KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI JUU YA UTEUZI WA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI KWA
SERIKALI YA JAMUHURI YA MUNGANO WA TANZANIA.
Awali ya yote shirikisho la vyuo vya elimu ya juu CCM –
Zanzibar
linapenda kuchukua fursa hii , kumshukuru
M/Mungu
kwa kutujaalia nchi yetu kuwa
katika hali ya
amani
na utulivu.
Pili, tunachukua fursa hii kuwashukuru nyinyi vyombo vya
habari kwa mahudhurio yenu mazuri kuja
kuchukua taarifa kwa lengo la kuwahabarisha umma juu ya mustakbal wa nchi yetu.
Shirikisho la vyuo vya elimu ya juu
CCM -
Zanzibar Linampongeza Rais wa
Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na
wasaidizi wake Makamu wa Rais na Waziri mkuu kwa kulitangaza Baraza jipya la
mawaziri.
Aidha, sisi shirikisho la vyuo vya
Elimu ya juu CCM Zanzibar tunampongeza sana Mhe. Rais Magufuli kwa kufanya
uteuzi wa baraza jipya la mawaziri kwani watu walioteuliwa wana uwezo wa
kutosha katika kuisaidia jamii ya watanzania.
Pamoja na kuunga mkono wa uteuzi wa
baraza hilo, pia tunampongeza kwa kasi alioaanza nayo ya kubana matumizi katika
kuendesha serikali, kitendo hicho kinaashiria moyo wa dhati aliokuwa nao katika
kuleta maendeleo ya Tanzania na watanzania kwa ujumla.
Ndugu waandishi wa habari tunaomba
ifahamike kuwa Mhe. Rais anatekeleza ilani ya CCM 2015/2020 ambayo imetoa
vipaumbele katika maeneo manne makuu
i.
Kupunguza
umaskini wa watanzania
ii.
Kutatua
changamoto ya ajira kwa vijana.
iii.
Kupambana
na rushwa na ufisadi na
iv.
Kudumisha
amani ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Ndugu wandishi wa habari, kutokana na
baraza la mawaziri na watu walioteuliwa tunaamini ya kwamba ilani yetu ya CCM
itatekelezwa kwa asilimia kubwa na itarejesha heshima kwa chama chetu.
Tunawaomba kwa dhati mawaziri
walioteuliwa watekeleze majukumu yao kwa nguvu zao zote katika kumsaidia DK.
Magufuli kusukuma gurudumu la maendeleo la taifa letu.
Ifahamike kuwa, Mhe. Rais amefanya
mambo makubwa wakati hajateuwa baraza la mawaziri, hivyo kupitia taarifa hii
tunawaomba wateule hao kuengeza kazi kwa kuchapa kazi ili wamsaidie Mhe. Rais
kuyatumbua majipu bila ya woga.
Sambamba na hayo, shirikisho la Vyuo
vya Elimu ya juu CCM Zanzibar tunampongeza sana Mhe. Balozi Seif Ali Iddi Makam wa pili wa Rais wa Serekali ya M
apinduzi ya Zanzibar, pia mjumbe wa kamat ya ccmi kwa utendaji wake mzuri kwa kuwataka mamlaka ya
maji Zanzibar (ZAWA) kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua watendaji waliotumia
dhamana zao vibaya katika kusimamia huduma za maji.
Lakini pia tunampongeza Mhe. Makamu
wa pili kwa kusitisha mara moja Bw. Anuar Abdulla kufanya ujenzi wa nyumba ya
ghorofa katika maeneo ya makaazi ya watu hapo mlandege kwani eneo hili
linatumika kwa ajili ya shughuli za kijamii.
Mwisho, shirikisho la vyuo vya Elimu
ya juu Zanzibar linawaomba viongozi wa juu wa serikali ya Mapinduzi
Zanzibar pamoja na watendaji wote kuiga
mfano wa Mhe. Magufuli katika kufanya kazi kwa maslahi mapana ya umma pamoja na
kudhibiti matumizi mabaya ya serekali pia kudhibiti mianya ya uvujaji wa mapato
sambamba na kuwatumikia wananchi wa Zanzibar. Kwani hii imejidhihirisha wazi
wazi katika ahadi za mwana ccm ambayo inasema ˵Cheo ni dhamana, sitatumia cheo
changu wala cha mtu mwengine kwa faida yanguˮ
Ahsanteni kwa
kunisikiliza.
‘’ Mungu
ibariki Zanzibar’’
‘’Mungu ibariki Tanzania ‘’
‘’Mungu ibariki Afrika”
KIDUMU CHAMA CHA
MAPINDUZI
Imetiwa Saini na Katibu,
………………………………………..
No comments:
Post a Comment