Afisa wa Polisi S.P Zakaria Benard akitoa shukrani kwa niaba
ya Jeshi la Polisi kwa uamuzi wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
wa kuifariji familia ya askari wa ngazi ya chini ya Jeshi la Polisi
Nchini Marehemu Yesaya aliyefariki kwa ajali ya Piki piki akiwa kazini.
Jeshi la Polisi Nchini limeelezea faraja yake kutokana na
mfumo wa Viongozi wa Kitaifa kuonyesha muelekeo wa kuwajali watumishi wao
kutoka Taasisi tofauti za Umma na hata binafsi lakini zaidi wake watumishi wa
ngazi ya chini.
Afisa wa Polisi S.P Zakaria Benard alitoa faraja hizo kwa
niaba ya Jeshi la Polisi wakati akitoa shukrani za Jeshi hilo mbele ya Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika katika Kata ya Goba
Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam kutoa mkono wa pole pamoja na kuifariji
Familia ya Koplo Yesaya Mwakambi aliyefariki Dunia kwa ajali ya Piki pili
Ubungo Jijini Dar es salaam.
Koplo Yesaya ni miongoni mwa Askari wa Usalama Bara barani
wa Jeshi la Polisi Nchini wanaowajibika kuiongoza Misafara ya Viongozi Wakuu wa
Kitaifa akiwemo wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipata ajali akiwa
kazini mwezi Mmoja na nusu uliopita .
S.P Zakaria Benard alisema kitendo cha Viongozi hao wa
Kitaifa kuungana na Watumishi wao wa ngazi ya chini kimeonyesha upendo, huruma
na moja ya njia itakayotowa mapenzi ya dhati kati ya pande hizo mbili kuendelea
kushirikiana katika ujenzi wa Taifa.
Kamanda Zakaria alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif kwa uamuzi wake wa kutenga muda kwa lengo la kuifariji
Familia ya Koplo Yesaya.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafamilia wa Koplo huyo
Mchungaji Isaya Isaleka aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuisadia
Familia ya Marehemu Koplo Yesaya Mwakambi ili iweze kuwa na nguvu za
kukabiliana na maisha yao ya baadaye.
Mchungaji Isaleka alisema katika uhai wake tayari alikuwa
aameshaanza kujenga hatma ya familia yake ya watoto wawili wadogo kwa kuwawekea
vitega uchumi alivyovianzisha kwa nia ya kuwasaidia hapo baadaye lakini
kukatika kwa uhai wa Kijana huyo pia umeenda sambamba na kusita kuendelea kwa
vitega uchumi hivyo.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiifariji Familia
hiyo inayoongozwa na Mke wa Marehemu Bibi Wema Sanga alisema familia
ilikuwa ikimpenda sana Marehemu, lakini Mwenyezi Muungu alimpenda zaidi na ndio
maana akaamua kumrejesha katika himaya yake ya milele.
Balozi Seif aliitaka familia ya marehemu Yesaya hasa Mkewe
Mama wa watoto wawili Bibi Wema Sanga kwa kuwa na moyo wa subira katika kipindi
hichi kifupi walichoondokewa na Mpendwa wao.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa 9ili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment