tangazo
Wednesday, December 2, 2015
KMKM NA JKU WANGARA LIGI KUU ZANZIBAR
kikosi cha timu ya kmkm zanzibar
kikosi cha timu ya jku zanzibar
Na: Abubakar Kisandu, Zanzibar.
Timu ya mabaharia ya KMKM leo hii imeonja ladha ya ushindi kwa mara ya kwanza kwenye ligi kuu soka Zanzibar kanda ya unguja walipoifunga Mtende Renger (Kilimani city) bao 1-0 mchezo uliosukumwa saa 10 za jioni kwenye uwanja wa Amaan.
Bao pekee la KMKM limefungwa na Faki Mwalim mnamo dakika ya 23 ya mchezo huo.
Pambano jengine lilisukumwa saa nane mchana JKU imejipatia ushindi wake watatu mfululizo baada yakuifunga Polisi jumla ya magol 2-1.
Magoli ya JKU yamefungwa na Mbarouk Chande dk 73 na khamis said dk 78 wakati lile la Polisi limefungwa na Muhamed Seif Belo dk 10.
Kwa matokeo hayo polisi amecheza michezo 2 na yote ameshafungwa ambapo wa kwanza alifungwa na black sailors mabao 2-1, na leo hii tena akipigwa na JKU mabao 2-1.na kwenye msimamo Polisi wapo nafasi ya 13 kati ya timu 14.
Lakini kwa upande wao JKU kwasasa ndio kinara wa ligi hiyo wakiwa wamecheza michezo 3 na yote wamepata ushindi, walianza kuwafunga mafunzo mabao 2-1, wakaitwanga Black Sailor mabao 2-0, na leo hii kaitwanga Polisi mabao 2-1.
Kwa upande wao Mtende Renger wanashika nafasi ya 12 kati ya timu ya 14 za kanda ya unguja ambapo wanapoint 1 tu katika michezo yao 4.
KMKM wao wanashika nafasi ya 4 wakiwa na point 6 katika michezo yao 4 walocheza.
Ligi hiyo kesho itakwenda mapumziko na itasukumwa tena ijumaa kwa kuchezwa michezo 2 kwenye uwanja wa Amaan.
Saa8 za mchana wataanza kati ya Kijichi na Miembeni na saa10 watapepetana Black Sailors na Zimamoto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment