Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu Fak akifunga mafunzo ya walimu wa michezo wa Skuli katika Skuli ya Elimu Mbadala Rahaaleo Mjini Zanzibar.
washiriki wakiangalia kwa makini vyeti vyao
Na Rahma Khamis Maelezo
Zanzibar
Idara ya ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imeshauriwa
kuwaandalia michezo nje ya nchi walimu wa michezo wa skuli kwa lengo la
kujipatia taaluma zaidi na kukukuza mechezo nchini .
Hayo yameelezwa huko Rahaleo katika Ukumbi wa Elimu Mbadala
na Watu wazima na Mkurugenzi Idaraya hiyo Zanzibar Mashavu Faki wakati
akifunga mafunzo yalioandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)
yaliyofunguliwa tarehe 1 mwezi huu.
Amesema iwapo walimu wa michezo watapatiwa mafunzo zaidi nje
ya nchi wataweza kuwasomesha wanafunzi wao wa skuli na kuinua sekta ya
michezo Zanzibar.
Mkurugenzi Mashavu amesema katika mwaka 2013 kulifanywa
utafiti wa kimchezo na kuonekana kuwa nchi zinazoimarisha michezo maskulini
ndizo zinazofanya vizuri zaidi katika masomo yao.
Aidha amesema michezo huimarisha afya, kujenga upendo,
udugu na uzalendo katika jamii hivyo hakuna budi kuendelezwa kwa manufaa
ya wanamichezo wenyewe na Taifa kwa jumla.
Sambmba na hayo Mkurugenzi huyo amewashauri waalimu
waliopata mafunzo hayo kwa kushirikiana na Idara husika kuandaa mafunzo
kila baada ya miezi mitatu.
Nae mkufunzi wa mafunzo hayo Suleiman Mahamoud Jabir
amewataka washiriki wa mafunzo hayo kujenga moyo wa kujitolea kwani katika
kufundisha mara nyingi hujitokeza matatizo mengi.
Kwa upande wao waalimu waliopata mafuzo hayo Mussa Abdulrab
na Arafa Talib Omar wamesema wamejifunza mambo mengi wasioyajua na
kuahidi kuwa watayafanyia kazi.
Mafunzo hayo ya siku tano ya walimu wa michezo wa skuli
mbali mbali za Zanzibar yameandaliwa na Kamati Tanzania.
No comments:
Post a Comment