PEMBA.
KLABU ya Waandishi wa habari kisiwani Pemba, Pemba Press
Club imelaani vikali kitendo cha kuchomwa moto kwa kituo cha Radio cha Hist FM
kilichopo Migombani Mjini Unguja hivi karibuni.
PPC imesema wanahabari wa Pemba, hawafurahishwi na vitendo
vyovyote vya kuhujumu au vinavyokwaza uhuru wa habari, kwa namna yoyote ile,
kwani haki ya habari ni miongoni mwa haki muhimu zinatambuliwa na katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
kauli hiyo imetolewa na katibu wa klabu ya waandishi wa
habari Pemba, Khatib Juma Mjaja wakati alipokuwa akisoma risala ya PPC, kwa
mgeni rasmi katika mafunzo ya siku nne juu ya uwandishi wa makala, huko katika
ukumbi wa Tume ya Ukimwi Chake Chake Pemba.
Alisema kitendo hicho kimelenga sio tu kuviza demokrasia ya
habari kwa jamii, lakini pia kinakwenda kinyume na katiba zote mbili ya
Zanzibar na jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Aidha alisema wafanyakazi wa kituo hicho ni watu wenye
familia zinazowategemea katika maisha yao ya kila siku, kutokana na tatizo la
ajira linalokabili jamii, kuchomwa moto kituo hicho kinasababisha kuongezeka
kmwa ukali wa maisha kwa wafanyakazi.
Hata hivyo PPC imeziomba taasisi zinazohusika kulifanyia
kazi suala hilo na sheria kuchukuwa mkono wake kwa wale wote watakaobainika
mkuhusika na kitendo hicho dhalimu.
Nao baadhi ya waandishi wa habari kisiwani Pemba,
walisikitishwa sana na tukio hilo na kudai kuwa tasnia ya habari sasa imeanza
kupotea.
Ali Khatib Chwaya mwandishi Mkongwe alilitaka jeshi la
Polisi Kuhakikisha inawachukulia hatua kali wote waliohusika na kitendo hicho
kwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
“kile ni kitendo cha kinyama na kinapaswa kulaniwa na kila
mtu, kinasikitisha sana na kimeweza kurudisha nyuma maisha ya watu, watu
wanategemea kuendesha familia zao pale halafu wanakwamishwa na watu
wachache”alisema.
Alisema tasnia ya habari imekuwa kihimiza maendeleo ya nchi,
ikiwemo vijana kujiajiri wenyewe na kutokutegemea ajira kutoka serekalini,
amevitaka vilabu vya habari kuwa mtari wa mbele kukisaidia kituo hicho kwa hali
namali.
Kwa upande wake Saidi Mohamed Ali alisema sasa wakati
umefika kwa wamiliki wa vyombo vya habari kuwatafutia bima ya maisha
wafanyakazi wao, kutokana na matukio ya kuvamiwa kwa vituo vya redio kuendelea
kutokea.
“Mungu aliwajaaliwa hawakuweza kumzuru mwandishi aliyekuwemo
studio kama wangemdhuru wangekuwa wameshapoteza malengo yake”alisema.
Alisema matukio kama hayo yanaashiria kurudisha nyuma uhuru
wa habari, jambo ambalo ni kwenda kinyume na katika za nchi ambazo zimehimiza
haki ya kutoa na kupata habari.
No comments:
Post a Comment