Shilingi milioni 700 zimeshatumika.

Nao wazee wa Tumbatu walitoa pongezi kwa Dk. Shein kwa juhudi za makususdi anazozichukuwa za kuwapelekea maendeleo wananchi wa kisiwa hicho sambamba na kutekeleza kwa vitendo ahadi anazowaahidi.


Sambamba na hayo, Wazee hao walimueleza Dk. Shein kuwasaidia kukiimarisha kituo chao cha polisi kwa lengo la kuimarisha hali ya usalama katika kisiwa chao.  

BAADA YA KUVUNJA MKATABA NA TIMU YA SIMBA NA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA ZANZIBAR , SAMIH AELEZEA MADUDU YALIOPO SIMBA MPAKA AKAONDOKA




samihi alipofanyiwa operesheni akiwa azam

Na: Abubakar Khatib (Kisandu) zanzibar.

Mlinzi wa kushoto  Samih Haji Nuhu ambae ameondoka Simba kwenye dirisha dogo la usajili na kujiunga na Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Zanzibar timu ya  Mafunzo, ameelezea sababu kubwa ya kuvunja mkataba na timu hiyo ya Msimbazi na kujiunga na Mabingwa wa Zanzibar.
“ Sasaivi nipo timu ya Mafunzo kule  nilivunja mkataba mimi sijafukuzwa Simba, mana Simba nimeondoka kwasababu kuna mambo hatujakubaliana kwaiyo nikaamua mimi mwenyewe niondoko mana nahisi uongozi hauangalii nini mchezaji afanyiwe kwasababu wanaingilia mambo ya makocha, uongozi wa Simba haupo sawa, mimi nimeamua niondoke kwa nia safi ili siku nyengine wakinihitaji nirudi kwa aman na salama”.

Aidha Samih alizidi kufichuwa mengi kwenye klabu ya Simba likiwemo pia la kuondoka kwa Elius Maguli.

“ Mfano kama Maguli kaondoka Simba kutokana ya viongozi kutokuwa makini kwenye kazi yao, kwani kuna baadhi ya viongozi hawafai kwenye timu ya Simba”. Alisema Samih.

Samih Haji Nuhu kwasasa ataitumikia timu ya Mafunzo ya Zanzibar kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika na pia atacheza kwenye Kombe la Mapinduzi pamoja na mzunguko wa pili kwenye ligi kuu soka zanzibar kanda ya Unguja.

Tuesday, December 29, 2015

WANAUME 1500 KUJITANGAZA KUWA NI MASHOGA HUKO IRINGA??


Kukithiri kwa biashara haramu ya ngono pamoja na tabia ya ushoga mkoani Iringa kunadaiwa kusababishwa na baadhi ya vijana wa vyuo vikuu waonafika mkoani humo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu, huku miongoni mwao wakitaka starehe zilizo nje ya uwezo wao.
Tamaa ya kumiliki vitu vya thamani – ni miongoni mwa mambo yanayotajwa kuwahadaa baadhi ya wasomi hao wa vyuo vikuu, jambo linalosababisha wengi wao kuangukia katika wimbi la biashara ya ngono na ushoga na kuufanya ongezeko la maambukzi ya vvu.
Kwa mkoa wa iringa inadaiwa kuwa zaidi ya mashoga 1500 wamejitangaza wenyewe kuendesha biashara haramu ya ngono, jambo ambalo kiafya linadaiwa kuwa ni hatari kwa maambukizi ya virus vya ukimwi.
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Iringa ndiyo wanaonyooshewa kidole kuhusika na biashara hiyo ya ngono na tabia ya ushoga- ambapo shirika la restless development linalojihusisha na masuala ya afya ya uzazi na makuzi kwa vijana- kupitia mradi wa dance for life- limewakutanisha viongozi hawa wa serikali ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa- ili kujadili namna ya kujinasua katika wimbi hilo la ushoga na biashara haramu ya ngono.
Serikali inaona tatizo hilo la ushoga na biashara ya ngono litamalizwa na jamii yenyewe, endapo tu wazazi na walezi watakemea mapema mienendo hatarishi ya vijana wao.
Ushoga ni tabia inayofanywa na baadhi ya wanaume, kwa kujihusisha kimapenzi na wanaume wenzao, suala ambalo kwa kiwango kikubwa linatajwa kuchochewa na mambo ya utandawazi, ambao unaibua mitindo mbalimbali na tabia mpya kila uchwao.
chanzo sadiktv

MKUTANO MKUU WAPIGWA STOP NA MKUU WA WILAYA



Na: Abubakar Khatib (Kisandu), Zanzibar.

Mkutano mkuu wa dharura wa ZFA uliokuwa ukitarajiwa kufanyika leo saa4 asubuhi kwenye uwanja wa Judo Amani umepigwa stop baada ya mkuu wa wilaya ya mjini Abdi Mahmoud Mzee kupitia afisi yake kuagiza kusimamisha mara moja mkutano huo hadi pale taratibu za kisheria zitakapowaruhusu kufanya hivyo.

Afisi hiyo tayari imetoa barua kwa kutaka kusitisha zoezi hilo barua ambayo ameandikiwa Rais wa chama cha mpira wa miguu Zanzibar Ravia Idarous Faina.

Mtandao huu umezungumza na  Afisa habari wa ZFA Ali Bakar na kuthibitisha kutokuwepo kwa mkutano huo baada ya kupokea barua kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini.
“ Kama tunavojua kesho ilikuwa ufanyike mkutano mkuu wa dharura wa ZFA, lakini tumepokea barua kwa kusitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mjini, kwasasa mkutano huo haupo baada ya kupata taarifa kutoka kwa Rais wa ZFA na kunipatia barua hiyo ya kutokuwepo mkutano, kwaiyo mkutano kesho haupo”. Alisema Bakari.

Wajumbe mbali mbali kutokea kisiwani Pemba tayari yamewasili leo hii kisiwani Unguja kwa ajili ya mkutano huo mkuu wa dharura ambao kesho ndo haupo tena .

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



 Kaimu Mkurugenzi wa Habari Mawasiliano na Umma-CUF Ismail Jussa katikati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amewataka Wananchi wa Zanzibar kusubiri Taarifa rasmi ya Matokeo ya mazungumzo yanayowahusisha viongozi wakuu wa kisiasa yanayofanyika Ikulu ambayo amedai kuwa yapo katika hatua za mwisho kumalizika.


Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia Taarifa iliyokuwa ikitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari Mawasiliano na Umma-CUF Ismail Jussa.Katika Mkutano huo Jussa amewataka Wananchi wa Zanzibar kusubiri Taarifa rasmi ya Matokeo ya mazungumzo yanayowahusisha viongozi wakuu wa kisiasa yanayofanyika Ikulu ambayo amedai kuwa yapo katika hatua za mwisho kumalizika.


Kufuatia taarifa iliyotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho iliyokutana Zanzibar juzi, tarehe 27 Desemba, 2015, waandishi wengi wa habari wametupigia simu wakitaka kujua Chama Cha Wananchi (CUF) kimepokea vipi taarifa ile.

Vikao vya CCM ni vikao vya CCM. Si kawaida yetu kutolea taarifa maamuzi ya vikao vya vyama vyengine. Hata hivyo, tunaelewa ni kwa nini kumekuwepo na shauku ya kusikia CUF inasema nini kwa sababu yale yaliyokuwemo kwenye taarifa hiyo yaligusia pia mazungumzo yanayofanyika Ikulu Zanzibar yanayolenga kupata ufumbuzi wa mgogoro wa uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.

Baada ya kuipitia taarifa ya CCM na mengine yaliyoelezwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar wakati akitoa ufafanuzi wa yale yaliyomo kwenye taarifa hiyo, CUF tunapenda kuwaeleza Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla haya yafuatayo:

1. Taarifa yenyewe haionekani kama imeandaliwa na watu makini wala haioneshi kama walioitoa wanajua nini kilichopo. Hilo liko wazi kutokana na taarifa yenyewe kuwa na maudhui yanayopingana ambayo yamekuja kukorogwa zaidi na maelezo yaliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar mbele ya waandishi wa habari na kuoneshwa katika vituo kadhaa vya televisheni:

(a) Taarifa inawataka wanachama wa CCM wajiandae na uchaguzi wa marudio lakini papo hapo inaeleza kwamba kikao kimeridhia mazungumzo yanayoendelea Ikulu Zanzibar. Taarifa haisemi iwapo maamuzi ya vikao vya mazungumzo hayatakuwa na suala la kurudiwa uchaguzi, upi ni mwelekeo wa CCM.

(b) Taarifa inazungumzia uchaguzi wa marudio lakini papo hapo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar anasema CCM haina imani na Tume ya Uchaguzi iliyopo na kwa hivyo uchaguzi huo wa marudio lazima ufanyike chini ya Tume mpya. Baada ya hapo hasemi Tume iliyopo ambayo muda wa utumishi wa Makamishna wake unalindwa kikatiba itaondolewa vipi na Tume mpya itapatikana vipi.

(c) Taarifa inawataka wanachama wa CCM wajiandae na uchaguzi wa marudio lakini Katibu wa itikadi na Uenezi anasema hata usiporudiwa ndani ya siku 90, bado Dk. Ali Mohamed Shein ataendelea kuwa Rais.
Nukta hizi tatu ambazo haziwezi zote kusimama kwa pamoja bila ya kupingana moja dhidi ya nyengine zinaonesha tu ni kwa kiasi gani viongozi wa CCM Zanzibar wamepoteza mwelekeo na hawana uhakika wa nini kitatokea katika kuondokana na mgogoro huu wa kutengenezwa.

2. Taarifa ya CCM haiwasaidii wanachama wa CCM wala wananchi wa Zanzibar kwa kuwapa matumaini ya kumalizika kwa mgogoro wa kutengenezwa wa uchaguzi wa Zanzibar na badala yake inaonekana imelenga kuwachanganya zaidi wananchi kwa maelezo yanayopingana.

3. Taarifa inaonyesha ni jinsi gani CCM kilivyopoteza mvuto kwa kujiweka mbali na wananchi. Taarifa hiyo inapongeza eti kuwepo kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii wakati wananchi wa Zanzibar, bila ya kujali itikadi zao za kisiasa, siyo tu wanumia kutokana na sera mbovu za CCM lakini sasa wanazidi kuteketea na maisha yao kuwa magumu zaidi kutokana na fadhaa (tension) na taharuki iliyopo katika nchi kutokana na kutokuwepo kwa Serikali yenye ridhaa yao. Harakati za maisha zimeathirika sana huku bidhaa vikiwemo vyakula vikipanda bei. Viongozi wa CCM hawaonekani kujali hali hii mradi wao yao yanawaendea. Tabia hii ya CCM kutowajali wananchi wanyonge wa nchi hii ndiyo iliyopelekea wananchi kukiadhibu chama hicho katika uchaguzi mkuu na kupelekea mgombea wake wa Urais wa Zanzibar na wagombea Uwakilishi kushindwa vibaya kwa tofauti ya zaidi ya kura 25,831.

4. Taarifa inaendeleza utamaduni wa unafiki wa kisiasa kwa eti kuwapongeza viongozi wa CCM na jumuiya zake kwa kazi ya kukiimarisha chama chao huku wakijua kwamba viongozi wao hasa wale walioongoza Kamati ya Kitaifa ya Kampeni za CCM Zanzibar walishindwa kazi na kupoteza mwelekeo. Matokeo ya kazi mbovu ya Kamati ya Kampeni ya CCM Zanzibar ni kukisababishia chama hicho kipigo kikubwa katika uchaguzi huo kilichopelekea kushindwa katika nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa zaidi ya kura 25,831 na kupoteza viti tisa (9) vya Uwakilishi kisiwani Unguja mbali ya kutopata hata kiti kimoja kisiwani Pemba. Viongozi hao walishindwa kuwajibika licha ya kutumia mabilioni ya fedha walizopewa kwa ajili ya kampeni.

5. Katika maelezo yake ya ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar anaitupia lawama Tume nzima ya Uchaguzi ya Zanzibar kwa kushindwa kazi huku akijua na ikijulikana na kila mmoja kwamba tamko la kufuta uchaguzi limetolewa na Jecha Salim Jecha kinyume na Katiba, kinyume na Sheria ya Uchaguzi na kinyume na maadili ya kazi yake. Katiba inataka Jecha achukuliwe hatua za kufukuzwa kazi kwa kuanza na kumuundia Tume Maalum ya kumchunguza, na siyo kutafuta mbinu za kumlinda kwa kuwaingiza wasiokuwemo.

6. Maelezo ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar kwamba Dk. Ali Mohamed Shein ataendelea kuwa Rais hata baada ya miezi mitatu ni kielelezo na ushahidi mwengine wa jinsi CCM isivyoheshimu Katiba. Kwa hakika, hili suala la kutaja siku 90 ambalo linatajwa sana na CCM na wapambe wake haijulikani hata linatokea wapi. Hakuna pahala popote katika Katiba ya Zanzibar wala Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar panapotajwa sharti la kurudiwa uchaguzi ndani ya siku 90 kwa sababu Katiba yenyewe na Sheria ya Uchaguzi haina sehemu yoyote inayozungumzia kufuta uchaguzi na kufanya uchaguzi wa marudio.

7. Kwa ujumla, taarifa ya CCM Zanzibar iliyotolewa na Katibu wake wa itikadi na Uenezi inaonyesha jinsi chama hicho kisivyojali madhila wanayoyapata raia, fedheha iliyopata taifa na hali ya kiuchumi inayozidi kudorora kila siku Zanzibar ikiwaathiri mno wananchi wanyonge.

Baada ya uchambuzi huo wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, CUF inapenda kuwaeleza Wazanzibari yafuatayo:

1. Waipuuze taarifa hiyo ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar kwani haina lolote jipya zaidi ya kutaka kufunika kombe kutokana na hali ngumu inayotokana na hoja za viongozi wa ngazi za chini na wanachama wa CCM wanaotaka maelezo ya kwa nini chama hicho licha ya kutumia mabilioni ya shilingi kimeshindwa vibaya katika uchaguzi mkuu.

2. Wazanzibari wasubiri taarifa rasmi ya matokeo ya mazungumzo yanayowahusisha viongozi wakuu wa kisiasa yanayofanyika Ikulu Zanzibar ambayo yamo katika hatua za mwisho kumalizika.

3. Wampe nafasi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John Pombe Magufuli, ambaye anaendelea na juhudi katika ngazi za juu kabisa za kuhimiza kupatikana ufumbuzi wa haraka wa mgogoro wa uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015.

4. CUF inawahakikishia Wazanzibari kwamba haitotetereka na itasimamia kwa dhati maamuzi yao waliyoyafanya kwa njia za kidemokrasia kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na italinda chaguo lao la Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani wao.

5. Mwisho kabisa, inaendelea kuwapongeza Wazanzibari kwa kuonesha ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa na kuendelea kutunza amani na utulivu wakati wakisubiri matokeo ya kazi kubwa waliyoifanya tarehe 25 Oktoba, 2015 ambayo inaashiria ujenzi wa Zanzibar Mpya.

HAKI SAWA KWA WOTE

ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO NA UMMA – CUF
29 DESEMBA, 2015

KOMBE LA MAPINDUZI YATOA RATIBA, YANGA NA AZAM KUNDI MOJA , SIMBA YUPO NA MBABE WA YANGA “JKU”




Na: Abubakar Khatib (Kisandu), Zanzibar.

Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza rasmi visiwani Zanzibar  siku ya Jumamosi ya tarehe 02/01/2016 kati ya JKU na URA wakati wa Saa 10:15 jioni na saa 2:15 usiku watacheza kati ya Simba ambae ndie bingwa mtetezi dhidi ya Jamhuri kutoka Wete Kisiwani Pemba michezo yote itasukumwa kwenye dimba la Amaan.

Katika mashindano hayo yamejumuisha timu nane, tatu kutoka Visiwani Zanzibar ambao ni JKU, Mafunzo na Jamhuri ambapo pia timu 4 kutoka Tanzania bara zikijumuishwa Simba (Bingwa mtetezi), Yanga, Azam, na Mtibwa Sugar na timu kutoka nje ya Tanzania ni moja tu ambayo ni URA ya Uganda.

Timu hizo 8 zimegawanywa kwenye makundi mawili “A” na “B” kwa kila moja timu 4.

Kundi “A” kuna timu ya Simba, Jamhuri, JKU na URA, wakati kundi “B” kuna timu ya Yanga, Mafunzo, Azam na Mtibwa Sugar.

Timu 2 bora kwa kila kundi zinatarajiwa kutinga nusu fainali na zitakozofanikiwa kuingia fainali zitacheza fainali tarehe 13/01/2016 saa 2:15 kwenye dimba la Amaan.

Wednesday, December 23, 2015

TAARIFA ZA ULEMAVU WA KASSIM IMAN MOHAMMED.



Kassim Iman Mohammed ni mtoto wa miaka 14 anaeishi chini ya uangalizi wa wazee wake wote wawili, baba na mama.Anaishi kijiji cha Mbuguani, katika Shehia ya Mbuguani, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba.Kassim ni mtoto watano kwa kuzaliwa katika familia yenye watoto nane.
Chanzo cha matatizo ya Kassim yalijitokeza usiku wa manane baada ya yeye kuamka kwa lengo la kwenda kujisaidia akahisi maumivu makali kwenye misuli ya miguu yote miwili ambapo alishindwa kusimama na kumwamsha mama yake mdogo ambaye akiishi naye kwa kumpatia msaada.
Historia ya matatizo ya Kassim yalianza pole pole pale ishara na dalili za maumivu endelevu kuonekana  kila alipokuwa akitembea masafa ama kufanya mazoezi na wenzake. Misuli yake ilikuwa ikimuuma kwa sana na kuonyesha kuvimba kwa kiasi.
Kwa upande wa matibabu baada ya kuonekana tatizo la maumivu na kuvimba misuli linaendelea, wazazi wake walimpeleka Hospitali ya Abdalla Mzee ya Mkoani Pemba ambapo alipewa rufaa ya kwenda Hospitali  nyengine ambapo walimpeleka Hospitali ya Temeke –Dar es salam. Nayo  Hospitali ya Temeke ilimpa rufaa ya kumrejesha Hospitali Kuu ya Taifa ya Mnazi Mmoja –Zanzibar.
Aidha ushauri uliotolewa Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa kijana huyo ni kufanya zoezi kwa bidii ili aondokane na kadhia hiyo. Aliendelea vizuri kwa muda wa mwaka mmoja hapo hapo Unguja lakini hatima yake ikaishia kuganda na kuvimba misuli kwa ghafla.
Kwa upande wa elimu, Kassim ni mwanafunzi wa darasa la 5 katika Skuli ya Msingi ya Matetema katika kijiji cha Kazole huko Unguja. Aidha Kassim alichukuliwa uhamisho wa kimasomo toka Skuli ya Msingi Ng’ombeni B- Mkoani Pemba.

Hali ya sasa ya Kassim ni mbaya sana na inasikitisha kabisa kwani misuli ya miguu yake imevimba na yenye kumpa maumivu makali unapojaribu kumsimamisha na anaonekana kudhoofika kiafya kadri siku zikisonga mbele. Amekuwa mlemavu tayari, ni kweli sote ni walemavu watarajiwa kwani mtoto Kassim alikuwa yuko makini na mwenye afia nzuri miezi minne iliyopita. Allah ampe wepesi ili aweze kushiriki katika maendeleo ya Taifa letu, AMIN.        

MKUTANO MKUU WA DHARURA ZFA WAINGIA KIDUDU.



Na: Abubakar Khatib (Kisandu), Zanzibar.
Baada ya jana Jumannne kutangazwa tarehe ya kufanyika mkutano mkuu wa dharura wa ZFA hatimae leo yameibuka mengine mapya.
Makamo wa Urais Unguja wa chama cha mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) Haji Ameir “Mpakia” ameibuka na mapya kwa kusema mkutano mkuu hautokuwepo siku ya Jumapili ya tarehe 27 Disemba na utatangazwa tarehe nyengine mpya ya mkutano huo.
Aliyasema hayo wakati alipozungumza na waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Migombani Zanzibar.
“ Mkutano tarehe 27 Disemba hautokuwepo kwasababu sisi viongozi wengine wa juu wa kamati tendaji hatujui, na ZFA haina pesa ya kuendesha mkutano mkuu, pesa tutazipata wapi?, kwaiyo mkutano huo haupo mimi kama makamo wa Urais Unguja ZFA Haji Ameir nasema mkutano haupo”. Alisema Mpakia.
Katika barua ya kuahirishwa mkutano mkuu wa dharura wa ZFA yenye kumbukumbu namba Ref.ZFA/MMM/VOL.1/214 barua ambayo imeandikwa tarehe 22/12/2015 ambapo imesainiwa na wajumbe 8 wakiwemo Haji Ameir, Abdulghan Msoma, Massoud Attai, Ali Bakar, Ahmada Haji, Hashim Salum, Khatma Mwalim na Hussein Ali.
Lakini cha kushangaza Afisa Habari wa ZFA Ali Bakar ambae jana ndio alietoa taarifa ya kuwepo mkutano huo, yumo katika wajumbe 8 waliosaini kutokuwepo kwa mkutano huo, mtandao huu ukamtafuta tena Afisa Habari huyo na kutaka kujua vipi mbona wanawachanganya wadau wa soka , mara mkutano upo, mara haupo, Afisa Habari huyo alizidi kusisitiza kuwa mkutano upo licha ya kuwa na yeye yumo kwenye wajumbe 8 waliotia saini kwa kukataa mkutano kutokuwepo.
“ Mkutano upo siku ile ile ya jumapili ya Disemba 27 na pale pale Aman Judo tutafanya, mimi kweli nimetia saini ya kukataa kutokuwepo mkutano huo, lakini ni shindikizo tu la kutakiwa nisaini , lakini mimi kwenye kikao hicho sijakuwepo nililazimishwa tu, kama afisa habari wa ZFA nasema mkutano upo kama kawaida mpaka anipe taarifa Rais wangu kuwa mkutano haupo. Alisema afisa habari wa ZFA Ali Bakar Cheupe.
Jana afisa habari wa ZFA alitoa taarifa za kuthibitisha kuwepo mkutano huo huku akisema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya rais wa chama hicho Ravia Idarous Faina kupata baraka za kamati tendaji za ZFA juu ya kufanyika mkutano huo.
Ajenda kuu kwenye mkutano huo kama ilivyokubaliwa ndani ya kikao cha pamoja kilichosimamiwa rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi ni kuunda kwa kamati maalum ya kushughulikia katiba ya ZFA, Kupitia mahesabu ya ZFA na kuangalia utendaji wa kamati tendaji ya chama hicho.
Shirikisho la soka Tanzania TFF lililazimika kuingilia kati mtafaruku wa soka visiwani Zanzibar baada ya barua kutoka Shirikisho la soka barani Afrika CAF kutishia kuifungia Zanzibar.

ZANZIBAR SAND HEROES YARUDI NYUMBANI NA USHINDI WA PILI.


Na: Abubakar Khatib (Kisandu), Zanzibar.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar kwa soka la Ufukweni (Sand Heroes) kimerejea visiwani zanzibar na kombe la ushindi wa pili kwenye mashindano ya Afrika ya soka la Ufukweni yaliofanyika nchini Kenya hivi karibuni.
Katika mashindano hayo Zanzibar Sand Heroes imeshinda nafasi ya pili kufuatia kufungwa kwenye fainali na timu ya Kenya “A” kwa jumla ya mabao 10-9.
Baada ya kurejea visiwani timu hiyo mtandao huu ulizungumza na kocha msaidizi wa timu hiyo Kijo Nadir Nyoni na kusema kuwa wao wamefurahi kupata nafasi ya pili kwenye mashindano makubwa kama hayo.
“ Tumefurahi sana kupata nafasi ya pili, lakini uwezo mkubwa tulikuwa nayo kurudi na kombe lakini si bahati yetu, ila tutajipanga tena kuwaonesha wazanzibar kuwa sisi tunaweza kuwakilisha vyema kuliko mchezo mwengine kama mpira wa miguu”.
Hata hivyo Kijo alielezea siri ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo ambapo alisema wazanzibari wanaoishi Kenya waliwaunga mkono sana na kuishangiria timu yao.
“ Tunawashukuru sana wazanzibar wanaoishi Kenya na hata wale wengine ni wa Kenya lakini wazee wao wengine wazanzibar, katika mji wa Malindi kule Kenya tulijiona kama tupo Zenj mana jamaa zetu waliokuwepo kule wametushangiria siku zote na tukajiona tupo nyumbani”. Alisema Kijo.
Mbali ya ushindi wa pili kupata timu hiyo ya Zanzibar, pia wametoa mchezaji bora kwenye mashindano hayo ambapo alikuwa ni Talib Ame pia alifanikiwa kufunga mabao 14 na kuzawadiwa medali ya dhahabu.
Mashindano hayo yalifanyika Kilifi Mtaa wa Malindi nchini Kenya ambapo yalianza tarehe 18 Disemba na kumalizika tarehe 20 Disemba huku bingwa walifanikiwa timu ya Kenya “A”

Tuesday, December 22, 2015

HAKUNA ATAKAYEKOPWA KARAFUU ZAKE.

MKURUGENZI MWENDESHAJI WA SHIRIKA LA BIASHARA LA TAIFA ZANZIBAR (ZSTC) BI. MWANAHIJA ALMAS ALI AMEKANUSHA UZUSHI UNAODAI KUWA SHIRIKA LA ZSTC LIMEISHIWA FEDHA ZA KUNUNULIA KARAFUU NA KUWAKOPA WAKULIMA KARAFUU ZAO.
AKIZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI MAKAO MAKUU YA SHIRIKA MAISARA ZANZIBAR, BI. MWANAHIJA AMESEMA PAMOJA NA KUONGEZEKA KWA MANUNUZI YANAYOTOKANA NA KUONGEZEKA KWA UZALISHAJI KATIKA MSIMU WA 2015/2016 SHIRIKA LINAPESA ZA KUTOSHA ZA KUNUNULIA KARAFUU ZOTE KATIKA MSIMU MZIMA NA HAKUNA MKULIMA YOYOTE ALIYEKOPWA.
AMESEMA SHIRIKA TANGU KUANZISHWA KWAKE MWAKA 1968 HALIJAWAHI KUWAKOPA WAKULIMA NA AMESEMA KUWA MADAI HAYO NI UZUSHI USIOKUWA NA UKWELI WOWOTE.
AMESEMA ZSTC NI SHIRIKA LA SERIKALI HIVYO KAMA LIKIPUNGUKIWA NA FEDHA ZA MANUNUZI YA KARAFUU SERIKALI INA UWEZO WA KULIPA FEDHA ZA KUTOSHA ZINAZIHITAJIKA NA SIO KUWAKOPA WAKULIMA.
AIDHA AMESEMA HAKUNA MKULIMA ALIYEKOPWA NA WALA HAKUNA SHIDA YA KUKOPA KUTOKA TAASISI ZA KIFEDHA KWA VILE SHIRIKA LIMESHAJIPANGA VIZURI KUNUNUA KARAFUU ZOTE KUTOKA KWA WAKULIMA KWA FEDHA TASLIMU.
HATA AMEWATAKA WAKULIMA WA ZAO LA KARAFUU KUTOKUWA NA WASI WASI WOWOTE JUU YA MANUNUZI YA KARAFUU ZAO NA AMEWATAKA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA KATIKA KULIHUDUMIA ZAO VIZURI.
BI. MWANAHIJA AMEFAHAMISHA KUWA MANUNUZI YAMEONGEZEKA MWAKA HUU WA 2015/2016 KINYUME NA ILIVYOKADIRIWA AWALI KUTOKANA NA HALI YA HEWA KUBADILISHA MSIMU WA MWAKA KUWA MSIMU WA VULI AMBAO HUWA NI MSIMU MKUBWA.
SABABU NYENGINE ALIZOZITAJA KUWA NI UZAZI WA MIKARAFUU MIDOGO ILIYOPANDWA KATI YA MWAKA 2005 HADI 2013 AMBAPO MIKARAFUU HIYO TAYARI IMEANZA KUZAA VIZURI NA KUONGEZA UZALISHAJI.

SAMBAMBA NA HAYO PIA AMESEMA KUANZISHWA KWA MFUKO WA MAENDELEO YA KARAFUU IMEKUWA NI HATUA NYENGINE MUHIMU YA KUONGEZEKA KWA UZALISHAJI WA ZAO LA KARAFUU KUTOKANA NA KAZI NZURI ZINAZOFANYWA NA MFUKO HUO ZA KUSHAJIHISHA WAKULIMA KUIMARISHA ZAO HIO.

JENERETA LAZUA TAHARUKI HOSPITALI KUU YA ZANZIBAR MNAZIMMOJA

ZANZIBAR
GENERATOR  LINALOTUMIKA  KATIKA  HOSPITALI YA MNAZI MMOJA  LIMENUSURIKA  KUUNGUA   KUTOKANA NA KUFANYA KAZI KWA MUDA MREFU  TOKA JANA BAADA  YA  SHIRIKA LA UMEME  ZANZIBAR  KUKATA  UMEME  KATIKA  BAADHI YA MAENEO YA KISIWA CHA ZANZIBAR.
HALI HIYO ILIZUA TAARUKI KWA WAGONJWA NA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI HIYO BAADA YA KUTOKEA KWA MOSHI   KATIKA  GENERATOR   HILO  ULIOZAGAA  KATIKA MAENEO MBALIMBALI  YA HOSPITALI HIYO.
FUNDI WA GENERATOR HILO AMBARE HAKUTAKA JINA LAKE LIANDIKWE KATIKA  VYOMBO VYA HABARI AMESESEMA KUWA KUFANYA KAZI MUDA MREFU  BILA YA KUPUMZISHWA  NDIYO SABABU  YA KUTOKEA  KWA MOSHI HUO   KUTOKANA NA KUWEPO KWA JENERATOR MOJA KATIKA  HOSPITALI HIYO.
HATA HIVYO MAFUNDI WALIOKUWEPO KATIKA HOSPITALI HIYO WALILIZIMA GENERATOR HILO BILA YA KUTOKEA  ATHARI YEYOTE  KWA WAGONJWA WALA WAHUDUMU WA AFYA WA HOSPITALI HIYO.

KUTOKANA NA HALI HIYO NI  VYEMA SERIKALI KUANGALIA   GENERATOR  HILO IKIWEZEKANA KUONGEZA GENERATOR  LINGINE  ILI KUNUSURU  MAISHA YA WAGONJWA WANAOPATIWA HUDUMA   KATIKA HOSPITALI HIYO.

Saturday, December 19, 2015

MKUU WA CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA) AWATUNUKU SHAHADA, STASHAHADA NA VYETI WAHITIMU 691 KATIKA MAHAFALI YA KUMI NA MOJA KAMPASI YA TUNGUU.

 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia wanafunzi, wazazi  na wageni waalikwa  katika Mahafali ya kumi na moja YA Chuo hicho yaliyofanyika Kampasi ya Tunguu Mkoa Kusini Unguja.
Picha na Makeme Mshenga-Maelezo Zanzibar.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akimtunuku Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Kemia Khamis Mohammed Saidi kwenye mahafali ya kumi na moja yaliyofanyika Kampasi ya Tunguu Mkoa Kusini Unguja.
 Mwanafunzi aliefanya vizuri zaidi katika Mahafali ya kumi na moja ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Rauhiya Ahmed Hamdun akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiutangazia mkusanyiko uliokuwepo kiwanja cha Kampasi ya Tunguu kuwa ni Mahafali ya kumi na moja ya Chuo hicho, (kulia) Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Said Bakari Jecha na kushoto Makamu Mkuu wa chuo Prof. Idriss Ahmad Rai.

Maandamano ya wahitimu wa Mahafali ya kumi na moja ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) yakiingia katika kiwanja cha Mahafali  hayo yaliyofanyika Kampasi ya Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja. Picha na Makeme Mshenga-Maelezo Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amekitaka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kuendelea kufanya tafiti kwa kuzingatia mahitaji yaliyopo na kuhakikisha kuwa matokeo ya tafiti hizo yanasambazwa kwa taasisi na sekta zinazohusika na yanatumika ipasavyo katika mipango ya maendeleo.

Dk. Shein aliyasema hayo leo huko katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), kiliopo Tunguu, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja katika Mahafali ya Kumi na Moja ya Chuo hicho baada ya kuwatunuku vyeti wahitimu 699 katika fani 15 wakiwemo 7 wa Shahada ya Uzamili ya Sayasi katika Kemia.

Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa ameridhishwa sana na dhamira na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na SUZA hivi sasa za kuimarisha shughuli za utafiti na ubunifu kwani amekuwa akihimiza ufanyaji wa utafiti kila mahali na ndio maana akaanzisha Idara za utafiti kwa kila Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Dk. Shein alisema kuwa kwa kufanya hivyo itakuwa ni rahisi kutimiza dhamira ya chuo hicho ya kukifanya kuwa kinaongoza katika Ukanda wa Afrika Mashariki kwa utoaji wa taaluma bora, ufanyaji wa tafiti na kukuza ubunifu katika fani mbali mbali.

“Matunda ya jitihada zenu tayari yanaonekana tukijua kwamba wakati vyuo vyengine vinakosa waombaji wa kujiunga na masomo, SUZA imepata zaidi idadi inayohitajika tena wakiwa na sifa nzuri zaidi ya viwango vilivyowekwa”,a lsiema Dk. Shein.

Aidha, Dk. Shein alikitaka chuo hicho kuendeleza utamaduni wa kuzishirikisha taasisi za Serikali katika mafunzo mbali mbali yanayotolewa Chuoni kupitia miradi iliyopo kila inapotokezea fursa za aina hiyo kwani utamaduni huo utasaidia sana juhudi za Serikali za kuwajengea uwezo watumishi wa Umma.

Dk. Shein pia, alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa SUZA pamoja na wahitimu kwa ongezeko la wahitimu wa fani nyengine tatu mpya ambazo ni Stashahada ya Usimamizi wa Urithi wa Kale na Utalii, Stashahada ya Ukutubi na Shahada za Uzamili ya Kemia.

Alisema kuwa kupata wahitimu katika kiwango cha Shahada ya Uzamili, katika masomo ya Sayansi kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar ni tukio kubwa na la kutia moyo.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alisema kuwa sekta ya utalii hivi sasa ndiyo sekta kiongozi kwa uchumi wa Zanzibar hivyo matumaini yake ni kuwa wahitimu wa fani ya Usimamizi wa Urithi wa Kale na Utalii watakuwa ni chachu ya mabadiliko na watasaidia kukabiliana na vyema na changamoto za usimamizi wa maeneo ya urithi wa kale.

Aidha, wahitimu wa diploma ya ukutubi watasidia kwa kiasi kikubwa kufikia azma ya Serikali ya kuanzisha maktaba katika skuli zote za Sekondari na msingi na kutoa wito kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kufanya jitihada za kuwaajiri na kuwaenzi vijana hao pale hali itakaporuhusu ili waweze kutoa mchango wao katika fani hiyo.

Dk. Shein alisema kuwa amevutiwa na taarifa za maandalizi ya kuanzisha masomo ya fani mbali mbali katyika ngazi ya Uzamili kama vile Usimamizi wa Mali Asili na Tabianchi pamoja na ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni.

Alisema kuwa ni wazi kwamba licha ya mafanikio hayo yaliopatikana hadi sasa, uongozi wa chuo unahitaji kuendelea kuongeza kasi kwa kufanya kazi kwa umakini na ubunifu wa hali ya juu, kwani Serikali na wananchi wanategemea maendeleo makubwa zaidi katika Chuo hicho.

Sambamba na hayo, Dk. Shein alsiema kuwa Wizara Ya Elimu pamoja na Uongozi wa Chuo wamefikia hatua nzuri ya kulifanyia kazi agizo la Serikali la kuziunganisha na SUZA taasisi tatu za elimu ya juu ikiwemo Chuo cha Taalamu za Sayansi za Afya kiliopo Mbweni, Chuo cha Uongozi wa Fedha na Chuo vcha Utalii Maruhubi.

Katika hotuba yake hiyo pia, Dk. Shein alieleza kufurahishwa kwake na juhudi za SUZA za kuimarisha fursa za elimu kwa wanawake kwani katika mahafali hiyo sehemu kubwa ya wahitimu ni wanawake ambao ni sawa na asilimia 64.2 ambapo pia mwanafunzi wa kike kwa mara nyengine tena ndie aliyefanya vizuri katika masomo ya sayansi.

Dk. Shein pia, aliueleza uongozi wa SUZA kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi zao ili malengo ya kuanzishwa kwa Kampasi ya Benjamin William Mkapa iliyopo Mchanga Mdogo Pemba, yaweze kufikiwa  huku akiwataka wananchi wa Pemba waitumie fursa hiyo huku Serikali ikiwa na nia ya kuanzisha Chuo Kikuu kisiwani humo.

Katika nasaha zake kwa wahitimu hao, Dk. Shein aliwataka kila mmoja kuhakikisha anajiwekea malengo ambayo yatakuwa na tija kwake mwenyewe, familia, jamii na nchi kwa jumla sambamba na kupanga mikakati ya kuyafikia malengo hayo.

Pia, aliwataka wahitimu kuendelea kuwa waadilifu na wazalendo kwa nchi yao na kuwahimiza hasa kwa wale wote walioomba mikopo Serikalini na wakakopeshwa, kufanya juhudi za kurejesha mikopo hiyo kwa mujibu wa sheria na makubaliano yaliopo ili fedha hizo ziweze kuwasaidia wanafunzi wengine wanaotaka kujiendeleza.

Pia, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuiagiza Wizara ya Fedha, Wizara ya Elimu pamoja na Tume ya Mipango kukaa pamoja na kuhakikisha katika mahafali kama hiyo hapo mwakani  inafanyika katika ukumbi maalum badala ya maeneo yanayofanyika hivi sasa.

Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Ali Juma Shahuna alieleza juhudi zinazofanywa na Serikali kupitia Wizara yake katika kutoa mashirikiano na chuo hicho na kumpongeza Dk. Shein kwa uongozi wake na juhdui zake za kukisimamjia na kukionoza chuo hicho akiwa Mkuu wa Chuo hicho.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idrisa Ahmada Rai, alimueleza Dk. Shein mikakati iliyowekwa na chuo hicho sambamba na mafanikio yaliopatikana  ikiwa ni pamoja na kuanzisha televisheni ya chuo hico (SUZA TV) itakayotumika kutoa taaluma ya masomo ya sayansi kwa skuli za Sekondari za Zanzibar sambamba na kuitumia TEHAMA kwa kufundishia.


Pamoja na hayo, alieleza azma ya ujenzi wa daghalia kwa mashirikiano ya ZSSFna PBZ pamoja na majengo mengine ya chuo hicho. Aidha, alieleza mafanikio ya wanawake chuoni hapo na kupongeza kwa jinsi wanavyofanya vizuri katika masomo yao. 

Friday, December 18, 2015

Uhai ni maisha na maisha ni uhai

Na Pili Khatib na Zuhura Omar, MUM


Uhai ni maisha na maisha ni uhai ili kuwa na uhai tunahitaji chakula na chakula bora ni chakula kinachotokana na kilimo hai, kilimo hai ni kilimo kilicho bora zaidi. Je unakifahamu kilimo hai?
Kilimo hai au organic farming ni aina ya kilimo kinachozingatia matumizi endelevu ya rasilimali za uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo. Kilimo hicho kinatumia mbolea na madawa yasiyotengenezwa viwandani na kinazingatia utunzaji wa mazingira kwa ajili ya manufaa kwa jamii, kiuchumi na kiafya.
Tumeirithi ardhi kutoka kwa vizazi vilivyotangulia ikiwa na ubora wa asili, lakini kutokana na matumizi ya muda mrefu, ardhi huzeeka na kushindwa kutoa mazao bora, hivyo kumfanya binadamu kutafuta namna nyingine ya kuifanya ardhi hiyo itoe mazao mengi.
Baada ya kuona ardhi imechoka Wakulima wengi huamua kutafuta maeneo mengine yaliyo bora na kuanza kuyatumia. Wakati mwingine hulazimika kufyeka misitu ili kupata mashamba mapya, hali ambayo siyo tu inaharibu mazingira, lakini pia inaweza kututia umaskini wa milele kwa sababu ardhi iliyoachwa awali huwa haitafutiwi njia muafaka ya kuifanya irejee kwenye ubora wake.
Wakulima wengine hutafuta mbolea, hasa za chumvi chumvi, na kuzitumia katika ardhi ile inayoonekana kuzeeka. Lakini matatizo mengi huibuka kutokana na matumizi ya mbolea pamoja na madawa ya kemikali kwenye kilimo.
Mbolea hizo zina kemikali na madawa ya kuua wadudu yana madhara yake kwani yana sumu isiyoonekana. Sumu hiyo tunakula au tunakunywa na ndizo zinazoleta madhara kwa binadamu na udongo.
Mazao yanayotokana na kilimo cha mbolea za kemikali yanaleta athari kubwa zisizoonekana kwa binadamu na hata wanyama. Lakini jambo la kuzingatia kwa sasa, kila mtu anatakiwa kuvuta kumbukumbu zake kulingana na umri alioishi na kuangalia yafuatayo: Hali ya udongo enzi zile na sasa ikoje? Kiwango cha maradhi wakati ule na sasa kikoje? Uwezo wa udongo kuzalisha mazao umepungua au unazidi mwaka hadi mwaka.
Inaonyesha kuwa mbolea za chumvichumvi zimechakaza udongo na hivyo kufanya uzalishaji upungue. Hata mazao yanayotokana na matumizi ya mbolea hizo yamekosa ubora wa asili unaotakiwa.
Hali hiyo inatia shaka kama umaskini wa Mkulima utakwisha ikiwa hatabadili aina ya pembejeo kuokoa ardhi yake isizidi kuchakaa na wakati huo huo kupunguza sumu isiyoonekana kwenye udongo na vyanzo vya maji.
Ni ukweli usiopingika kwamba, mbolea za chumvi chumvi zikiisha muda wake hugeuka sumu na baadaye Mkulima analazimika kutumia gharama kubwa kuweka mbolea za mboji ili kurudisha udongo katika hali nzuri. Sumu hii isiyoonekana inaharibu udongo, vyanzo vya maji na hata mwili wa binadamu wanaotumia vyakula hivyo.
Katika Mataifa yaliyoendelea, mbolea za chumvi chumvi zinatumika kupandia na kukuzia miti, hasa ya mbao. Vile vile inatumika kutengenezea mazingira kwa maeneo ambayo hayatumiki kuzalisha mazao ya chakula cha binadamu.
Wao wamekuwa wakipiga sana vita vyakula vilivyolimwa kwa kutumia mbolea za chumvi chumvi na ndiyo maana hivi sasa katika soko la dunia bidhaa zilizozalishwa kwa kutumia mbolea hizo za chumvi chumvi zimekuwa zikiuzwa kwa bei ya chini kuliko zile zinazolimwa kwa kutumia kilimo hai.
Sasa tujiulize, kwa nini sisi tunaendelea kutumia mbolea hizo zinazoua udongo wetu na kuweka sumu? Hivi hakuna mbolea nyingine mbadala? Jibu ni kwamba, mbolea mbadala zipo.
Mbolea mbadala ni zile zinazotokana na marejea na uozo wa asili, uozo wa asili unaotokana na majani mbalimbali, samadi ya mifugo asili, mabaki ya nafaka au mazao mbalimbali (kama maganda na mabua ya mahindi na mpunga).
Mbolea hizi zinaweza kupatikana au kutengenezwa katika mazao tunayolima, kwenye mazingira tunayoishi. Mbolea hizi zinasaidia kurudisha udongo katika hali ya rutuba na asili yake na gharama za mbolea hizi ni nafuu kabisa na zinadumu ardhini kwa muda mrefu.
Mazao yatokanayo na kilimo cha mbolea za kemikali hayana bei kubwa katika soko la dunia ikilinganishwa na mazao yatokanayo na kilimo hai, ambacho kwa sasa ndicho kinachohamasishwa ulimwenguni kwa sababu kinatumia viuatilifu asilia ambavyo siyo tu vinaongeza tija ya mazao, lakini pia ni rafiki wa mazingira.
Kwa mfano, wastani wa bei ya karafuu ya kilimo hai ni TZS 170,000 kwa kilo ambayo ni asilimia ya bei ya karafuu isiyo ya kilimo hai kutoka Shirika la ZSTC.
Ili bidhaa zikubalike katika Soko la Kimataifa kuwa zimezalishwa kwa kutumia mbinu za kilimo hai, zinapaswa kwanza kupitishwa na Taasisi zinazosimamia ubora wa bidhaa hizo.
Wazalishaji wa mazao ya kilimo hai huwa hawachanganyi mazao ya kilimo hai na yale ya kawaida, hivyo hutumia  kanuni za kilimo hai katika kusindika mazao katika mfumo huo wa kilimo hai.
Kilimo hai Tanzania kilianza kupata umaarufu katika miaka ya 1990 baada ya Serikali kuruhusu Taasisi kadhaa za Serikali na zisizo za Kiserikali (NGOs) kueneza elimu na teknolojia za kilimo hai kwa Wakulima nchini.
Kwa upande wa Zanzibar Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar ZSTC limeanzisha na kuendeleza mradi wa mazo ya kilimo hai ambapo kwa hatua ya awali Shirika limeanza na mazao manne (4) ya viungo ambayo ni Karafuu, Pilipili manga, Mdalasini na Pilipili hoho.
Hii ni habari njema kwa Wakulima wa Zanzibar kwani mazao ya kilimo hai  yanafaida kubwa kwa Afya ya mtumiaji na yana bei nzuri hasa katika soko la nje hivyo ni vyema Wakulima wakachangamkia kilimo hicho  kwa ajili ya kuongeza kipato na kukuza uchumi wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika hilo la Biashara Zanzibar Mwanahija Almas Ali mpango wa kilimo hai ni Mradi maalumu wenye lengo la kuwaongezea kipato Wakulima Nchini.
Hivyo Shirika la ZSTC limeunga mkono juhudi za Serikali katika kuendeleza kilimo hai kwani ambapo linaitoa elimu kwa Wakulima na Wasindikaji wa mazao ya kilimo hai ya Karafuu, Pilipili manga, Pilipili hoho na Mdalasini.
Kanuni ni maelekezo ya utekelezaji wa mambo ili yaende sawa kama yanavyotakiwa na kanuni hufuatwa kwa ajili ya kufikia malengo yaliyokusudiwa. Kilimo hai kina kanuni zake ambazo kila Mkulima anawajibu wa kuzifahanu na kuzifuata.
Kanuni hizo ni kanuni za Afya, mazingira, kuhifadhi udongo, haki na usawa na kanuni ya uangalizi ambazo zote hizo ni muhimu katika kuweka uwazi katika mfumo wa kilimo hai.
Ni lazima kuzingatia kanuni hizo za  kilimo hai katika kulinda ubora wa mazao ya kilimo hai ya Karafuu, Mdalasini, Pilipili hoho na Pilipili manga kuanzia kuyapokea kutoka kwa Mkulima hadi yanachambuliwa na hatimaye kuhifhadhiwa na kusafirishwa kuelekea sokoni.
Miongoni mwa kanuni hizo ni kuwepo na orodha ya Wakulima waliopasishwa kwa kilimo hai katika msimu husika na kuwepo kwa orodha ya Wakulima walioruhusiwa kuuza mazao ya kilimo hai ambapo wamepasishwa baada ya ukaguzi wa nje.
Kanuni nyengine ni kuwepo taarifa ya kiasi kinachohitajika kupokelewa na kilichokuwepo. Kuwepo kwa orodha ya Wakulima waliouza mazao ambayo yanapokewa kwa hati za kusafirishia mazao hayo.
Wakati wa kupokea mazao kutoka kwa Wakulima wa kilimo hai lazima kuzingatia uwepo wa usahihi wa nyaraka na kumbukumbu hizo za kila Mkulima wa kilimo hai.
Katika ufungashaji, mazao ya kilimo hai hufungashwa kwa vifungashio maalum vinavyokubalika kitaalumu na inatakiwa iwekwe nembo maalumu ya kilimo hai ili bidhaa itoa utambulisho.
Kanuni hizo na nyengine zote za kilimo hai zinazingatia urutubishaji wa udongo, mimea, wanyama na uzalishaji wa chakula chenye ubora na usalama wa hali ya juu kwa binadamu, hivyo   ulimaji, uvunaji, uhifadhi, usafirishaji na usambazaji unahitaji uangalifu wa hali ya juu.
Pamoja na uzuri na faida wa kilimo hai, uzalishaji wake unakabiliwa na changamoto ya uzalishaji mdogo ukilinganisha na mahitaji hasa katika soko la nje.
Wakulima wengi wanakosa uwezo wa kuzalisha kwa wingi kutokana na kukosa mahitaji ya msingi katika uzalishaji wa kilimo hicho hasa mbolea isiyokuwa na kemikali.
Ni jukumu la Serikali na wadau wengine wa maendeleo kuwasaidia Wakulima wa kilimo hicho kwa kuwapatia pembejeo ili waweze kuzalisha kwa wingi kukidhi mahitaji ya soko hasa soko la nje ambapo itachangia kukuza kipato chao na Taifa.

JITIHADA ZA RAISI WA TANZANIA TUNAZIPONGEZA

19/12/2015
ADA TADEA
JITIHADA ZA RAISI WA TANZANIA TUNAZIPONGEZA
ATALETA MAENDELEO MAKUBWA YA KUICHUMI KWA WA TANZANIA KWA SABABU ANA MOYO WA DHATI KWA KUWALETEA MAENDELEO ENDELEVU YANO LENGO LA KUONDOSHA KAYA MASIKINI NA KUTUFIKISHA KATIKA UCHUMI WA KATI TUNAPOFIKA 2025 KAMA YALIVO MALENGO MAKUU YA SEREKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KWA KAULI MBIU YAKE HII YA HAPA NI KAZI TU INAASHIRIA KUA MTU NI KAZI LAKINI TAIFA LINALOFANYA KAZI KWA UFANISI HUPATA MAENDELEO MAKUBWA
NA HILI TUMELIONA KATIKA MATAIFA MINGI ULIMWENGUNI YAMEPATA NA YANAENDELEA KUPATA MAFANIKIO MAKUBWA KWA KUCHAPA KAZI NA KUONEKANA KATIKA MATAIFA HAYO KUA KAZI NI MSINGI MKUBWA WA MAENDELEO YA JAMII NA MAENDELEO YA MTU KWA MTU NA KWA KULIONA HILO NASISI TANZANIA TUTAFIKIA MALENGO YETU YA KIUCHUMI KAMA TUJALI KAZI NA TUTAFANYA KAZI KWA UFANISI TUTAKWAMUKA KIUCHUMI NA KUFIKIA UCHUMI WAKATI NA KUONDOSHA KAYA MASIKINI IFIKAPO 2025 MALENGO MAKUU HAYA YATAKUA KAMA TUTAONDOSHA UZEMBE UBADHILIFU WA MALI ZA SEREKALI SAMBAMBA NA KUONDOSHA MUHALI RUSHWA NA KUA HAPA KAZI KWA MAFANIKIO.
NA KWA UPANDE WA BARAZA LA MAWAZIRI NALO NI ZURI NA LINALETA MATUMAINI KWA HIVO HAPA NI KAZI.
TUNAMPONGEZA SANA DR MAGUFULI KWA AHADI ILIYO ISEMA IFIKAPO TAREHE 1/1/2016 KUA ELIMU ITAKUA NI BURE YAANI BILA YA MALIPO NA KASISITIZA KUA ITAKUA BURE TENA BURE KWELI KWA HILI NI FARAJA KWA WATANZANIA KWA SABABU HAKUNA MTANZANIA ILIYOKUA HAUSIANI NA ELIMU KWA NJIA MOJA AU NYENGINE NA KWA HILO IMEPUNGUZA MZIGO KWA WAZAZI NA HILI LA IFIKAPO MWAKA 2020 KUA ATAPUNGUZA AJIRA KWA ASILIMIA 40 KWA KUTUMIA VIWANDA AMBAVYO NI VIWANDA MAMA AMBAVO VITATUMIA KILIMO,  UVUVI, MIFUGO SAMBAMBA NA KUIMARISHA SERA YA VIWANDA UVUVI KILIMO MIFUGO MPAKA SASA IMEOKOA MABILIONI KWA SAFARI ZA NJE NA UDOGO WA BARAZA  LA MAWAZIRI SAMBAMBA NA TAFRIJA MBALIMBALI LAKINI ZAIDI KATIKA BANDARI UPOTEVU WA MAKONTENA KWA KUGUNDUA UFISADI MBALIMBALI KWA HIYO TUNAJUA TUTATATUA MALENGO MAKUBWA YA KUPUNGUZA UMASIKINI NA KUFIKIA UCHUMI WA KATI IFIKAPO 2025 KAMA INAVOJULIKANA KATIKA MALENGO MAKUU YA SEREKALI ZETU NA HAPO TUTAKUA TUNAJIKOMBOA NA WANANCHI KUONA FAIDA YA UHURU NA FAIDA YA KUA MTANZANIA WALEO.
KWA HIVO TUNAHITAJI UCHUMI WA KASI NA HATA KUFIKIA MALENGO KAMA DR MAGUFULI ATAUSHIRIKISHA MUHIMILI  WANNE ULIOKUA HAUKO RASMI NAO NI MUHIMILI WA HABARI TASNIA HII INAWEZA KUTUVUSHA NA KUSAIDIA SANA KATIKA KUONDOA UFISADI NA  KUSUKUMA MAENDELEO KATIKA SEKTA ZA MAENDELEO KAMA UVUVI KILIMO VIWANDA MIFUGO NA HATA KATIKA MIHIMILI MITATU YA SEREKALI KAMA TUNAVOJUA HABARI NDIO MPANGO MZIMA WA MAENDELEO MIJINI NA VIJIJININA KWA HIVO TANZANIA NI MIJI NA VIJIJINI BASI IPO HAJA SEREKALI KUUDHAMINI NA KULITUNZA KWA KUONGEZA RUZUKU NA KUUPATIA RUZUKU YA SEREKALI ITOLEWA KWA VYOMBO VYA HABARI VYA SEREKALI NA ITOLEWE KWA VYOMBO VYA HABARI VYA SEREKALI NA VYA WATU BINAFSI ILI KUKUZA HABARI NCHINI KWAA MISINGI YA KUPATA MAENDELEO YA HABARI KWA KUKUZA TAIFA ILI IFIKIE MABADILIKO YA HABARI NA MAENDELEO ENDELEVU KWA HARAKA SANA KAMA TUNAVOJUA KUNA WAANDISHI WA HABARI WA VIWANDA UCHUMI KILIMO MIFUGO UVUVI MISITU WANYAMA NA HIFADHI MBALIMBALI ZA KITAIFA KAMA UTALII KWA VILE TUKIWATUMIA WAANDISHI VIZURI TUTAINUA MAENDELEO YA KWELI KAMA TUNAVOJUA TANZANIA INA MIHIMILI MITATU MAHAKAMA, UTAWALA NA BUNGE NA MIHIMILI HII YOTE ILI IFANYE KAZI VIZURI NI LAZIMA IPATE HABARI.
NATUKISEMA HABARI NI ZILE ZA UHAKIKA ZAKINA NA ZILIZOFANYIWA KAZI VIZURI NA ZENYE MAADILI YA HABARI NA HABARI ZINAENDA NA VIFAA VYA KISASA VINAVOENDANA NA WAKATI WA HABARI ULIMWENGUNI KWA HIVO KUWEZESHA NI JAMBO ZURI KWA HIVYO KUNA NCHI NYINGI ULIMWENGUNI ZIMEPATA MAENDELEO MAKUBWA YA KISIASA NA KIUCHUMI KWA KUTUMIA MUHIMILI HUU WA HABARI NCHI KAMA SEKENDNAVIA CANTURE ZIMEPATA MAENDELEO YA KIUCHUMI MAKUBWA KWA KUPATA NGUVU MUHIMU HUU WA HABARI LAKINI HATA UNGERZA MAREKANI ZIMEKUA NCHI ZENYE UTALUME WA KIUCHUMI DUNIANI KWA KUWATUMIA WANAHABARI KWA KUKUZA UCHUMI KWA KUIBUA VITU MBALIMBALI KAMA RUSHWA, WAHUJUMU UCHUMI WALETA MADAWA YA KULEVYA NA KUSUKUMA MAENDELEO NA KUSHAWASHI MAENDELEO YA KASI KIUCHUMI NA NDO MAANA UKAAMBIWA HABARI NI MUHIMILI WANNE ULIOKUA HAUKO RASMINI NA KWA SASA TANZANIA TULIVOKUA UCHUMI WATU NA KUPUNGUZA KA YA UMASIKINI DR MAGUFULI LAZIMA UUWONE MUHIMILI HUU KWA NGUVU ZOTE ILI TUFIKIE MALENGO KWA KUHAKIKISHA KILA IDARA YA SEREKALI NA SEKTA ZAKE ZOTE ZINA TOA HABARI KWA KUA NA WATU WA HABARI NA HATA ZA WATU BINAFSI ZIWE NA MAOFISA WA HABARI KWA MSINGI WA KUPATA HABARI NA KUIBUA MAENDELEO KWA MANA TANZANIA LAZIMA IWE NA SERA YA HABARI INOENDANA NA WAKATI NA ULIMWENGU KWA HIVYO ULIMWENGU UNATAKA HABARI NA UNAENDA KWA HABARI MBALIMBALI KWA HIVO TANZANIA IKO HAJA YA KWENDA KIHABARI ILI KUPATA MAENDELEO ENDELEVU YANOENDANA NA WAKATI HABARI NDIO MPANGO MZIMA KWA MAENDELEO YA DUNIA AFRICA NA TANZANIA KWA UJUMLA
AHSANTE
TUNAZIPONGEZA JITIHADA ZA RAISI WA AWAMU YA TANO DK JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUFUFUA MAENDELEO YAWATANZANIA

CHAMA CHA TADEA
RASHID YUSSUF MCHENGA
MWANASIASA MKONGWE/MWANAHARAKATI
NA KATIBU MWENEZI TAIFA TADEA

0733560243 % O715560243

CCM YAJIANDAA NA UCHAGUZI WA MAREJEO

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.

   
CHAMA Cha Mapinduzi Zanzibar kimewataka wanachama wake kuepuka kupeba fikra na  propaganda potofu za wapinzani na badala yake wajiandae ipasavyo kuendelea kuunga mkono CCM ili iweze kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa marudio utakapowadia.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, wakati akizungumza na Wanachama wa chama hicho  wa Tawi la Mbuyu Tende, Jimbo la Kijini, Wilaya ya Kaskazini ‘A’, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Amesema  sula la kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu uliofutwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) halina mjadala wala mbadala, hivyo wanachama wa chama hicho hawanabudi kuendelea kuhamasisha na kujiandaa kikamilifu kupiga kura kwa lengo la kuhakikisha chama hicho kinashinda  katika Uchaguzi mkuu huo.

Vuai ameeleza  kwamba msimamo wa CCM katika suala la kwamo wa kisiasa uliopo hivi sasa Zanzibar ni kurudiwa uchaguzi na siyo vinginevyo, hivyo wanachama na wananchi kwa ujumla wanatakiwa kuendelea kuwa wavulivu huku wakisubiri uamuzi halali wa tume ya uchaguzi Zanzibar.

 Amesema   hata kama uchaguzi unarejewa suala la maandalizi na utayari kwa kila mfuasi wa chama hicho ni lazima liwepo kwani ushindi wa kisiasa haupatikani kwa maneno matupu bila ya vitendo.

Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo  ametumia nafasi hiyo,  kuwakabidhi hati Vikundi Saba (7) vya Ushirika vya Akinamama ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ya kuwapatia hati za usajili wanaushirika hao.

Vikundi hivyo vilivyopatiwa hati za usajili ni pamoja na Nyota Njema, Atoae Allah (Mola) na  Tumia Jasho lako. Vyengine ni Penye Riziki Hapakosi Fitina, Riziki ya Makunge, Tujipatie Kitu na Heri Liwe.

Hata hivyo,  Vuai amewapongeza  wanaushaurika hao kwa kuunda vikundi vya ujasiriamali kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kuwataka kujenga  moyo wa kuaminiana na kuvumiliana miongoni mwao.

Thursday, December 17, 2015

UNION RANGER KAZINI





MAMBO 10 AMBAYO MKE MWEMA HAFANYI

NA KABUGA KANYEGERI

MAMBO 10 AMBAYO MKE MWEMA HAFANYI
Ni matumaini yangu kuwa ulisoma mada iliyopita juu ya “dondoo 10 zinazochangamsha ukaribu wenu wa kimapenzi”, na ni imani yangu kuwa imesaidia katika kuboresha ndoa yako.
Kama ni hivyo basi, leo tena ninakuletea kitu kizuri chenye manufaa katika kuboresha ndoa yako na kuifanya kuwa maridhawa.
Kama wataka kuwa na ndoa yenye furaha jiweke mbali na tabia hizi mbaya ambazo zitakufanya uwe mke mwenye kuogofya sana.
Hapa nimekuwekea orodha ya mambo 10 mabaya ambayo unaweza ukawa unamfanyia mumeo na yakawa hayana msaada wowote kwenye ndoa yako:
1. Usumbufu
Amini usiamini, mumeo ni mtu mzuri na maridadi sana. Nakwambia kweli, ni mtu maridhawa. Mara nyingi anasikiliza unachosema, anaelewa kinachotakiwa kufanyika, na mara nyingi anakuwa na nia ya dhati ya kufuata hicho unachokitaka. Lakini, atakifanya kwa muda wake na kwa njia anayoiona yeye, na hata ufanye usumbufu kwa kiwango gani huwezi kuibadilisha hiyo. Usumbufu utazidisha mvutano.
2. Kulalamika
Maisha yenu yanaweza yasiwe mazuri sana, lakini kulalamika kuhusu maisha hayo hakuwezi kuyafanya yawe mazuri. Naam, ni muhimu umshirikishe mumeo vitu ambavyo unahisi kama vinakuudhi, ambavyo vinakutibua na kukuchanganya au kukuhuzunisha. Lakini, hakikisha kuwa mambo hayo hayawi mambo pekee unayomwambia. Malalamiko endelevu na mtazamao hasi unaweza kutawala na kutamalaki uhusiano wenu. Hivyo, jaribu kuwa na mtazamo chanya na kufanya vitu chanya.
3. Udhalilishaji au Umbea
Bila shaka wewe na marafiki zako mnapenda kukaa pamoja na kuzungumzia kila kitu kinachopatikana chini ya jua. Lakini, wakati mwingine mazungumzo yenu hayo huenda mbali sana. Marafiki zako wanaweza wakataka kujua kila kitu kuhusu maisha yako binafsi, lakini hilo si jambo zuri. Usimfanyie hila mumeo mbele ya marafiki zako, hata kama wao wanawafanyia hila waume zao. Usijaribu kumkosoa mbele ya watu. Kama kuna mambo yanatakiwa kushughulikiwa, basi tafuta muda mzuri mnapoweza kuzungumza na kuyashughulikia kwa pamoja – wewe na mumeo tu.
4. Kukosa heshima
Waume wengi sio wakamilifu, na wengi wao wanalijua hilo. Licha ya mapungufu yao, inaonekana kuwa wanaume wengi hukubali kurekebishwa pindi urekebishaji na ukosoaji huo unapofanyika katika njia ya upendo na yenye nia ya kujenga – wanachotaka wao ni kuona kuwa wanaheshimiwa wakati wa kuwarekebisha. Kuna namna nyingi unaweza ukawa unamvunjia heshima na adabu mumeo kwa kujua au kwa kutojua. Miongoni mwa njia hizo ni pamoja na kuendelea kumkatisha anapokuwa akizungumza, kutomshauri katika kufanya maamuzi muhimu, au kubadilisha maamuzi yake.
5. Kuwapa kipaumbele watu wengine
Ninafahamu kuwa labda umetingwa na kazi. Unaweza ukawa na majukumu ya kazi, watoto, na mazungumzo na marafiki zako. Kila mtu anaweza kuona kuwa wewe ni mwanamke mchapazi – isipokuwa mume wako. Anaweza kuhisi kuwa amepuuzwa. Tafadhali usimsahau kwa kuwaweka watu wengine au vitu vingine mbele yake. Anahitaji kujua kwamba yeye ndio kipaumbele chako namba moja.
6. Kumnyima jimai
Tendo la ndoa halipaswi kuwa kama kitu cha kubembelezea. Kufanya hivyo kunalifanya tendo hilo kuwa kitu kisichokuwa na thamani. Linapaswa kuwa nyenzo ya kuwaunganisha na kuwaweka karibu zaidi. Usilitumie kama nyenzo ya kumdhibiti mume. Tendo la ndoa ni ndoa yako. Mahitaji yako ya tendo la ndoa yanaweza kutofautiana na mahitaji yake, lakini hiyo haina maana ulichukulie kama peremende unayompa mwanao kwa kuwa mtoto mwema. Kama kuna kitu kinakuzuia kumpatia haki hiyo, basi jadiliana naye kuhusu tatizo hilo na mtafute suluhisho kwa pamoja.
7. Matumizi ya pesa kupita kiwango
Ninatambua kuwa hali za kiuchumi za wanandoa zinatofautiana, lakini ni ukweli kwamba masuala ya pesa yamekuwa chanzo cha migogoro ya ndoa nyingi na hata talaka nyingi. Iwapo wewe na mumeo hamtaafikiana katika masuala ya kifedha na kiuchumi, migogoro na mivutano inaweza ikazidi na hata kushindwa kuidhibiti.
8. Kuwa kama Mama yake
Mume wako ni mtu mzima, ingawa anaweza asionekane hivyo, na hajakuoa uwe mama yake wa pili. Sasa usijiweke katika nafasi ya mama yake. Badala yake, jitahidi uwe rafiki yake mpenzi na mtu ambaye anaweza akamuamini na kumpa siri zake. Pambana na tabia ya kukumuendesha, kumkaripia kwa kila analofanya au kumuamulia mambo yake. Ukimuacha azungumze na kukushirikisha mambo yake kwa njia anayoiona yeye ni bora kuliko kujaribu kumpeleleza au kudukiza taarifa zake.
9. Kuwa na matarajio yasiyokuwa na uhalisia
Mumeo anakupenda sana. Anataka kufanikisha mambo mazuri ambayo hata yumkini usingeyatarajia. Lakini, wakati fulani matarajio yanaweza kuwa makubwa na yasiweze kufikiwa. Anaweza kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya maajabu, lakini hata mtu wa aina hiyo uwezo wake una kikomo. Sikwambii kwamba ushushe kiwango cha hayo matarajio yako, lakini kumbuka tu kwamba baadhi ya vitu huchukua muda kukamilika, na huna sababu ya kuchanganyikiwa unapoona kuwa maendeleo yenu yanaenda taratibu. Waume wengi huona kuwa presha wanaoipata kutoka kwa waajiri, majirani au wakwe ni bora kuliko presha hiyo itoke kwa wake zao.
10. Kuchukua nafasi yake
Wanaume wanayapenda majukumu yao yanayowahusu. Huwafanya wajihisi kuwa wana nguvu. Jaribu kufikiria mumeo atakavyojisikia utakapotwaa mamlaka na madara yake. Anaweza kuhisi kuwa anapingwa na kuwa mwenye mtazamo wa kujilinda. Pamoja na mgawanyo wa majukumu katika ndoa yenu, muache mumeo awe mume, awe baba, kiongozi wa familia na kutekeleza majukumu yake. Usinyakue mamlaka yake. Anapotekeleza kazi yake vizuri mpongeze na umshukuru pia.
Ninatambua kuwa ndoa ina mambo mengi sana. Lakini ukiachana na tabia hizi mbaya na badala yake ukawa na matendo mazuri, unaweza kufurahia raha isiyokuwa na kikomo kutokana na ndoa yako kuwa maridhawa.
Ni matumaini yangu kuwa somo hili litakuwa na faida kwako itakayoongeza furaha tele!
Ungana nami katika mada ijayo…
NDOA MARIDHAWA GROUP..
WhatsApp: +255 763 348 213

Sunday, December 13, 2015

WALIMU NCHINI WATAKIWA KUWAHAMASISHA WANAFUNZI

WAALIMU NCHINI WAMETAKIWA KUWAPA FURSA NA KUWAHAMASISHA WANAFUNZI WA SKULI MBALIMBALI  KUSHIRIKI KATIKA MICHEZO  ILI KUWEZESHA  KUPATA TIMU NZURI NA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA.
HAYO YAMEELEZWA NA MKURUGENZI WA IDARA YA MAENDELEO YA MICHEZO WIZARA YA HABARI UTAMADUNI WASANII NA MICHEZO TANZANIA LEONA TADEO  KATIKA  UWANJA WA AMANI NJE WAKATI ALIPOKUA AKIFUNGA SHAMRASHAMRA ZA  TAMASHA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
AMESEMA KATIKA NCHI YA TANZANIA WANANCHI WENGI HULALAMIKA  KWA KUTOFANYA VIZURI KATIKA MICHEZO  KUTOKANA NA  WAALIMU KUSAHAU  WAJIBU WAO WA KUWAJENGA WANAFUNZI WAO KIMICHEZO TANGU WADOGO WAKATI WAPO MASKULINI JAMBO AMBALO LINAREJESHA NYUMA  MAENDELEO YA MICHEZO HIYO.
AIDHA AMEFAHAMISHA KUWA IWAPO JAMII ITASHIRIKI KATIKA MICHEZO MBALIMBALI  ITAWEZA KUJIEPUSHA NA MARADHI SAMBAMBA NA KUJENGA AFYA HIVYO ZOEZI HILO LIWE ENDELEVU KWANI KUFANYA HIVYO KUTASAIDIA WALIMU KUWA IMARA KIMICHEZO.
HATA HIVYO MKURUGENZI HUYO AMEWATAKA WAALIMU KUTOA FURSA  KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA HUUSIKA KWENDA KUSOMA KATIKA CHUO CHA MAENDELEO YA MICHEZO TANZANIA BARA ILIKUONGEZA UWEZO NA IDADI YA WAALIMU WA MICHZO.

KWA UPANDE WAKE MWALIMU MUSSA  ABDULRABI  KUTOKA WIZARA YA ELIMU AMESEMA LENGO LA KUFANYA TAMASHA HILO NI KUWAFANYA WALIMU KUSHIRIKI MICHEZO MBALIMBALI NA KUONESHA VIPAJI VYAO  KATIKA MICHEZO HIYO.
AMESEMA KATIAKA MWAKA HUU HAKUNA CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA HIVYO  WANAJIANDAA KWA AJILI YA MWAKANI ILI WAWE NA UWEZO WA KUFANYA VIZURI ZAIDI  KATIKA TAMASHA LIJALO .
SAMBAMBA NA HAYO MWALIMU HUYO AMEAAHIDI KUWA WATAWASHAJIISHA WALIMU WENZAO KWENDA KUJIUNGA NA CHUO CHA MAENDELEO   YA MICHEZO ILI  KUPATA WALIMU WENGI  KWA AJILI YA MICHEZO KWANI SEREKALI INA NIA YA KUENDELEZA MICHEZO .
WAKIELEZEA FURAHA ZAO WASHINDI KATIKA TAMASHA HILO WAMEIOMBA WIZARA KUANGALIA SUALA LA MICHEZO ZAIDI KWA KUANDALIWA MAFUNZO MAALUM ILI KUWEZA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO  MBALIMBALI.
KATIKA SHAMRASHAMRA HIZO KUMEFANYIKA MICHEZO MBALI MBALI IKIWEMO KUVUTA KAMBA, MPIRA WA MKONO,MBIO ZA GUNIA PAMOJA NA MPIRA WA MIGUU  KUTOKA KATIKA MIKOA MITATU YA ZANZIBAR IKIWEMO MKOA KUSINI UNGUJA , KASKAZINI UNGUJA NA MKOA WA MJINI MAGHARIB AMBAPO MKOA WA KASKAZINI NA MJINI NDIO WALIOIBUKA WASHINDI IKIFUATIWA NA MKOA WA KUSINI UNGUJA.

                                                           MWISHO