tangazo

tangazo

Monday, December 7, 2015

TUME YA MIPANGO ZANZIBAR YATAKIWA KUHARAKISHA KILA KILICHOPANGWA KWA WAKATI.

PEMBA.

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe: Mwanajuma Majid Abdalla, ameitaka Tume ya Mipango Zanzibar, kuharakisha kila kilichopangwa kiweze kutekelezeka bila ya Usumbufu wowote.

Mhe: Mwanajuma alisema kama tume itaweza kutekeleza yale yote yaliyoyomo ndani ya sheria na kanuni yake, basi Serikali inaweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo.

Hayo aliyaeleza huko ofisini kwake Cheke Chake wakati, wajumbe wa Tume ya Mipango Zanzibar ilipofika kwa lengo la kujitambulisha uwepo wao, wakiongozwa na Kamishana wa Tume hiyo Mashavu Khamis.

Aliwapongeza wajumbe wa tume hiyo, kufika kwao kujitambulisha ili kuweza kujuwana, kwani kazi zao wanazozifanya maafisha Mipangano ni nzito.

Alifahamisha kuwa Tume ya Mipango ndio Utu wa mgogo wa Serikali, hivyo wajumbe wanapaswa kuhakikisha yote yanatekelezeka kwa mujibu wa sheria na kanuni.

“Kama Tume itakwenda sawa sawa na haya yaliyomo kwenye sheria yenu basin chi itaweza kupiga hatua kubwa sana kwani wananchi watafurahi na kuridhika nayo”alisema Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Wilaya ya Mkoa Mhe: Hemed Suleiman Abdalla, alisema Duniani kote Tume ya Mipango ndio kitu muhimu katika nchi yoyote ile katika kufikia maendeleo.

Alisema licha ya kuwa mpya lakini wanapaswa kuendelea kujitahidi ili sehemu zenye zenye mapungufu ziweze kutekelezeka kama ilivyopangwa katika sheria zenu.

“Kazi zenu ni ngumu sana ila Mwenyezi Mungu atawasaidia katika kutekeleza yote muliojipoangia na kuweza kufikia mafanikio”alisema.

Kwa upande wake afisa Mipango Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Sheha Mtumwa Mpate aliitaka tume ya Mipango kuhakikisha inawaongezea nguvu katika utendaji wao wa kazi ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ya Kila Mwaka.

Naye kamishna wa Tume ya Mipango Zanzibar Mashavu Khamis, aliwashukuru Viongozi wa Serikali ya Mkoa wa kusini Pemba, huku akuwataka viongozi hao kuwaombea dua katika utendaji wao wa kazi.


Alisema tume imekuwa ikihitaji mambo mengi ikiwemo nyezo za kufanyia kazi, lakini upatikanaji wake ni mdogo hivyo watajitahidi kuhakikisha wanafuata kanuni na sheria katika utendaji wao wa kazi.

No comments:

Post a Comment