tangazo

tangazo

Friday, December 11, 2015

Mkutano  mkuu wa mwaka wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania .

 Mwenyekiti wa Kamisheni ya wachezaji Tanzania (KAWATA) Ramadhan Zimbwe akizungumza na Wanamichezo  mbalimbali waliohudhuria katika Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa kituo cha Utengamano Welezo Mjini Zanzibar.
 Katibu Mkuu wa TOC Filbert Bayi akizungumza na wana Michezo  mbalimbali waliohudhuria katika Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa kituo cha Utengamano Welezo Mjini Zanzibar.
 Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka waliohudhuria katika Mkutano huo wakisikiliza maelezo  kwa Mgeni Rasmi Katibu Mkuu msaidizi Jamali Nassor Adi hayupo pichani.
 geni Rasmi Jamal Nassor Adi akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa kamisheni ya Wachezaji Tanzania (KAWATA) katika Ukumbi wa Kituo cha Utengamano Welezo Mjini Zanzibar.
Wajumbe wakiwa katika picha ya Pamoja.

Na Rahma Khamis /Miza Othman -Maelezo Zanzibar.

Kamati ya Olimpiki Tanzania  (TOC)  wamewataka Viongozi  wa Mashirika ya  Vyama  vya Michezo  Tanzania  kusaidiana na wanamichezo mbalimbali ili kufikia hadhi ya kimataifa .
Hayo yameelezwa na na Katibu mtendaji wa TOC Jamal  Nassor Adi  huko Kituo cha Utengamano Welezo  Zanzibar  wakati alipokua akifungua  Mkutano  mkuu wa mwaka wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania .
Amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuhamasisha na kuamsha ari kwa Wachezaji ili kuweza kurejesha hadhi ya Michezo  Tanzania.
 Katibu Jamal amefahamisha kuwa wachezaji  ndio wahusika wakuu  wa michezo hivyo ni lazima kushirikishwa na kupatiwa elimu ili kuweza kufahamu  wajibu wao katika michezo   na kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.
Akizungumzia suala la dawa za kuongeza nguvu kwa wanamichezo,  Katibu Jamal amesema  ni vyema wachezaji kuzifahamu na kujiepusha nazo kwani kitendo hicho kinaweza kupelekea nchi kupigwa marufuku kushiriki michezo ya Kimataifa.
Nae Katibu wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania Filbert Bayi  amesema kuwa michezo ni chanzo cha kujipatia  ajira  kwa vijana  hivyo ni vyema michezo  iendelezwe ili kuleta maendeleo kwa wachezaji wenyewe  na Taifa kwa ujumla.
Aidha  amesema katika kuimarisha michezo Nchini   suala la   kuteuliwa wawakilishi  wenye uwezo   ni jambo muhimu  na amewashauri washiriki wa mkutano  huo kusaidia ili kupunguza malalamiko.
Mwenyekiti wa  Kamsheni ya  Wachezaji Tanzania (KAWATA)   Ramadhani Zimbwe ameahidi kupambana na rushwa kwa viongozi na watendaji  wa michezo nchini kwani  vitendo hivyo vinarudisha nyuma  ufanisi wa michezo.
Amesema rushwa ni adui wa haki na mara nyingi hupelekea mtu mwenye uwezo wa kifedha kupata haki asiyostahiki na kumuacha mwenye haki hiyo kuikosa kutokana na kukosa fedha.

No comments:

Post a Comment