Wa kwanza kutoka Kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Afya na
Elimu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Bibi Kokushubila Kairuk na
kati kati ni Mkuu wa Kitengo cha Michezo wa Chuo hicho Mwalimu Alphage Liwa.
Dr. Mambi akikabidhi pia Kikombe ambacho kinaweza kusaidia
mashindano ya Timu za Wanafunzi wa mikupuo tofauti wa chuo hicho cha Kumbu
kumbu ya Hubert Kairuki.
Bibi Kokushubila Kairuk wa kwanza kutoka kushoto ambae ni
Mwenyekiti wa Mtandao wa Afya na Elimu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert
Kairuki akitoa shukrani kwa Balozi Seif kutokana na mchango wake chuoni hapo
katika sekta ya Michezo.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Afya na Elimu wa Chuo Kikuu cha
Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Bibi Kokushubila Kairuk alisema kitendo cha baadhi
ya Viongozi na washirika wa maendeleo kuendelea kuunga mkono Taasisi za Umma za
zile binafsi huleta faraja katika Jamii.
Bibi Kokushubila alieleza hayo wakati akipokea msaada wa
vifaa vya michezo vilivyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Mtaa wa Mikocheni Mjini Dar es salaam.
Vifaa hivyo vikiwa ni pamoja na Seti ya Jezi, Mipira ya
kandanda na Vikapu, soksi, Bukta pamoja na sare za mlinda Mlango kwa ajili ya
Timu ya Chuo Kikuu hicho viliwasilishwa Chuoni hapo na Daktari wa Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Dr.Juma Mbwana Mambi kwa niaba yake vikiwa na thamani ya
zaidi ya shilingi Milioni Moja.
Bibi Kokushubila alisema michezo ni moja ya eneo
linalounganisha jamii hasa Vijana ambayo linahitaji kupewa msukumo kwa vile
huchangamsha Vinjana hao Kiakili na kimawazo.
Mwenyekiti huyo wa Mtandao wa Afya na Elimu wa Chuo Kikuu
cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi kwa msaada wake huo ambao umeleta faraja kwa Wanafunzi
sambamba na Uongozi wa Chuo hicho.
Bibi Kokushubila alisisitiza umuhimu wa kuendelezwa kwa
ushirikiano baina ya Taasisi husika na washirika wa sekta ya Michezo ili kuona
fani hiyo inapata nguvu zaidi kwa vile tayari imeshaonyesha muelekeo wa kutoa
ajira kwa kundi kubwa la Vijana.
Mapema akiwasilisha msaada huo wa Vifaa vya Michezo Dr. Juma
Mbwana Mambi kwa Niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Mh. Balozi
Seif aliahidi kuendelea kusaidia sekta ya michezo kutokana na umuhimu wake kwa
hivi sasa.
Dr. Mambi alisema juhudi zitaendelea kuchukuliwa na
Mh. Balozi ili kuona michezo Nchini inadumishwa na kuendelezwa zaidi kwa faida
na ustawi wa Jamii yote.
Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki kiliopo
Mikocheni Mjini Dar es salaam mbali ya kutoa Taaluma ya Elimu ya Afya pia
kinadumisha michezo kwa nia ya kuwajenga afya wanafunzi na walimu wake.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa 9ili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment