Kassim Iman
Mohammed ni mtoto wa miaka 14 anaeishi chini ya uangalizi wa wazee wake wote
wawili, baba na mama.Anaishi kijiji cha Mbuguani, katika Shehia ya Mbuguani,
Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba.Kassim ni mtoto watano kwa kuzaliwa
katika familia yenye watoto nane.
Chanzo cha
matatizo ya Kassim yalijitokeza usiku wa manane baada ya yeye kuamka kwa lengo
la kwenda kujisaidia akahisi maumivu makali kwenye misuli ya miguu yote miwili
ambapo alishindwa kusimama na kumwamsha mama yake mdogo ambaye akiishi naye kwa
kumpatia msaada.
Historia ya
matatizo ya Kassim yalianza pole pole pale ishara na dalili za maumivu endelevu
kuonekana kila alipokuwa akitembea
masafa ama kufanya mazoezi na wenzake. Misuli yake ilikuwa ikimuuma kwa sana na
kuonyesha kuvimba kwa kiasi.
Kwa upande
wa matibabu baada ya kuonekana tatizo la maumivu na kuvimba misuli linaendelea,
wazazi wake walimpeleka Hospitali ya Abdalla Mzee ya Mkoani Pemba ambapo alipewa
rufaa ya kwenda Hospitali nyengine
ambapo walimpeleka Hospitali ya Temeke –Dar es salam. Nayo Hospitali ya Temeke ilimpa rufaa ya kumrejesha
Hospitali Kuu ya Taifa ya Mnazi Mmoja –Zanzibar.
Aidha
ushauri uliotolewa Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa kijana huyo ni kufanya zoezi
kwa bidii ili aondokane na kadhia hiyo. Aliendelea vizuri kwa muda wa mwaka
mmoja hapo hapo Unguja lakini hatima yake ikaishia kuganda na kuvimba misuli
kwa ghafla.
Kwa upande
wa elimu, Kassim ni mwanafunzi wa darasa la 5 katika Skuli ya Msingi ya
Matetema katika kijiji cha Kazole huko Unguja. Aidha Kassim alichukuliwa
uhamisho wa kimasomo toka Skuli ya Msingi Ng’ombeni B- Mkoani Pemba.
Hali ya sasa
ya Kassim ni mbaya sana na inasikitisha kabisa kwani misuli ya miguu yake
imevimba na yenye kumpa maumivu makali unapojaribu kumsimamisha na anaonekana
kudhoofika kiafya kadri siku zikisonga mbele. Amekuwa mlemavu tayari, ni kweli
sote ni walemavu watarajiwa kwani mtoto Kassim alikuwa yuko makini na mwenye
afia nzuri miezi minne iliyopita. Allah ampe wepesi ili aweze kushiriki katika
maendeleo ya Taifa letu, AMIN.
No comments:
Post a Comment