MUDATHIR KHAMIS
Baada ya kuzagaa taarifa hizo kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa mlinda mlango wa Yanga mudathir Khamis ameachwa, mtandao huu leo hii tukamtafuta mchezaji huyo na kusema kuwa amependelea aongee kocha wake wa zamani wa KMKM Ali Bushir taarifa hizo ambapo tayari kamuonesha barua yake.
Tukamtafuta kocha Ali Bushir na kuthibitisha kuwa kweli Muda ameachwa na Yanga.
“ Nikweli Muda ameachwa na Yanga na mimi leo asubuhi kaniletea barua hiyo ambayo kasaini katibu wa Yanga, nimeipitia barua hiyo ya kusitisha rasmi Yanga na kumuwachia muda awe huru kwenda klabu yoyote, iyo barua imeeandikwa tarehe 21 ya mwezi ulopita ikisema kuwa Muda si mchezaji tena wa Yanga”. Alisema kocha Bush.
Aidha kocha Bushir alisema wachezaji lazima wawe makini pale wanapotia mkataba na timu kwa kutafuta mwana sheria ambae atakaemsimamia ili asije kukosa haki zake za msingi pindi zitapotokea matatizo mengine ya kusitishwa mikataba yao kiholela.
No comments:
Post a Comment