Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Utalii na Michezo Issa Mlingoti akifungua Mkutano wa Mfuko wa usimamizi wa Magofu Duniani kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ali Mwinyikai. Mkutano huo ulijadili mambo mbalimbali juu ya uhifadhi wa mambo ya kale pamoja na kutembelea na kuzungumzia namna ya kuyafanyia matengenezo majumba yaliyo chakaa ili yasitoweke katika Mji Mkongwe wa Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Makumbusho na mambo ya kale Zanzibar Dkt. Amina Issa akionesha Picha ya Uchakavu wa Jengo wakati alipokuwa akitoa Mada katika Mkutano wa wadau wa kutembelea na kuzungumzia namna ya kuyafanyia matengenezo majumba mabovu ili yasitoweke katika Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Stephen Battle kutoka Mfuko wa Kimataifa wa kuyaendeleza majengo ya Miji Mikongwe Duniani na kuyatunza {World Monument Fund} akitoa mada katika Mkutano wa Mkutano wa kutembelea na kuzungumzia namna ya kuyafanyia matengenezo majumba mabovu ili yasitoweke katika Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Mkutano wa kutembelea na kuzungumzia namna ya kuyafanyia matengenezo majumba mabovu ili yasitoweke katika Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Na Ali Issa Maelezo- Zanzibar
Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutunza na kulinda Utamaduni wa Zanzibar na kuyafanyia matengenezo majengo ya Mji Mkongwe yaliyochoka kwa ushirikiano wa Mfuko wa Kimataifa wa kuyaendeleza majengo ya Miji Mikongwe Duniani na kuyatunza {World Monument Fund}.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Utali na Michezo Issa Mlingoti wakati akifungua mkutano kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo wa kutembelea na kuzungumzia namna ya kuyafanyia matengenezo majumba mabovu ili yasitoweke katika Mji huo.
Amese matengenezo hayo hufanywa kwa mashirikiano ya pamoja kati ya Serikali, wahisani na Mashirika mbalimbali ya Kimataifa.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar Issa Makarani amesema hivi sasa kuna majengo yapo hatarini kupotea katika urithi wa Kimataifa kutokana na kuchakaa na kufikia hatua ya kuanguka hivyo kutokea mfuko huo kusaidia ni jambo la faraja.
Aidha alisema wananchi kwa upande wao wanalazimika kufuata kanuni na taratibu za kuuhifadhi na kuulinda Mji Mkongwe wa Zanzibar ikiwamo kuacha kupitisha magari makubwa ambayo hupelekea kupasuka kwa majengo.
“Kuazia mwakani kutakua na sheria maalumu ya kupitisha vyombo vya moto katika maeneo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar ambayo madereva watalazimika kuifuata,” alisema Makarani.
Nae Meneja wa Mfuko wa Kimataifa wa kuyaendeleza majengo ya Miji Mikongwe Duniani na kuyatunza kwa nchi za Jangwa la Sahara Stephen Battle amesema taasisi hiyo imekuwa ikifanya matengenezo majengo ya miji yenye urithi wa Kimataifa ikiwemo Kanisa la Mkunazini liliopo Mji mkongwe wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment