ZANZIBAR
GENERATOR
LINALOTUMIKA KATIKA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA LIMENUSURIKA
KUUNGUA KUTOKANA NA KUFANYA KAZI
KWA MUDA MREFU TOKA JANA BAADA YA
SHIRIKA LA UMEME ZANZIBAR KUKATA
UMEME KATIKA BAADHI YA MAENEO YA KISIWA CHA ZANZIBAR.
HALI HIYO ILIZUA TAARUKI KWA WAGONJWA NA WAFANYAKAZI WA
HOSPITALI HIYO BAADA YA KUTOKEA KWA MOSHI
KATIKA GENERATOR HILO
ULIOZAGAA KATIKA MAENEO
MBALIMBALI YA HOSPITALI HIYO.
FUNDI WA GENERATOR HILO AMBARE HAKUTAKA JINA LAKE LIANDIKWE
KATIKA VYOMBO VYA HABARI AMESESEMA KUWA
KUFANYA KAZI MUDA MREFU BILA YA
KUPUMZISHWA NDIYO SABABU YA KUTOKEA
KWA MOSHI HUO KUTOKANA NA KUWEPO
KWA JENERATOR MOJA KATIKA HOSPITALI
HIYO.
HATA HIVYO MAFUNDI WALIOKUWEPO KATIKA HOSPITALI HIYO WALILIZIMA
GENERATOR HILO BILA YA KUTOKEA ATHARI
YEYOTE KWA WAGONJWA WALA WAHUDUMU WA
AFYA WA HOSPITALI HIYO.
KUTOKANA NA HALI HIYO NI
VYEMA SERIKALI KUANGALIA
GENERATOR HILO IKIWEZEKANA
KUONGEZA GENERATOR LINGINE ILI KUNUSURU
MAISHA YA WAGONJWA WANAOPATIWA HUDUMA
KATIKA HOSPITALI HIYO.
No comments:
Post a Comment