CHAMA CHA ADA
– TADEA
UHURU WA TANGANYIKA KUFIKIA MIAKA 54
Ni fahari ya
watanganyika kusherehekea uhuru wao kwa kujua wapi wanapotoka na wapi
wanapokwenda kwa mujibu wa sheria.
Kama tunavojua Tanganyika
ilipata uhuru kutoka kwa mkoloni tarehe 9
December 1961 na wakapata kiti cha umoja wa Mataifa tarehe 14 December 1961 namba ya kiti chao (GA Resolution 1667(XVI) na ikawa nchi huru. Lakini ilipofika tarehe 26 April 1964 iliungana na Zanzibar na kua Tanzania ambayo ipo mpaka sasa
lakini tukirudi nyuma maendeleo makubwa ya miji na watu sambamba na maendeleo
ya miundombinu na mawasiliano ya kitaifa na kimataifa mawasiliano ya jamii na
ya mtu kwa mtu. Lakini kama hiyo haitoshi uhuru huu umeleta heshima kwa taifa
na jamii na umeondondosha dharau na
kuimarisha upendo kwa kuondoa ubaguzi wa rangi ukabila na udini na kuijengea
sifa Tanganyika na watanganyika wenyewe . Lakini uhuru huo wa Tanganyika kuna changamoto nyingi za maendeleo
kwa mfano; 1962 Tanganyika ilikua ninchi ya pili
duniani inayozalisha mbao. nchi ya kwanza ilikua ni Crprus. Lakini kwa sasa
Tanganyika kama Tanzania tunashuhudia watoto wa shule wanakaa chini lakini kama
nchi ilokua inatoa mbao nyingi na kama hiyo haitoshi Tanganyika kwa sasa
wanahifadhi za kitaifa18 sambamba na
mbuga za wanyama, tukilinganisha na nchi
za jirani Kenya waliopata uhuru wao tarehe 10/December
1963 ilojulikana kama (madaraka day) ambao wanasherehekea kesho lakini
Kenya wao wanahifadhi 8 za kitaifa lakini Kenya ni ndogo sasa kwa Tanzania
hawana ardhi kubwa hata katika hecta za miraba Tanganyika bado kubwa.
Tanganyika wana watu wasiopungua milioni 40,000,000
kenya wao wana watu wasiopungua milioni 18,000,000
lakini wakenya wapo juu kiuchumi unaoendana na elimu sahihi na kwa hilo kwa
ushindi mwengine pesa ya Kenya ilikuwa sawa sawa mia kwa mia kubadilishana
lakini kwa sasa pesa ya Kenya ipojuu mia Kenya kwa 12 ya Tanzania. Na hii
inatokana na kushuka kiuchumi na ukizingatia Tanganyika
ina rasilimali nyingi kulikokenya kama vile
gasi, uranium, chuma ambayo madini hayo yanatosha kwa kuinua uchumi wa taifa.
Lakini siri kubwa ya maendeleo ya wakenya inatokana na kutumia vyema rasilimali
zao sambamba na kutumia rasilimali watu kwa kutumia vipaji na elimu ya wakenya
kwa kuinua maendeleo na ustawi wa jamii kwa mujibu wa sheria ya Kenya. Na kwa Tanganyika wanatakiwa walione hilo . Na wapunguze uzembe ubadilifu na rushwa ili kuleta maendeleo ya
kweli sambamba kutumia rasilimali zao na rasilimali watu kwa kudumisha umoja na
kutooneana muhali kwa wale wanaohujumu mali za serikali. Lakini hata hivyo
sera ya kilimo kwanza itawakomboa watanganyika kama
tunavyojua asilimia 75 watanzania ni wakulima na wafugaji lakini hata hao
wafanyakazi nao ni wakulima na wafugaji ipo haja kwa sasa serikali kuimarisha
pembejeo za kilimo na kuwa kilimo cha kisasa ambacho hutumia mbolea. Tatizo la
wakulima ni masoko ya kununulia bidhaa sambamba na viwanda vya kilimo kwa sasa
kunahitajika viwanda vya matunda kama vile lushoto kunatakiwa kiwanda kikubwa
cha kusindika matunda ili kuokoa matunda yasiharibike ovyo lakini kwa kuacha
wakulima wa pamba na wa korosho kutowalipa na kuwacheleweshaea kuwalipa pesa zao. Kunapunguza jitihada za wakulima na
kupelekea kudumaza sera ya kilimo kwanza. Lakini kufika miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika uhuru huo ni faraja na
heri kwa watanganyika ili kuondosha tatizo la afya, elimu na ajira. Na hili ni
tatizo kubwa kwa maendeleo ya watanganyika na hata watanzania kwa ujumla
ikiwepo Zanzibar .
Bado wananchi wanataka afya bora elimu juu na ajira zaidi.
Na kwa upande wa
afya kuna haja ya kuboresha vituo vya afya katika kata na vitongoji ili
wananchi ziwafilie huduma hizo tena huduma ziwe bora na kuhusu suala la elimu
bado watanganyika wanahitaji elimu bora inayoendana na wakti kwa kuwa na
mitaala bora, shule za mabweni zenye maabara kwa mfumo huo wa elimu mzuri
unaofuata vigezo vya mataifa ili kupata elimu bora itakayokwenda sambamba na
katika shule za kata tarafa na vijiji. Kwa sababu taifa lolote linakua bora kwa
elimu. Na kwa upande wa ajira kufufua viwanda vilivyokufa na kuongeza vingine ili
kuweza kupata ajira kama tunavyojua ajira sahihi ya nguvu kazi kama tunavyojua
ajira sahihi ulimwenguni ni ile ya viwanda ambayo hutoa ajira ambao wamesoma na
ambao hawajasoma ( ajira ya nguvu kazi).
Kwasasa
watanganyika au watanzania ni fahari yao kwa kuwa na kiongozi ambae John Joseph
Pombe Magufuli ambae ana sera ya hapa ni kazi tu na ndiomana siku ya Uhuru wa
Tanganyika amesema tusherehekee kwa kuokoa fedha na kupeleka katika maendeleo ya
jamii kama vile barabara. Hata hivyo sera zake kama vile kuendeleza viwanda, mifugo
wakulima,uvuvi na hata kusema atakuwa na sera ya viwanda ambayo itatokana na
kilimo, mifugo, uvuvi na kuondosha tatizo la ajira kwa asilimia 40% ifikapo 2020 na kuona tatizo la ajira linaondoka kwa kias. Lakini itapofika
2016 ilimu itakua bure yaani bila
malipo, hii yote ni faraja na maendeleo makubwa kwa Tanganyika na Tanzania kwa
ujumla lakini uokozi wa fedha za serikali zilizokua zishapotea umakini wa
viongozi hawa unaweza kuleta maendeleo kwa sasa Mh Rais Magufuli, Waziri mkuu
Majaaliwa Kassim na Mama Jasiri Samia Suluhu ni wachapakazi na wafatilia wasimamizi
wa shughuli za jamii kwa kuona kazi zinafanyika kua hapa kazi tu . Watu
wataweza kuona tunainuka kiuchumi kwa muda mfupi tu kwa kufikia uchumi wa kati
na kupunguza umasikini na kuona jirani zetu Kenya tunawapita kwa maendeleo kwa
kutumia rasilimali watu kiuhakika sambamba na rasilimali zetu zilizomo nchini
kama mafuta, gesi, urenim, chuma na madini mbalimbali yalozuka nchini na
yalokuwemo sambamba na kutumia hifadhi za kimataifa kwa kukuza utalii wa ndani
na nje kwa kuzifanyia kazi vizuri nilizozitaja nchini ya awamu mpya ya uongozi
wa Mh John Pombe Magufuli tutatimiza malengo makuu ya kiuchumi na ulimwengu
utaona hilo
Ahsante
ITAWEZEKANA SANA TUKIONDOSHA UZEMBE, UFISADI, RUSHWA
MUHALI NA TUKIFUATA KAULI MBIU YA WAASISI WETU WALIPOSEMA UHURU NA KAZI.
Wako Mwanasiasa Mkongwe (Mwanaharakati)
Katibu mwenezi
Taifa ADA
– TADEA
………………………..
RASHID YUSSUF MCHENGA
0715560243
0773560243
No comments:
Post a Comment