MKURUGENZI MWENDESHAJI WA SHIRIKA LA BIASHARA LA TAIFA
ZANZIBAR (ZSTC) BI. MWANAHIJA ALMAS ALI AMEKANUSHA UZUSHI UNAODAI KUWA SHIRIKA
LA ZSTC LIMEISHIWA FEDHA ZA KUNUNULIA KARAFUU NA KUWAKOPA WAKULIMA KARAFUU ZAO.
AKIZUNGUMZA NA WANDISHI WA HABARI MAKAO MAKUU YA SHIRIKA MAISARA
ZANZIBAR, BI. MWANAHIJA AMESEMA PAMOJA NA KUONGEZEKA KWA MANUNUZI YANAYOTOKANA
NA KUONGEZEKA KWA UZALISHAJI KATIKA MSIMU WA 2015/2016 SHIRIKA LINAPESA ZA
KUTOSHA ZA KUNUNULIA KARAFUU ZOTE KATIKA MSIMU MZIMA NA HAKUNA MKULIMA YOYOTE ALIYEKOPWA.
AMESEMA SHIRIKA TANGU KUANZISHWA KWAKE MWAKA 1968 HALIJAWAHI
KUWAKOPA WAKULIMA NA AMESEMA KUWA MADAI HAYO NI UZUSHI USIOKUWA NA UKWELI
WOWOTE.
AMESEMA ZSTC NI SHIRIKA LA SERIKALI HIVYO KAMA LIKIPUNGUKIWA
NA FEDHA ZA MANUNUZI YA KARAFUU SERIKALI INA UWEZO WA KULIPA FEDHA ZA KUTOSHA
ZINAZIHITAJIKA NA SIO KUWAKOPA WAKULIMA.
AIDHA AMESEMA HAKUNA MKULIMA ALIYEKOPWA NA WALA HAKUNA SHIDA
YA KUKOPA KUTOKA TAASISI ZA KIFEDHA KWA VILE SHIRIKA LIMESHAJIPANGA VIZURI
KUNUNUA KARAFUU ZOTE KUTOKA KWA WAKULIMA KWA FEDHA TASLIMU.
HATA AMEWATAKA WAKULIMA WA ZAO LA KARAFUU KUTOKUWA NA WASI
WASI WOWOTE JUU YA MANUNUZI YA KARAFUU ZAO NA AMEWATAKA KUENDELEA KUSHIRIKIANA
NA SHIRIKA KATIKA KULIHUDUMIA ZAO VIZURI.
BI. MWANAHIJA AMEFAHAMISHA KUWA MANUNUZI YAMEONGEZEKA MWAKA
HUU WA 2015/2016 KINYUME NA ILIVYOKADIRIWA AWALI KUTOKANA NA HALI YA HEWA
KUBADILISHA MSIMU WA MWAKA KUWA MSIMU WA VULI AMBAO HUWA NI MSIMU MKUBWA.
SABABU NYENGINE ALIZOZITAJA KUWA NI UZAZI WA MIKARAFUU MIDOGO
ILIYOPANDWA KATI YA MWAKA 2005 HADI 2013 AMBAPO MIKARAFUU HIYO TAYARI IMEANZA
KUZAA VIZURI NA KUONGEZA UZALISHAJI.
SAMBAMBA NA HAYO PIA AMESEMA KUANZISHWA KWA MFUKO WA
MAENDELEO YA KARAFUU IMEKUWA NI HATUA NYENGINE MUHIMU YA KUONGEZEKA KWA
UZALISHAJI WA ZAO LA KARAFUU KUTOKANA NA KAZI NZURI ZINAZOFANYWA NA MFUKO HUO
ZA KUSHAJIHISHA WAKULIMA KUIMARISHA ZAO HIO.
No comments:
Post a Comment