Rais Yahya Jammeh wa Gambia ameitangaza nchi hiyo ya
Kiafrika kuwa Jamhuri ya Kiislamu.
Akitangaza hatua hiyo, Rais Jammeh amesema kuwa, kuanzia
sasa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu unatawala nchini humo ikiwa ni katika juhudi
za kutoa utambulisho kwa thamani za kidini.
Rais Yahya Jammeh amesema kuwa, kwa kuwa raia waliowengi wa
nchi hiyo ni Waislamu, Gambia haiwezi kuendelea kuvumilia turathi za kikoloni.
Rais wa Gambia amesisitiza kuwa, wafuasi wa dini nyingine
nchini humo hawatabughudhiwa na wanaweza kuishi kulingana na mafundisho ya dini
zao.
Rais Jammeh ambaye mwaka 2013 alitangaza kujitoa nchi hiyo
katika Jumuiya ya Madola, Commonwealth na kuitaja kuwa ni ukoloni mamboleo,
anataraji nchi za Kiarabu zitaisaidia nchi yake ili iweze kuziba pengo la
misaada iliyokatwa na itakayokatwa ya madola ya Magharibi. Machi mwaka huu
serikali ya Gambia ilibadilisha lugha yake rasmi ya Kiingereza na kuifanya kuwa
Kiarabu.
Gambia ina wakazi milioni moja na laki nane huku asilimia 95
wakiwa ni Waislamu. Gambia ilikoloniwa na Uingereza hadi mwaka 1965 ilipopata
uhuru.
Nchi hiyo inategemea zaidi kilimo na utalii kama sekta kuu
na uti wa mgongo wa uchumi wake.
No comments:
Post a Comment