Zanzibar 7.12.2015
RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Ndugu Abeid Juma Ali, kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Micheweni Pemba.
Wakati huo huo, Dk. Shein amemuapisha ndugu Ali Khamis Juma, kuwa Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar
na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria katika hafla hiyo ni Dk. Mwinyihaji
Makame Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora, Waziri wa Fedha
Mhe. Omar Yussuf Mzee, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara
Maalum Mhe. Haji Omar Kheir, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassn Said .
Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis
Haji, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Meya wa Manispaa ya Mji
wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib,Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi
wengine wa Serikali.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
No comments:
Post a Comment