WAALIMU NCHINI WAMETAKIWA KUWAPA FURSA NA KUWAHAMASISHA
WANAFUNZI WA SKULI MBALIMBALI KUSHIRIKI KATIKA MICHEZO ILI
KUWEZESHA KUPATA TIMU NZURI NA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA.
HAYO YAMEELEZWA NA MKURUGENZI WA IDARA YA MAENDELEO YA
MICHEZO WIZARA YA HABARI UTAMADUNI WASANII NA MICHEZO TANZANIA LEONA TADEO
KATIKA UWANJA WA AMANI NJE WAKATI ALIPOKUA AKIFUNGA SHAMRASHAMRA ZA
TAMASHA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
AMESEMA KATIKA NCHI YA TANZANIA WANANCHI WENGI HULALAMIKA
KWA KUTOFANYA VIZURI KATIKA MICHEZO KUTOKANA NA WAALIMU
KUSAHAU WAJIBU WAO WA KUWAJENGA WANAFUNZI WAO KIMICHEZO TANGU WADOGO
WAKATI WAPO MASKULINI JAMBO AMBALO LINAREJESHA NYUMA MAENDELEO YA MICHEZO
HIYO.
AIDHA AMEFAHAMISHA KUWA IWAPO JAMII ITASHIRIKI KATIKA MICHEZO
MBALIMBALI ITAWEZA KUJIEPUSHA NA MARADHI SAMBAMBA NA KUJENGA AFYA HIVYO
ZOEZI HILO LIWE ENDELEVU KWANI KUFANYA HIVYO KUTASAIDIA WALIMU KUWA IMARA
KIMICHEZO.
HATA HIVYO MKURUGENZI HUYO AMEWATAKA WAALIMU KUTOA FURSA
KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA HUUSIKA KWENDA KUSOMA KATIKA CHUO CHA
MAENDELEO YA MICHEZO TANZANIA BARA ILIKUONGEZA UWEZO NA IDADI YA WAALIMU WA
MICHZO.
KWA UPANDE WAKE MWALIMU MUSSA ABDULRABI KUTOKA
WIZARA YA ELIMU AMESEMA LENGO LA KUFANYA TAMASHA HILO NI KUWAFANYA WALIMU
KUSHIRIKI MICHEZO MBALIMBALI NA KUONESHA VIPAJI VYAO KATIKA MICHEZO HIYO.
AMESEMA KATIAKA MWAKA HUU HAKUNA CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA
HIVYO WANAJIANDAA KWA AJILI YA MWAKANI ILI WAWE NA UWEZO WA KUFANYA
VIZURI ZAIDI KATIKA TAMASHA LIJALO .
SAMBAMBA NA HAYO MWALIMU HUYO AMEAAHIDI KUWA WATAWASHAJIISHA
WALIMU WENZAO KWENDA KUJIUNGA NA CHUO CHA MAENDELEO YA MICHEZO ILI
KUPATA WALIMU WENGI KWA AJILI YA MICHEZO KWANI SEREKALI INA NIA YA
KUENDELEZA MICHEZO .
WAKIELEZEA FURAHA ZAO WASHINDI KATIKA TAMASHA HILO WAMEIOMBA
WIZARA KUANGALIA SUALA LA MICHEZO ZAIDI KWA KUANDALIWA MAFUNZO MAALUM ILI
KUWEZA KUSHIRIKI KATIKA MASHINDANO MBALIMBALI.
KATIKA SHAMRASHAMRA HIZO KUMEFANYIKA MICHEZO MBALI MBALI
IKIWEMO KUVUTA KAMBA, MPIRA WA MKONO,MBIO ZA GUNIA PAMOJA NA MPIRA WA
MIGUU KUTOKA KATIKA MIKOA MITATU YA ZANZIBAR IKIWEMO MKOA KUSINI UNGUJA ,
KASKAZINI UNGUJA NA MKOA WA MJINI MAGHARIB AMBAPO MKOA WA KASKAZINI NA MJINI
NDIO WALIOIBUKA WASHINDI IKIFUATIWA NA MKOA WA KUSINI UNGUJA.
MWISHO
No comments:
Post a Comment