tangazo

tangazo

Monday, December 7, 2015

ABDI KASSIM “BABI” ASEMA HAJAUMIA KUACHWA STARS NA HEROES, NA YUPO TAYARI HATA KUREJEA LIGI KUU BARA KAMA MASLAHI YATAKUWA POA



Na: Abubakar Kisandu, Zanzibar.

Kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar,  Yanga, na Azam  Abdi Kassim ‘Babi’ ambae kwasasa anaitumikia timu ya Ligi Kuu Malaysia, University Technology Mara FC (UiTM) amepiga stori na Mtandao huu.

 Babi kwasasa yupo nyumbani kwao Visiwani Zanzibar kaja mapumziko baada ya ligi kuu ya Malaysia kumalizika na yeye kurudi nyumbani kupumzika.

Mtandao huu umefanikiwa kupiga stori na mchezaji huyo  akizungumzia mengi tu kuhusu kuwepo likizo kwa miezi 2 hapa zenj lakini pia huwenda akajiunga na timu nyengine na akaicha UiTM  ya Malaysia ambapo ambapo kashaanza mazungumzo na timu nyengine za ligi kuu ya Indonesia ambapo pia amesema hata ikija timu ya ligi kuu Tanzania bara kama ina maslahi atakwenda, mbali na hayo Babi pia kagusia kuachwa Taifa Stars na Zanzibar  Heroes huku akisisitiza kuwa yeye hajaumia sana lililoumia ni taifa la Tanzania baada ya kumuwacha yeye mtu muhimu.

 “ Kwasasa nipo mapumziko hapa Zanzibar kwa miezi miwili na jioni huwa nakwenda kuangalia ligi kuu soka ya Zanzibar”.

Kwa upande mwengine Babi amesema kuna timu za Indonesia zinamuhitaji lakini bado mapema mno kulizungumzia suala hilo.

“ Sijui kama ntarudi tena timu yangu ya huko Malaysia mana kuna timu nyengine za ligi kuu ya Indonesia kama mbili, tatu hivi zinanihitaji , nasubiri simu tu wanipigie muda ukifika mana kule ligi yao inaanza mwezi wa pili katikati , lakini kwa ufupi Kisandu usiniulize sana muda wake bado kwasasa” Alisema Babi.

Kuhusu kucheza tena kwenye ligi kuu soka ya Tanzania bara Babi amesema yeye anaangalia maslahi hata timu itoke ligi yoyote.

“ Mimi siangaliii jina la timu naagalia maslahi tu popote tu ntakwenda , mfano nilikuwa Vietnam mwaka 2011 lakini mwaka 2012 nilikuja kucheza Azam na niliangalia maslahi tu sijaangalia timu, kwaiyo mimi timu yoyote nacheza kama ina maslahi na mimi”.



Katika  Ligi Kuu Malaysia timu ya Abdi Kassim “Babi” ya University Technology Mara FC (UiTM) imemaliza kwenye nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi yao ambapo ilishindwa kupata nafasi 6 bora na kukosa kucheza kombe la Malaysia CUP ambapo huwa na mvuto mkubwa nchini humo .

No comments:

Post a Comment