tangazo

tangazo

Friday, January 31, 2014

UZALENDO KWA RAIA


ZANZIBAR

IMELEZWA KUWA  TAIFA LOLOTE DUNIANI HALIWEZI KUPIGA HATUA YA MAENDELEO ENDELEVU BILA YA RAIA WAKE KUWA NA UZALENDO.

 

HAYO YAMEELEZWA NA MKURUGENZI  WA MIPANGO NA UENDESHAJI SERA WA CHAMA CHA WAKULIMA TANZANIA AFP NDUGU RASHIDI YUSSUF MCHENGA KATIKA TAARIFA YAKE KWA VYOMBO VYA HABARI.

 

AMESEMA UZALENDO NI KITU MUHIMU KWA TAIFA,JAMII NA HATA MTU MMOJA MMOJA NA ILI KUFIKIA MAENDELEO  NI LAZIMA KWA KILA MTU KUFUATA UTARATIBU WA KANUNNI ZA NCHI NA HAKI ZA BINADAMU KWA MUJIBU WA SHERIA.

 

HATA HIVYO AMESEMA NCHI NYINGI ZILIZOPIGA HATUA DUNIANI WATU WAKE WALIKUWA NA MOYO WA KIZALENDO NA KUPELEKEA MKUBWA KUMUHESHIMU MDOGO NA MDOGO KUMUHESHIMU MKUBWA.

 

VILEVILE AMETOLEA MFANO KWA NCHI KAMA SYRIA,MISRI,LIBYA NA SUDANI KUSINI WANANCHI NA VIONGOZI WAO WALIKOSA UZALENDO NA KUAMUA KUVUNJA SHERIA NA KATIBA ZAO NA KUPELEKEA KUZIHARIBU NCHI ZAO KIUCHUMI NA KIMAENDELEO KWA KUHARIBU MIUNDOMBINU MBALI MBALI SAMBAMBA NA MALI ZA UMMA.

 

SAMBAMBA NA HAYO AMESEMA KUNA HAJA YA KUTOLEWA ELIMU YA URAIA KWA WANANCHI WA TANZINIA KUANZIA NGAZI YA SHEHIA,VITONGOJI,KATA NA HATA NGAZI YA TAIFA SAMBAMBA NA KUPELEKA ELIMU HIYO MASHULENI ILI RAIA WAKE WAWE WAZALENDO.

RAIS SHENI NA BALOZI WA FINLAND


ZANZIBAR

 

RAIS WA ZANZIBAR AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN JANA AMEKUTANA NA WAZIRI MKUU WA FINLAND BWANA JYRKI KATAINEN NA KUFANYA MAZUNGUMZO KUHUSU UHUSIANO NA USHIRIKIANO KATI YA ZANZIBAR NA FINLAND.

 

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO YALIYOFANYIKA IKULU ZANZIBAR DK. SHEIN AMEISHUKURU SERIKALI YA FINLAND KWA MISAADA YAKE MBALIMBALI AMBAYO IMEKUWA IKIITOA KWA ZANZIBAR NA TANZANIA KWA JUMLA.

 

ALIBAINISHA KUWA UHUSIANO MZURI KATI YA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA FINLAND IMEIWEZESHA ZANZIBAR KUPOKEA MISAADA KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA MAENDELEO, HUDUMA ZA JAMII NA HIFADHI YA MAZINGIRA.

DK. SHEIN ALIELEZA KUFURAHISHWA KWAKE NA UAMUZI WA SERIKALI YA FINLAND KUENDELEZA USHIRIKIANO WAKE NA ZANZIBAR KWA KUENDELEZA MRADI WA UHIFADHI WA ARDHI NA MAZINGIRA KWA AWAMU YA PILI (SMOLE II) BAADA YA KUMALIZIKA KWA AWAMU YA KWANZA.

 

HATA HIVYO RAISI WA ZANZIBAR AMEKARIBISHA WAZO LA KUSHIRIKIANA NA FINLAND KATIKA KUTEKELEZA AZMA YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YA KUTAFUTA NJIA MBADALA ZA KUPATA NISHATI YA UMEME.

 

ALIELEZA KUWA NI KWELI HIVI SASA ZANZIBAR INAPATA UMEME WA KUTOSHA KUPITIA MKONGA WA UMEME TOKA TANZANIA BARA LAKINI HAITAKUWA AJABU BAADA YA MIAKA MICHACHE IJAYO KUTOKANA NA KASI YA ONGEZEKO LA MATUMIZI YA UMEME YANAYOTAKANA NA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI KIASI KILICHOPO SASA KIKAWA HAKITOSHI HIVYO NI JAMBO LA BUSARA KUWA NA MPANGO MBADALA WA KUPATA NISHATI HIYO.

 

WAKATI HUO HUO WAZIRI MKUU WA FINLAND BWANA JYRKI KATAINEN AMEMPONGEZA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI KWA MAFANIKIO ALIYOYAPATA KATIKA KUIONGOZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ILIYO CHINI YA MFUMO UMOJA WA KITAIFA.

AMESEMA MFUMO HUO UNASAIDIA KULETA MAELEWANO BAINA YA VYAMA NA UZOEFU UNAONYESHA KUWA UTAMADUNI WA UENDESHAJI WA SERIKALI KWA MFUMO KAMA HUO NA MINGINE INAYOFANANA NA HUO UNATUMIKA SANA HIVI SASA.

AJALI KASKAZINI UNGUJA KWA MWAKA JANA


MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

 

JUMALA YA MATUKIO SABINI NA MOJA YA AJALI ZA BARABARANI YAMERIPOTIWA KUTOKEA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2013.

 

AKIZUNGUMZA NA ADHANA FM REDIO KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI MKOA WA KASKAZINI UNGUJA HASSAN MSANGI AMESEMA KUTOKANA NA KUWEPO KWA HALI YA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA BARABARANI KWA BAADHI YA MADEREVA  KUMEPELEKEA ZAIDI YA WATU ISHIRINI KUPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUPATA ULEMAVU WA VIUNGO.

 

AKIYATAJA MAENEO YALIYOONGOZA KWA MATUKIO YA AJALI ZA BARABARANI NI PAMOJA NA KAZOLE,MGAMBO,MKWAJUNI NA NUNGWI.

 

AMEFAHAMISHA KUWA KWA SASA JESHI LA POLISI LIMEIMARISHA ULINZI ZAIDI KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA MKOA HUO KWA LENGO LA KUEPUSHA AJALI ZA BARABARANI.

 

SAMBAMBA NA HAYO AMEWATAKA MADEREVA WAWE WAANGALIFU NA KUFUATA SHERIA BILA YA KUSHURUTISHWA SAMBAMBA NA KUZINGATIA ALAMA ZA BARABARANI ILI KUWAEPUSHIA USUMBUFU WATEMBEA KWA MIGUU.

WAKULIMA WA MWANI


WILAYA YA KUSINI UNGUJA

 

WAKULIMA WA MWANI WAMEYAOMBA MAKAMPUNI YA KUNUNUA MWANI KUANDAA UTARATIBU MAALUM WA KUWAONGEZEA BEI YA BIDHAA HIYO ILI WAWEZA KUENDELEZA NA KUBORESHA ZAO HILO NCHINI.

 

WAKIZUNGUMZA NA ADHANA FM REDIO MMOJA YA WAKULIMA HAO BI MTUMWA SULEIMANI KHAMIS HUKO MAKUNDUCHI WILAYA YA KUSINI,AMESEMA WAKULIMA WA MWANI WANAKATA TAMAA YA KUENDELEZA KILIMO HICHO KUTOKANA NA BEI YA MWANI KUWA NDOGO.

 

WAMESEMA LICHA YA KUONGEZEKA JITIHADA ZA KUENDELEA KULIMA ZAO HILO LAKINI KUTOKANA NA BEI NDOGO YA ZAO HILO LIMEWASABABISHIA KUACHA KULIMA ZAO HILO.

 

KWA UPANDE WAKE MNUNUZI WA MWANI KITUO CHA MAKUNDUCHI NDUGU KHATIBU ABDAALLAH OMARI AMESEMA MWANI NI BIASHARA AMBAYO HUUZWA NJE YA NCHI NA INATUMIA GHARAMA KUBWA HADI KUFIKA KATIKA SOKO JAMBO AMBALO LINAWAPELEKEA KUTOKUZIDISHA BEI YA ZAO HILO.

 

HATA HIVYO AMEIOMBA SERIKALI KUPUNGUZA  USHURU KWA MAKAMPUNI YANAYOSAFIRISHA MWANI MWANI ILI WAWEZE KUONGEZA BEI KWA WAKULIMA WA ZAO HILO.

Thursday, January 30, 2014


RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA UHUSIANO NA USHIRIKIANO KATI YA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR NA INDIA UMEKUWA UKIIMARIKA SIKU HADI SIKU AMBAPO WAKATI WOTE PANDE MBILI HIZO ZIMEKUWA ZIKIFANYA JITIHADA ZA KUONA USHIRIKIANO HUO UNALETA TIJA ZAIDI KWA KILA UPANDE.

DK. SHEIN AMESEMA HAYO LEO WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA BALOZI MDOGO WA INDIA BWANA PAWAN KUMAR AMBAYE ALIFIKIA IKULU KUMUAGA RAIS BAADA YA KUMALIZA KIPINDI CHAKE CHA KUITUMIKIA NCHI YAKE HUMU NCHINI.

AMEBAINISHA KUWA TANGU UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA ULIPOANZISHWA MIAKA YA SITINI NCHI HIZO ZIMESHUHUDIA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UHUSIANO HUO HUKU PANDE HIZO ZIKISHIRIKIANA KATIKA MAENEO MBALIMBALI IKIWEMO ELIMU.

ALIONGEZA KUWA AMEFARAJIKA KUONA KUWA KATIKA KIPINDI HICHO HASUSAN KATIKA MIAKA YA HIVI KARIBUNI WATUMISHI WENGI WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WAMEPATA FURSA ZA MASOMO KWA MSAADA WA NCHI HIYO KWA MAFUNZO YA MUDA MFUPI NA MUDA MREFU.

DK. SHEIN ALISISITIZA KUWA HISTORIA YA USHIRIKIANO KATI YA WATU WA ZANZIBAR NA WATU WA INDIA UMEDUMU KWA KARNE NYINGI HIVYO KUNA KILA SABABU KUONA KUWA HISTORIA HIYO INAENDELEZWA KWA KUZIDI KUSHIRIKIANA KATIKA MAENEO MENGI ZAIDI.

ALIMSHUKURU BALOZI KUMAR KWA KUTEKELEZA VYEMA MAJUKUMU YAKE AKIITUMIKIA NCHI YAKE ZANZIBAR NA AMEKIRI KUWA KATIKA KIPINDI CHAKE AMESHUHUDIA UHUSIANO KATI YA NCHI MBILI HIZO UKISHIKA KASI KWA PANDE HIZO KUONYESHA ARI YA KUUENDELEZA NA KUUIMARISHA.

KWA UPANDE WAKE BALOZI KUMAR ALIELEZA KUWA AMEFURAHI KUPATA FURSA YA KUITUMIKIA NCHI YAKE HAPA ZANZIBAR NA KUONGEZA KUWA ANAAMINI AMETEKELEZA VYEMA JUKUMU LAKE LA KUIMARISHA UHUSIANO KATI YA NCHI YAKE NA ZANZIBAR LAKINI ALIKIRI KUWA NCHI MBILI HIZO ZINA FURSA ZAIDI ZA KUIMARISHA UHUSIANO HUO.

WAKATI HUO HUO RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INAKARIBISHA USHIRIKIANO KATI YA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI KATIKA SEKTA YA ELIMU KWA KUTAMBUA KUWA LENGO NI KUTOA FURSA ZAIDI KWA WATOTO NA KUIMARISHA HUDUMA YA ELIMU NCHINI.

DK. SHEIN AMESEMA HAYO LEO WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA UJUMBE WA TAASISI ISIYO YA KISERIKALI KUTOKA NCHINI MAREKANI- OPPORTUNITY EDUCATION FOUNDATION ULIOONGOZWA NA MWANZILISHI WA TAASISI HIYO BWANA JOE RICKETTS.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO DK. SHEIN ALIMUELEZA BWANA RICKETTS KUWA AMEFURAHI KUONA KUWA TAASISI HIYO IMEAMUA KUTOA MCHANGO WAKE KATIKA SEKTA MUHIMU YA ELIMU AMBAPO TAASISI HIYO IMEELEKEZA NGUVU ZAKE KATIKA KUIMARISHA KIWANGO CHA ELIMU KITOLEWACHO MASKULINI.

AMEBAINISHA KUWA NI JAMBO ZURI KUWA TAASISI HIYO IMEELEKEZA MISAADA YAKE KATIKA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI NA KUSISITIZA KUWA USHIRIKIANO KATI YA SEKTA HIZO NI JAMBO LINALOTILIWA MKAZO NA SERIKALI ANAYOINGOZA.

DK. SHEIN AMEELEZA KUWA LENGO LA TAASISI HIYO KUSAIDIA KUIMARISHA KIWANGO CHA ELIMU KATIKA SKULI ZA MSINGI NA SEKONDARI NI MUHIMU KWA KUWA LINAWEKA MSINGI MZURI KWA AJILI YA ELIMU VYUO NA VYUO VIKUU.

KWA HIVYO ALIELEZA MATUMAINI YAKE KUWA USHIRIKIANO HUO UTAENDELEZWA NA AMEIHAKIKISHIA TAASISI HIYO KUWA SERIKALI ITAIPA KILA USHIRIKIANO UTAKAOUHITAJI ILI KUFANIKISHA MALENGO YA TAASISI NA TAIFA KWA JUMLA.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO AMBAYO YALIHUDHURIWA PIA NA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ALI JUMA SHAMUHUNA NA KATIBU MKUU WAKE BIBI MWANAIDI SALEH ABDALLA, DK. SHEIN ALITUMIA FURSA HIYO KUMUELEZA BWANA RICKETTS HATUA MBALIMBALI ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA KUIMARISHA ELIMU IKIWEMO UJENZI WA SKULI BORA ZA KISASA ILI KUIMARISHA UTOAJI WA ELIMU NCHINI.

KWA UPANDE WAKE BWANA JOE RICKETTS ALISEMA KUWA AMEFURAHI TAASISI YAKE KUPATA FURSA YA KUFANYA SHUGHULI ZAKE ZANZIBAR NA KUMSHUKURU MHESHIMIWA RAIS KWA KUIUNGA MKONO TAASISI HIYO NA SHUGHULI INAZOZIFANYA.

TAASISI YA OPPORTUNITY EDUCATION FOUNDATION ILIANZISHWA MWAKA 2005 LENGO LAKE LIKIWA NI KUHAKIKISHA WATOTO KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA WANAPATA KIWANGO BORA CHA ELIMU AMBAPO TAASISI HIYO HUTOA MISAADA KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA KUFUNDISHA NA KUJIFUNZA KATIKA MASKULI.

KWA KUFANYA HIVYO TAASISI HIYO INAAMINI KUWA ITAWEZA KUINUA KIWANGO CHA MAISHA CHA WATOTO WA NCHI HIZO NA KUWAJENGEA MUSTAKABLI BORA WA MAISHA YAO.

HIVI SASA KWA UPANDE WA ZANZIBAR TAASISI HIYO INATARAJIA KUGAWA VIFAA VYA TEKINOHAMA KAMA VILE TABULETI KWA WALIMU NA WANAFUNZI KATIKA BAADHI YA SKULI IKIWEMO SKULI ZA SEKONDARI ZA LAURET ILIYOPO UNGUJA NA FIDEL CASTRO HUKO PEMBA.

USHIRIKIANO WA INDIA NA ZANZIBAR


RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA UHUSIANO NA USHIRIKIANO KATI YA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR NA INDIA UMEKUWA UKIIMARIKA SIKU HADI SIKU AMBAPO WAKATI WOTE PANDE MBILI HIZO ZIMEKUWA ZIKIFANYA JITIHADA ZA KUONA USHIRIKIANO HUO UNALETA TIJA ZAIDI KWA KILA UPANDE.

DK. SHEIN AMESEMA HAYO WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA BALOZI MDOGO WA INDIA BWANA PAWAN KUMAR AMBAYE ALIFIKIA IKULU KUMUAGA RAIS BAADA YA KUMALIZA KIPINDI CHAKE CHA KUITUMIKIA NCHI YAKE HUMU NCHINI.

AMEBAINISHA KUWA TANGU UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA ULIPOANZISHWA MIAKA YA SITINI NCHI HIZO ZIMESHUHUDIA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA UHUSIANO HUO HUKU PANDE HIZO ZIKISHIRIKIANA KATIKA MAENEO MBALIMBALI IKIWEMO ELIMU.

ALIONGEZA KUWA AMEFARAJIKA KUONA KUWA KATIKA KIPINDI HICHO HASUSAN KATIKA MIAKA YA HIVI KARIBUNI WATUMISHI WENGI WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR WAMEPATA FURSA ZA MASOMO KWA MSAADA WA NCHI HIYO KWA MAFUNZO YA MUDA MFUPI NA MUDA MREFU.

DK. SHEIN ALISISITIZA KUWA HISTORIA YA USHIRIKIANO KATI YA WATU WA ZANZIBAR NA WATU WA INDIA UMEDUMU KWA KARNE NYINGI HIVYO KUNA KILA SABABU KUONA KUWA HISTORIA HIYO INAENDELEZWA KWA KUZIDI KUSHIRIKIANA KATIKA MAENEO MENGI ZAIDI.

ALIMSHUKURU BALOZI KUMAR KWA KUTEKELEZA VYEMA MAJUKUMU YAKE AKIITUMIKIA NCHI YAKE ZANZIBAR NA AMEKIRI KUWA KATIKA KIPINDI CHAKE AMESHUHUDIA UHUSIANO KATI YA NCHI MBILI HIZO UKISHIKA KASI KWA PANDE HIZO KUONYESHA ARI YA KUUENDELEZA NA KUUIMARISHA.

KWA UPANDE WAKE BALOZI KUMAR ALIELEZA KUWA AMEFURAHI KUPATA FURSA YA KUITUMIKIA NCHI YAKE HAPA ZANZIBAR NA KUONGEZA KUWA ANAAMINI AMETEKELEZA VYEMA JUKUMU LAKE LA KUIMARISHA UHUSIANO KATI YA NCHI YAKE NA ZANZIBAR LAKINI ALIKIRI KUWA NCHI MBILI HIZO ZINA FURSA ZAIDI ZA KUIMARISHA UHUSIANO HUO.

WAKATI HUO HUO RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INAKARIBISHA USHIRIKIANO KATI YA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI KATIKA SEKTA YA ELIMU KWA KUTAMBUA KUWA LENGO NI KUTOA FURSA ZAIDI KWA WATOTO NA KUIMARISHA HUDUMA YA ELIMU NCHINI.

DK. SHEIN AMESEMA HAYO LEO WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA UJUMBE WA TAASISI ISIYO YA KISERIKALI KUTOKA NCHINI MAREKANI- OPPORTUNITY EDUCATION FOUNDATION ULIOONGOZWA NA MWANZILISHI WA TAASISI HIYO BWANA JOE RICKETTS.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO DK. SHEIN ALIMUELEZA BWANA RICKETTS KUWA AMEFURAHI KUONA KUWA TAASISI HIYO IMEAMUA KUTOA MCHANGO WAKE KATIKA SEKTA MUHIMU YA ELIMU AMBAPO TAASISI HIYO IMEELEKEZA NGUVU ZAKE KATIKA KUIMARISHA KIWANGO CHA ELIMU KITOLEWACHO MASKULINI.

AMEBAINISHA KUWA NI JAMBO ZURI KUWA TAASISI HIYO IMEELEKEZA MISAADA YAKE KATIKA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI NA KUSISITIZA KUWA USHIRIKIANO KATI YA SEKTA HIZO NI JAMBO LINALOTILIWA MKAZO NA SERIKALI ANAYOINGOZA.

DK. SHEIN AMEELEZA KUWA LENGO LA TAASISI HIYO KUSAIDIA KUIMARISHA KIWANGO CHA ELIMU KATIKA SKULI ZA MSINGI NA SEKONDARI NI MUHIMU KWA KUWA LINAWEKA MSINGI MZURI KWA AJILI YA ELIMU VYUO NA VYUO VIKUU.

KWA HIVYO ALIELEZA MATUMAINI YAKE KUWA USHIRIKIANO HUO UTAENDELEZWA NA AMEIHAKIKISHIA TAASISI HIYO KUWA SERIKALI ITAIPA KILA USHIRIKIANO UTAKAOUHITAJI ILI KUFANIKISHA MALENGO YA TAASISI NA TAIFA KWA JUMLA.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO AMBAYO YALIHUDHURIWA PIA NA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ALI JUMA SHAMUHUNA NA KATIBU MKUU WAKE BIBI MWANAIDI SALEH ABDALLA, DK. SHEIN ALITUMIA FURSA HIYO KUMUELEZA BWANA RICKETTS HATUA MBALIMBALI ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA KUIMARISHA ELIMU IKIWEMO UJENZI WA SKULI BORA ZA KISASA ILI KUIMARISHA UTOAJI WA ELIMU NCHINI.

KWA UPANDE WAKE BWANA JOE RICKETTS ALISEMA KUWA AMEFURAHI TAASISI YAKE KUPATA FURSA YA KUFANYA SHUGHULI ZAKE ZANZIBAR NA KUMSHUKURU MHESHIMIWA RAIS KWA KUIUNGA MKONO TAASISI HIYO NA SHUGHULI INAZOZIFANYA.

TAASISI YA OPPORTUNITY EDUCATION FOUNDATION ILIANZISHWA MWAKA 2005 LENGO LAKE LIKIWA NI KUHAKIKISHA WATOTO KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA WANAPATA KIWANGO BORA CHA ELIMU AMBAPO TAASISI HIYO HUTOA MISAADA KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA KUFUNDISHA NA KUJIFUNZA KATIKA MASKULI.

KWA KUFANYA HIVYO TAASISI HIYO INAAMINI KUWA ITAWEZA KUINUA KIWANGO CHA MAISHA CHA WATOTO WA NCHI HIZO NA KUWAJENGEA MUSTAKABLI BORA WA MAISHA YAO.

HIVI SASA KWA UPANDE WA ZANZIBAR TAASISI HIYO INATARAJIA KUGAWA VIFAA VYA TEKINOHAMA KAMA VILE TABULETI KWA WALIMU NA WANAFUNZI KATIKA BAADHI YA SKULI IKIWEMO SKULI ZA SEKONDARI ZA LAURET ILIYOPO UNGUJA NA FIDEL CASTRO HUKO PEMBA.

MAFANIKIO YALIYIPATIKANA KATIKA SEKTA YA AFYA


SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMESEMA KUENDELEZA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA KATIKA SEKTA YA AFYA NI SUALA INALOLIPA KIPAUMBELE KATIKA MIPANGO YAKE YA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA NCHINI.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA HAYO  WAKATI AKIZUNGUMZA NA MWAKILISHI WA SHIRIKA LA AFYA ULIMWENGUNI-WHO ZANZIBAR DK. PIERRE KAHOZI ALIYEMTEMBELEA OFISINI KWAKE IKULU KWA AJILI YA KUMUAGA BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE WA KULITUMIKIA SHIRIKA HILO NCHINI.

AMESEMA SERIKALI INATAMBUA CHANGAMOTO INAZOIKABILI KATIKA KUDUMISHA MAFANIKIO HAYO YAKIWEMO VITA DHIDI YA UGONJWA WA MALARIA NA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO LAKINI KURUDI NYUMA KATIKA MASUALA HAYO ITAKUWA NI KOSA KUBWA.

KWA HIYO ALIMUELEZA DK. KAHOZI KUWA SERIKALI INAENDELEZA JITIHADA ZAKE ZA KUPAMBANA NA MALARIA PAMOJA NA VITA DHIDI YA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO KWA KUCHUKUA HATUA MBALIMBALI IKIWEMO KUONGEZA BAJETI YA SEKTA YA AFYA ILI KUENDELEZA VITA HIVYO.

AKITOLEA MFANO WA VITA DHIDI YA MALARIA, DK SHEIN ALISEMA KUWA MAFANIKIO KUTOKA UWEPO WA ASILIMIA 40 YA MAAMBUKIZI YA UGONJWA HUO HADI KUFIKIA CHINI YA ASILIMIA MOJA NI MATOKEO YA JITIHADA ZA PAMOJA KATI YA SERIKALI NA WASHIRIKA WA MAENDELEO HIVYO KUZIENZI JITIHADA HIZO NI KUIONDOA KABISA MALARIA NCHINI.

KWA UPANDE WA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO ALIELEZA KUWA KUMEKUWEPO NA MAFANIKIO KUTOKA VIFO 476 MWAKA 2006 HADI VIFO 221 MWAKA 2013 KWA KILA MAMA WAJAWAZITO LAKI MOJA NA JITIHADA ZAIDI ZINAFANYIKA ILI KUFIKIA MALENGO YA MILENIA KATIKA SUALA HILO.

ALIBAINISHA KUWA MBALI YA KUONGEZA BAJETI YA SEKTA YA AFYA LAKINI PIA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEBORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WA AFYA ILI KUWAVUTIA KUBAKI NCHINI KULITUMIKIA TAIFA BADALA YA KWENDA NJE AMBAPO KUSABABISHA UHABA WA WATUMISHI HAO.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO YALIYOHUDHURIWA PIA NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA DK. SALEH MOHAMED JIDAWI, DK. SHEIN ALISEMA KWA UPANDE MWINGINE SERIKALI IMEWEKA MKAZO KATIKA KUFUNDISHA WATAALAMU ZAIDI WA SEKTA YA AFYA KWA KUWA HIVI SASA SEKTA HIYO INAKABILIWA NA TATIZO LA UHABA WA WATUMISHI HUSUSAN KADA YA MADAKTARI.

AKIFAFANUA ZAIDI ALIELEZA KUWA HATUA HIZO NI PAMOJA NA KUTOA MAFUNZO KWA KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU CHA TIBA HUKO CUBA, KUANZISHA SKULI YA UDAKTARI KATIKA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR-SUZA NA KUPELEKA NJE WATUMISHI WA AFYA KUPATA MAFUNZO ZAIDI.

KWA UPANDE WAKE DK. KAHOZI ALIIPONGEZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA MAFANIKIO YAKE ILIYOYAPATA KATIKA SEKTA YA AFYA YAKIWEMO YA KUPIGA VITA UGONJWA WA MALARIA NA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO AMBAPO ALIHIMIZA JITIHADA ZAIDI ZIFANYWE KUHAKIKISHA KUWA MAFANIKIO HAYO YANAKUWA ENDELEVU.

KWA HIYO ALITOA WITO KWA SERIKALI KUONGEZA ZAIDI BAJETI YA SEKTA YA AFYA KWA KUWA AFYA NI SEKTA MUHIMU KWA SEKTA NYINGINE ZINAHITAJI WATUMISHI WENYE AFYA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO.

ALIBAINISHA KUWA KUONGEZWA BAJETI KATIKA SEKTA HIYO KITAKUWA KUVUTIO KWA WASHIRKA WA MAENDELEO NAO KUONGEZA MISAADA YAO KATIKA SEKTA HIYO IKIWA NI KIELELEZO CHA KUTHAMINI WAJIBU WA SERIKALI KATIKA KUWATUMIKIA WANANCHI WAKE.

WALIMU WAKUU WATAKIWA KUAANDAA MAZINGIRA


PEMBA.

 

MKUU WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA  DADI FAKI DADI AMEWATAKA WALIMU WAKUU KATIKA WILAYA YA MICHEWENI KUANDAA MAZINGIRA YATAKAYO WAFANYA WANAFUNZI KUONDOA  NA DHANA KWAMBA MASOMO YA SAYANSI NI MAGUMU .

 

KAULI HIYO AMEITOA WAKATI AKIZUNGUMZA NA WALIMU WAKUU  NA WENYEVITI WA KAMATI ZA SKULI ZA WILAYA HIYO KATIKA MKUTANO ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA SKULI YA WINGWI .

 

AMESEMA KUWA DHANA HIYO AMBAYO IMEJENGEKA MIONGONI MWA WANAFUNZI INAPASWA KUONDOSHWA ILI KUPUNGUZA TATIZO LA UPUNGUFU WA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI .

 

AMESEMA KUWA MOJA YA MIKAKATI HIYO  NI PAMOJA NA KUANDAA WANAFUNZI  KUPENDA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI WAKIWA SKULI ZA MSINGI  HALI AMBAYO ITAWAJENGA UWEZO WA KUKABILIANA NA MASOMO HAYO .

 

NAO WASHIRIKI WA KIKAO HICHO WAMEIOMBA SERIKALI YA MKOA KUANDAA ZIARA MAALUMU YA KUTEMBELEA SKULI ZOTE NA KUZUNGUMZA NA WAZAZI ILI KUWAHAMISHA KUCHANGIA KAMBI ZA WANAFUNZI ZILIZOANZISHWA KWA LENGO LA KUWANDAA WANAFUNZI .

 

WAMESEMA KUWA  LICHA YA WALIMU NA KAMATI ZA SKULI KUWA NA MALENGO MAZURI YA KUINUA KIWANGO CHA ELIMU KATIKA WILAYA HIYO BADO JUHUDI ZAO ZIMEKUWA ZIKIVUNJWA NA WAZAZI AMBAO WAMEKUWA WAGUMU KUCHANGIA ILI KUENDELEZA KAMBI ZA MASOMO .

MAKAMO WA KWANZA SOUTH


Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema wakati umefika kwa viongozi wa Afrika kufuata maoni na matakwa ya wananchi, ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima baina ya viongozi na wananchi.

Amesema mara nyingi wananchi huamua kupingana na serikali baada ya kuona haki zao za msingi zinakiukwa, jambo ambalo serikali za sasa zinapaswa kuzingatia madai na haki za wananchi ili kuondosha mivutano hiyo.

Mhe. Maalim Seif ametoa nasaha hizo wakati akizungumza kwenye mkutano wa tisa wa Muungano wa vyama vya Kiliberali na Democrat kwa baadhi ya nchi za Ulaya, Pacific, Afrika na Caribbean (ALDEPAC), unaofanyika mjini Cape town nchini Afrika ya Kusini.

Amesema wananchi wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mengi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ambayo wanapoyapeleka serikalini huwa hayazingatiwi, hali inayopelekea kuibua hamasa miongoni mwa wananchi kuanzisha makundi haramu kupingana na serikali.

Mhe. Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema iwapo madai ya wananchi yatasikilizwa na kupatiwa haki zao za msingi hasa zile za kikatiba, pamoja kuzingatiwa kwa tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, mivutano baina ya wananchi na serikali zao inaweza kupungua.

Ametaja matatizo yanayozisumbua nchi nyingi za Afrika kuwa ni pamoja na umasikini, njaa, ukosefu wa ajira na utawala bora.

Amewaambia wajumbe wa mkutano huo kwamba Afrika sio tena bara lenye kiza, bali raia wake wameamka na kudai mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa ili kila raia aweze kuishi katika maisha bora yenye tija.

“Waafrika sasa wanahitaji maendeleo ya kiuchumi, elimu bora, huduma za afya, maji safi na salama pamoja na kuungwa mkono katika miradi yao ya maendeleo”, alifahamisha Maalim Seif na kuongeza,

“Kubwa zaidi wananchi wanataka uwajibikaji na uwazi katika serikali zao, pamoja na kuwepo uhuru wa kutoa maoni na kuheshimiwa kwa haki za binadamu”.

Amemshukuru Rais wa Muungano wa vyama vya Kiliberali Barani Afrika, Olivier Kamitatu, kwa kuamua kufanya mkutano wao mkuu Zanzibar mwezi uliopita, ambao amesema ulikuwa na mafanikio makubwa.

Mhe. Maalim Seif yuko nchini Afrika ya Kusini kwa mwaliko maalum wa muungano wa vyama vya kiliberali kuhudhuria mkutano huo.

 

UKARABATI SOKO LA DARAJANI


zanzibar.

 

SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMESEMA KUWA INAKUSUDIA KULIJENGA UPYA SOKO KUU LA DARAJANI MJINI ZANZIBAR ILI KUONDOSHA USUMBUFU WANAUPATA WAFANYABIASHARA  WA SOKO HILO.

HAYO  YAMEELEZWA NA Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SEREKALI  YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR  NDUGU  Haji Omar Kheir WAKATI AKIJIBU MASWALI YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI KATIKA KIKAO KINACHOENDELEA HUKO CHUKWANI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.

AMEFAFANUA KUWA SEREKALI INAFAHAMU SUALA LAKUWEPO VIPENU NA UCHAKAVU WA BAADHI YA SEHEMU ZA SOKO HILO HIVYO IMEAMUA KULIJENGA UPYA KWA NJIA YAKUTANGAZA TENDA

AIDHA WAZIRI HUYO AMEBAINISHA KUWA  SEREKALI IMESHAANDAA MICHORO YA UJENZI  WA SOKO HILO NA KILICHOBAKI NI KWA MAMLAKA YA MJI MKONGWE WA ZANZIBAR KUIKUBALI NAKUTOA MAELEKEZO YATAKAYOZINGATIA KUENDELEZWA KWA URITHI WA MJI HUO WAKIMATAIFA.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA


ZANZIBAR.

 

waziri wa katiba na sheria abuubakar khamis bakari amesema kuwa afisi ya mufti zanzibar imekuwa ikichukuwa HATUA MBALI MBALI ZAKUTOA ELIMU KWA MAIMAMU NA MASHEIKH NCHINI ILI KUZUIA MIGOGORO MISIKITINI.

 

WAZIRI ABUUBAKAR AMEELEZA HAYO WAKATI AKIWASILISHA RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA KAMATI YA KATIBA SHERIA NA UTAWALA YA BARAZA LA WAWAKILISHI KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA KATIKA KIKAO KINACHOENDELEA HUKO CHUKWANI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.

 

AMEBAINISHA KUWA HIVI KARIBUNI MAIMAMU 150 WA UNGUJA NA PEMBA WAMEPEWA MAFUNZO  KUHUSU JINSI YAKUEPUKA MIGOGORO MISIKITINI.

 

HATA HIVYO WAZIRI HUYO AMEONGEZA KUWA  WIKI IJAO BARAZA LA ULAMAA ZANZIBAR LINATARAJIWA KUKUTANA KUJADILI SABABU ZAKUONGEZEKA KWA MIGOGORO MISIKITINI.

 

AKIZUNGUMZIA NJIA YAKUONDOA MIGOGORO MISIKITINI  WAZIRI ABUUBAKAR AMESEMA KUWA NIKUREJEA KWA M/MUNGU NAKUFAHAMU KUWA MISIKITI NI NYUMBA YA M/MUNGU NA SI VITEGA UCHUMI.

Monday, January 27, 2014

sheni na miaka thelathini na saba ya ccm


 

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA TANGU MAPINDUZI YA TAREHE 12 JANUARI, 1964 ZANZIBAR IMEKUWA IKIONGOZWA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR AMBAYO INA MAMLAKA KAMILI YANAYOHESHIMIWA NDANI NA NJE YA JAMHURI YA MUNGANO WA TANZANIA.

AMEFAFANUA KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NI SERIKALI HALALI INAYOTAMBULIWA KOTE ULIMWENGUNI HUKU IKIWA INAONGOZWA CHINI YA MIHIMILI MIKUU MITATU; KATIBA, BARAZA LA KUTUNGA SHERIA NA MAHKAMA ILIYO HURU.

DK. SHEIN AMBAYE PIA NI MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR ALISEMA HAYO JANA WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA MAELFU YA WANANCHI WALIOHUDHURIA UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA KUZALIWA CHAMA CHA MAPINDUZI ULIOFANYIKA KATIKA KIWANJA CHA MICHEZO CHA KIEMBESAMAKI, WILAYA YA MAGHARIBI, MKOA WA MJINI MAGHARIBI UNGUJA.

“ZANZIBAR INA BENDERA YAKE, INA RAIS WAKE NA HIVYO HAKUNA ANAYEWEZA KUINGILIA MAMLAKA YA ZANZIBAR” ALISISITIZA DK. SHEIN HUKU AKIULIZA HAO WANAODAI ZANZIBAR ILIYO NA ‘MAMLAKA KAMILI’ WANATAKA NINI HASA.

ALISISITIZA KUWA HAKUNA ANAYEINGILIA MASUALA YA ZANZIBAR NA KUELEZA KUWA ZANZIBAR INAENDESHWA KWA MUJIBU WA KATIBA YAKE AMBAYO INAHESHIMIWA KAMA INAVYOHESHIMIWA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

“SERIKALI YA MAPINDUZI INAJIAMINI NA INAENDESHWA KWA MUJIBU WA KATIBA YAKE AMBAYO INAHESHIMIWA NA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, SASA NANI ANAYEISHUSHIA HADHI SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR?”DK. SHEIN ALIHOJI.

ALIWASHANGAA WATU WANAODAI KUTAKA ZANZIBAR YENYE ‘MAMLAKA KAMILI’ NA KUWAULIZA MAMLAKA HAYO KUTOKA WAPI WAKATI ZANZIBAR TANGU MAPINDUZI YA MWAKA 1964 IMEKUWA IKIJIENDESHA YENYEWE NA KUFANYA MAMBO YAKE BILA KUINGILIWA NA MTU.

DK. SHEIN ALIREJEA MSIMAMO WA CHAMA CHA MAPINDUZI KUHUSU MABADILIKO YA KATIBA NA KUSISITIZA KUWA CHAMA HICHO KINASIMAMIA SERA YAKE YA MUUNGANO WA SERIKALI MBILI.

“KILA MTU AMETOA MAONI YAKE KUHUSU KATIBA NA SISI TUNAONGOZWA NA SERA YETU, KATIBA YETU NA ILANI YETU HIVYO KATIKA HILI LA MUUNGANO SISI TUMESIMAMA KWENYE MUUNGANO WA SERIKALI MBILI” DK. SHEIN ALIELEZA HUKU AKISHANGILIWA NA WANA CCM NA WANANCHI WALIOHUDHURIA MKUTANO HUO.

ALISISITIZA KUWA CHAMA CHA MAPINDUZI HAKITARUDI NYUMA KATIKA MSIMAMO WAKE HUO NA KUSISITIZA KUUENZI KUULINDA NA KUUENDELEZA MUUGANO HUO.

ALIWAELEZA MAELFU YA WANANCHI WALIOKUWA WAKIKATISHA HOTUBA YAKE MARA KWA MARA KWA NDEREMO KUWA WANA CCM NA WANANCHI WANAPOADHIMISHA MIAKA 37 YA KUZALIWA KWA CCM NI KUDHIHIRISHA KUMBUKUMBU YA USHINDI WA VYAMA VYA AFRO SHIRAZI NA TANU VILIVYOWASHINDA WAKOLONI NA KUWALETEA WANANCHI UHURU WAO.

“TUNAPOADHIMISHA MIAKA 37 YA CCM AMBACHO NI MATOKEO YA MUUNGANO WA HIARI WA VYAMA VYA ASP NA TANU, TUNAADHIMISHA PIA KUMBUKUMBU YA USHINDI WA VYAMA VYETU HIVYO DHIDI YA WAKOLONI NA KUTULETEA UHURU WETU” DK. SHEIN ALISEMA.

ALIFAFANUA KUWA WAASISI WA VYAMA HIVYO WAKIONGOZWA NA MZEE ABEID AMANI KARUME NA MWALIMU JULIUS NYERERE WALIFANYAKAZI KUBWA YA KUWAONDOA WAKOLONI NCHINI AMBAPO KWA UPANDE WA ZANZIBAR ILIBIDI WAFANYE MAPINDUZI KULETA UHURU BAADA YA NIJA ZA KAWAIDA KUSHINDIKANA.

ALIWAKUMBUSHA WANA CCM NA WANANCHI KWA JUMLA KUWA MIEZI MICHACHE IJAYO WATAADHIMISHA MIAKA 50 YA MUUNGANO KATI YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR NA JAMHURI YA TANGANYIKA ULIOZAA JAMHURI YA MUUGANO WA TANZANIA HIVYO NI WAKATI MUAFAKA KWAO KUZINGATIA KUMBUKUMBU HIYO MUHIMU KATIKA HISTORIA YA KUJITAWALA.

MAKAMU MWENYEKITI HUYO WA CCM ALITUMIA FURSA HIYO KUMTAMBULISHA MGOMBEA NAFASI YA UWAKILISHI KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA KIEMBESAMAKI MAHMOUD THABIT KOMBO NA KUWATAKA WANANCHI KUMPIGIA KURA ILI CCM IWEZE KUKAMILISHA UTEKELEZAJI WA ILANI YAKE KATIKA JIMBO HILO.

AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO KATIBU MKUU WA CCM KANALI MSTAAFU ABDULRAHMAN KINANA ALIMPONGEZA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR KWA KUKIONGOZA CHAMA HICHO KWA UMAHIRI MKUBWA NA KUIFANYA ZANZIBAR KUENDELEA KUWA TULIVU NA YENYE UMOJA.

AMESEMA CCM ILIZALIWA ZANZIBAR MIAKA 37 ILIYOPITA KISIWANI UNGUJA NA HADI LEO SERIKALI ZOTE MBILI ZIMEENDELEA KUONGOZWA NA CHAMA HICHO HIVYO NI USHINDI MKUBWA KWA WANA CCM.

KATIBU MKUU HUYO ALIWAPONGEZA WANANCHI WA ZANZIBAR KWA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA MAPINDUZI NA KUWATAKA KUJIVUNIA MAENDELEO WALIYOYAPATA KATIKA KIPINDI HICHO CHA MIAKA 50.

“MAADHIMISHO HAYO NI USHINDI MKUBWA KWA WANANCHI WA ZANZIBAR KWA KUWA NDANI YA MIAKA 50 HIYO WAKO WALIYOYABEZA NA WAKO WALIOJITAHIDI KUYAPINGA KWA NGUVU ZAO ZOTE LAKINI WAMESHINDWA NA LEO HII YAMEFIKIA MIAKA 50 NA YATADUMU NA 50 MINGINE” ALISISITIZA KINANA.

ALIWAELEZA WANANCHI HAO KUWA CHAMA CHA MAPINDUZI KITAENDELEA NA JUKUMU LAKE LA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI KWA KUTEKELEZA MIPANGO MBALIMBALI YA MAENDELEO KAMA ILIVYOELEZWA KATIKA ILANI YAKE YA UCHAGUZI PAMOJA NA MIPANGO YA KITAIFA.

ALIWAAMBIA WANA CCM HAO KWAMBA CHAMA CHA MAPINDUZI DAIMA KITAENDELEA KUTEKELEZA JUKUMU LAKE LA KUTENDA MEMA KWA WANANCHI WOTE WA TANZANIA WAKATI VYAMA VYA UPINZANI VITAENDELEA NA JUKUMU LAO LA KUSEMA. “KUSEMA RAHISI KULIKO KUTENDA” ALISEMA KATIBU MKUU WA CCM.

UZINDUZI WA SHEREHE HIZO ULIHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA CCM AKIWEMO MJUMBE WA KAMATI KUU AMBAYE PIA NI MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI NA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR BWANA VUAI ALI VUAI.

raisi sheni amtumia salam za pongezi rais wa india


RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEMTUMIA SALAMU ZA PONGEZI RAIS WA INDIA MHESHIMIWA SHRI PRANAB MUKHERJEE KWA KUADHIMISHA MIAKA 65 YA UHURU WA NCHI HIYO.

KATIKA SALAMU ZAKE HIZO, DK. SHEIN AMESEMA WANANCHI WA ZANZIBAR WANAUNGANA NA NDUGU ZAO WA INDIA KUSHEREHEKEA MAFANIKIO MAKUBWA WALIYOYAPATA KATIKA KIPINDI HICHO CHA MIAKA 65 YA UHURU.

“TUNAUPONGEZA NA KUTHAMINI UHUSIANO ULIOPO KATI YA NCHI ZETU AMBAO UNAZIDI KUIMARIKA SIKU HADI SIKU NA TUNAELEZA DHAMIRA YETU YA DHATI YA KUPANUA USHIRIKIANO HUO KATIKA MAENEO YA UCHUMI, BIASHARA, UTAMADUNI NA MASUALA YA UFUNDI NA UHUSIANO WA KIMAITAIFA” DK. SHEIN AMEELEZA KATIKA SALAMU HIZO.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI AMEITUMIA FURSA HIYO KUMTAKIA RAIS MUKHERJEE AFYA NJEMA NA MAISHA YENYE FURAHA.

DRON ZA MAREKANI

MOGADISHU

MAREKANI IMEENDELEA KUTUMIA NDEGE ZISIZO NA RUBANI (DRONE) KUUA WATU NCHINI SOMALIA LICHA YA MALALAMIKO YANAYOONGEZA YA KIMATAIFA DHIDI YA MASHAMBULIZI HAYO YANAYOUA IDADI KUBWA YA RAIA WASIO NA HATIA KATIKA MAENEO MBALIMBALI DUNIANI.

AFISA MMOJA WA JESHI LA MAREKANI AMBAYE HAKUTAKA JINA LAKE LITAJWE AMESEMA NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZA NCHI HIYO JANA JUMAPILI ZILISHAMBULIA MSHUKIWA WA KUNDI LA AL SHABAB NCHINI SOMALIA.

HATA HIVYO AFISA HUYO WA JESHI LA MAREKANI HAKUTOA MAELEZO ZAIDI KUHUSU MLENGWA NA IWAPO OPERESHENI HIYO ILIKUWA NA MAFANIKIO AU LA.

MAAFISA WA MAREKANI WANASEMA KUWA MLENGWA ALIKUWA AFISA WA NGAZI ZA JU WA KUNDI LA AL SHABAB NA KWAMBA ALIKUWA AKIFUATILIWA NA MAREKANI KWA MIAKA MINGI.
AFISA MWINGINE WA JESHI LA MAREKANI AMESEMA KUWA SHAMBULIZI HILO LILIFANYIKA KARIBU NA ENEO LA BARAWE LILILOKO UMBALI WA MAILI 110 KUTOKA MOGADISHU.

MWEZI OKTOBA MWAKA JANA MAKOMANDOO WA JESHI LA MAREKANI WALIFANYA JARIBIO LA KUMTEJKA NYARA KIONGOZI WA AL SHABAB IKRIMA KATIKA MJI WA BARAWE LAKINI OPERESHENI HIYO HAIKUFANIKIWA.


UCHUNGUZI ULIOFANYWA NA BUREAU OF INVESTIGATIVE JOURNALISM (TBIJ) YENYE MAKAO YAKE NCHINI UINGEREZA UNAONYESHA KUWA NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZA MAREKANI ZIMEUWA KWA AKALI WATU 2,400 DUNIANI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO TOKEA RAIS BARACK OBAMA ACHUKUE MADARAKANI NCHINI HUMO

MAGAZETI YENYE MAANDISHI YA QUR-AN

ZANZIBAR

WAUMINI WA DINI YA KIISLAM NCHINI WAMETAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI WAKATI WANAPOFUNGIWA BIDHAA MBALI MBALI KWA KUTUMIA MAGAZETI AMBAYO MARA NYINGINE HUWA NA MAANDISHI MATAKATIFU YA QUR-AN.

WITO HUO UMETOLEWA LEO NA MUFTI MKUU WA ZANZIBAR SAMAHATU SHEKHE SALEH OMAR KAABI ALIPOKUTANA NA BAADHI YA VIJANA OFISINI KWAKE WALIOMPELEKEA MAGAZETI AMBAYO HUTUMIWA NA WAFANYA BIASHARA KWA AJILI YA KUFUNGIA BIDHAA MBALI MBALI HUKU BAADHI YA MAGAZETI HAYO YAKIWA NA AYA ZA QUR-AN NA HADITHI ZA MTUME.

KWA MUJIBU WA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA KATIBU WA MUFTI WA ZANZIBAR FADHILATU SHEKHE FADHILI SORAGA AMESEMA MUFTI MKUU AMELAANI VIKALI MTINDO HUO ULIOZUKA NA ZAIDI KATIKA SIKU ZA HIVI KARIBUNI.

AMESEMA WAUMINI WOTE WANAPASWA KUHESHIMU MAANDISHI HAYO MATAKATIFU NA NI MAKOSA MAKUBWA KWA MAANDISHI HAYO KUTUMIKA KUFUNGIA BIDHAA.

HATA HIVYO OFISI YA MUFTI ZANZIBAR IMEWATAKA WAINGIZAJI WOTE WA MAGAZETI YA KUFUNGIA BIDHAA KUTOKA NCHI ZA KIARABU,WANUNUZI NA WALE WANAOFUNGIA NA WALE WANAOFUNGIA BIDHAA KWA MAGAZETI HAYO KUHAKIKISHA KWAMBA AYA ZA QUR-AN TAKATIFU HAZITUMIKI NA HADITHI ZA MTUME (S.A.W) HAZITUMIKI KWA MALENGO HAYO.

Saturday, January 25, 2014

UCHAGUZI MDOGO K/SAMAKI

WILAYA YA MAGHARIBI.
Wapigakura Wa Jimbo La Kiembesamaki  Wametakiwa Kumchagua Mgombea Wa Chama Cha Tadea Ili Kuondoa Tatizo La Unyanyasaji Wakijinsia  Kwa Akinamama Na Watoto.

Akifungua Kampeni Za Uchaguzi Mdogo Wa Jimbo La Kiembesamaki Katibu Mkuu Wa Tadea Juma Ali Khatibuwakati Akizungumza Katika Viwanja Vya Kisima Mbaazi.

Amesema Kuwa Jimbo La Kiembesamaki Lina Rasilimali Za Ajira Ambazo Hadi Sasa Hazijafanyiwakazi Hivyo Iwapo Atachaguliwa Mgombea Wa Chama Hicho Ndugu Ali Mohd Mbongo Ataleta Maendeleo Hayo.

Aidha Ndugu Juma Amebainisha Kuwa Chama Chake Kitaangalia Wananchi Wote Wa Hali Za Chini Ili Kuhakikisha Kuwa Wanapata Huduma Zote Muhimu Ndani Ya Kipindi Cha Miezi Mitatu Iwapo Tadea Itapewa Ridhaa.
Amewataka Wakaazi Wa Kiembesamaki Kukichagua Chama Chake Ili Kuhakikisha Kinawaunganisha Wajasiriamali Nakuwapatia Maji Safi  Na Salama Katika Jimbo Hilo. 


Nae Mgombea Uwakilishi Wan Jimbo La Kiembe Samaki Kupitia Chama Cha Tadea Ali Mohd Mbongo Amewataka Wananchi Hao Kumpa Kura Za Ndio Ili Aweze Kuimarisha Dhana Ya Polisi Jamii Ndani Ya Jimbo La Kiembe Samaki Na Kuwalipa Mishahara Sambamba Na Kushughulikia Vituo Vya Afya Kila Shehia Ndani Ya Jimbo Hilo. 

ASASI ZA KIRAIYA


zanzibar.

Wanachama Wa Asasi Za Kiraia Wametakiwa Wametakiwa Kujifunza Mbinu Za Ushawishi Na Utetezi Katika Sera Na Bajeti Nchini.

Akifungua Mafunzo Kwa Wanachama Wa Angoza Katika Ukumbi Wa Eacrotanal Mjini Zanzibar Mwenyekiti Wa Jumuiya Ya Angoza Bi Asha Aboud Amesema Kuwa  Ushawishi Na Utetezi Ni Nyenzo Muhimu Katika Kuishauri  Serikali Kufanya Mabadiliko Ya Mambo Mbali Mbali Nchini.

Sambamba Na Hayo Amesema Kuwa  Katika Kuleta Ushawishi  Ni Vyema Kuwepo Na  Mtu Maalum Wapeleka Ujumbe ,Kufanywa Utafiti Na Kuwepo Fedha Na Tathmini  Hoja Hiyo.

Aidha Amesema Lengo La Mafunzo Hayo Kwa Wanachama Wao Ni Kuleta Mabadiliko Katika Jamii Na Kufahamu Dhana Muhimu Zaushawishi Na Utetezi.

Nae Mtoa Mada Katika Mafunzo Hayo Ndugu Hassan Khamis Juma  Amebainisha Kuwa Asasi Za Kiraia Ni Wadau Ni Wadau Muhimu Katika Katika Utungaji Wa Sera Mbali Mbali  .


Mafunzo Hayo Ya Wiki Nne Yaliwashirikisha Jumla Ya Wachama 40 Kutoka Asasi Za Kiraia Unguja Na Pemba Yameandaliwa Na Angoza Chini Ya Ufadhili Wa The Foundation For Civil Society. 

Waumini Wa Dini Yakiislam

Waumini Wa Dini Yakiislam Kote Nchini Wametakiwa Kuwa Tayari Kujitolea Kwa Hali Na Mali Kwaajili Ya Dini Yao.

Wito Huo Umetolewa Na Al-Ustadh Saleh Ali Wakati Akizungumza Na Waislam Katika Muhadhara Mkubwa Ulioandaliwa Na Jumuiya Na Taasisi Zakiislam Zanzibar  Katika Msikiti Wa Mkwajuni Kidombo Wilaya Ya Kaskazini A Unguja.

Aidha Muhadhiri Huyo Ameelezea Kuskitishwa Kwake Na Jinsi Waislam Wanavyonyanyaswa Nakudhalilishwa Katika Sehemu Mbali Mbali Duniani.

Ameelezea Haja Kwa Waislam Kufanya Maandalizi Yakutosha Ili Kukabiliana Ipasavyo Na Maadui Wa Dini Yao.


Muhadhara Huo Uliondaliwa Na Jumuiya Na Taasisi Zakiislam Zanzibar Umehudhuriwa Na Mamia Ya Waislam Kutoka Mkoa Wa Kaskazini Unguja Na Maeneo Jirani.

Thursday, January 23, 2014

RAIS SHENI ATEUWA WATENDAJI NA KUWAAPISHA


RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN LEO AMEWAAPISHA ND. AHMED KASSIM HAJI KUWA NAIBU KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS NA BIBI RUKIA MOHAMED ISSA KUWA MJUMBE WA KAMISHENI YA UTUMISHI WA UMMA NCHINI.

KUAPISHWA KWA WATENDAJI HAO KUNAFUATIA UTEUZI WAO ULIOFANYIKA HIVI KARIBUNI AMBAPO MHESHIMIWA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ALIMTEUA PIA DK. MOHAMED SEIF KHATIB KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA KISWAHILI ZANZIBAR.

MIONGONI MWA VIONGOZI WALIOHUDHURIA HAFLA HIYO YA KUAPISHWA NI PAMOJA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI, JAJI MKUU WA ZANZIBAR MHESHIMIWA OMAR MAKUNGU, SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI MHESHIMIWA PANDU AMEIR KIFICHO, MUFTI MKUU WA ZANZIBAR SHEIKH OMAR SALEH KABI, KATIBU MKUU KIONGOZI DK. ABDULHAMID YAHYA MZEE, MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA MJI WA ZANZIBAR MHESHIMIWA KHATIB ABDULRAHMAN KHATIB NA MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI ABDALLA MWINYI KHAMIS.

SHENI AKUTANA NA IGP ERNEST MANGU


RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI INSPEKTA JENERALI WA POLISI ERNEST MANGU.

MKUU HUYO WA JESHI LA POLISI ALIFIKA IKULU KUJITAMBULISHA BAADA YA KUTEULIWA HIVI KARIBU NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE KUSHIKA WADHIFA HUO.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO DK. SHEIN ALIMPONGEZA IGP MANGU KWA KUTEULIWA KUSHIKA WADHIFA HUO NA KUMSHUKURU KWA KUKUBALI UTEUZI HUO AMBAO UNAMPA JUKUMU KUBWA LA KUONGOZA JESHI HILO AMBAO WAJIBU WAKE WA KWANZA NI KULINDA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO.

DK SHEIN ALIMUELEZA IGP MANGU KUWA JESHI LA POLISI ZANZIBAR LINASHIRIKI VYEMA KATIKA KUHAMI UCHUMI WA ZANZIBAR KWA KUSHIRIKIANA NA IDARA MAALUM ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KATIKA KUKABILIANA NA MAGENDO YA KARAFUU NA PIA ULINZI KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA HASA YA KITALII.

ALIONGEZA KUWA ANAFARAJIKA KUONA KUWA KUNA UHUSIANO MZURI NA USHIRIKIANO WA KARIBU KATI YA JESHI LA POLISI ZANZIBAR NA WANANCHI HALI AMBAYO IMESAIDIA KATIKA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA NCHINI KUPITIA POLISI JAMII.

AMEFAFANUA KUWA MFUMO WA POLISI JAMII UMESAIDIA KULETA UTULIVU KATIKA MITAA HIVYO KUPUNGUZA VISA VYA UHALIFU KAMA VYA UVUNJAJI WA NYUMBA NA WIZI.

KWA HIVYO ALISEMA KWA UJUMLA HALI YA ULINZI NA USALAMA NCHINI NI SHWARI PAMOJA NA KUBAINISHA KUWA YAPO MATUKIO YA HAPA NA PALE YA WIZI HASA KATIKA MAENEO YA WATALII.

DK. SHEIN AMEMWAMBIA IGP MANGU KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEKUWA IKICHUKUA HATUA KADHA WA KADHA KUIMARISHA USALAMA KATIKA MAENEO YENYE SHUGHULI ZA KITALII LAKINI ALIBAINISHA KUWA JESHI LA POLISI HALINA BUDI KUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUUNGA MKONO HATUA HIZO.

AKIFAFANUA ZAIDI, DK. SHEIN ALISEMA USALAMA KATIKA SEKTA YA UTALII NI KIPAUMBELE CHA KWANZA KWA KUWA SEKTA HIYO, KWA MUJIBU WA MPANGO WA KUPUNGUZA UMASIKINI NA KUKUZA UCHUMI ZANZIBAR-MKUZA, NDIO SEKTA KIONGOZI KATIKA UCHUMI AMBAYO INAIPATIA ZANZIBAR ASILIMIA 80 YA FEDHA ZA KIGENI NA KUCHANGAIA ASLIMIA 27 YA PATO LAKE.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO IGP MANGU AMBAYE ALIKUWA AMEFUATANA NA NAIBU INSPETA JENERALI WA POLISI ABDULRAHMAN KANIKI NA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR CP HAMDANI OMAR MAKAME ALIMUELEZA RAIS KUWA JESHI LAKE LIMEJIPANGA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE IKIWEMO KUKABILIANA NA VITENDO VYOTE VYA KIHALIFU.

ALIELEZA KUWA JESHI LAKE LINAJIIMARISHA ZAIDI KATIKA MASUALA YA UCHUNGUZI WA MATUKIO YA KIHALIFU ZAIDI ILI KUZUIA VITENDO HIVYO KUFANYIKA KABLA HAVIJALETA ATHARI KWA JAMII.

SHEIN AKUTANA NA WAZIRI WA FEDHA WA TANZANIA


RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEKUTANA NA WAZIRI WA FEDHA WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA SAADA MKUYA SALUM.

 

WAZIRI SAADA ALIFIKA IKULU KUJITAMBULISHA RASMI YEYE NA MANAIBU WAKE ADAM KIGOMA ALI MALIMA NA MWIGULU LAMECK NCHEMBA KUFUATIA MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI YALIYOFANYWA HIVI KARIBUNI NA RAIS JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE AMBAPO MABADILIKO HAYO YALIIGUSA WIZARA HIYO.

 

KATIKA MAZUNGUMZO YAKE NA WAZIRI HUYO NA UJUMBE WAKE DK. SHEIN ALISISITIZA UMUHIMU WA USHIRIKIANO NA UTENDAJI KAZI WA PAMOJA ILI KUKIDHI MATARAJIO YA SERIKALI PAMOJA NA MATUMAINI MAKUBWA WALIYONAYO WATANZANIA KWAO.

 

ALIELEZA KUWA KUKABIDHIWA KWAO KUIONGOZA WIZARA HIYO YENYE MAJUKUMU MAZITO NA INAYOTEGEMEWA NA SERIKALI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZAKE NI CHANGAMOTO AMBAYO WANAPASWA KUIKABILI KWA KUDHIHIRISHA WELEDI NA UWEZO WAO KWA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA NA KWA KARIBU NDANI YA WIZARA NA KWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA NYINGINE.

 

DK. SHEIN ALIELEZA MATUMAINI YAKE KUWA UONGOZI HUO MPYA WA WIZARA UTAENDELEA PIA KUFANYA KAZI KWA KARIBU NA WIZARA YA FEDHA YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA MAMBO YANAYOZIHUSU SERIKALI ZOTE MBILI.

 

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI AMEMPONGEZA WAZIRI SAADA NA MANAIBU WAKE KWA UTEUZI HUO NA PIA KUWASHUKURU KWA KURIDHIA UTEUZI HUO KITENDO AMBACHO ALIKIELEZA KUWA KINADHIHIRISHA DHAMIRA YAO YA KWELI YA KUWATUMIKIA WANANCHI.

 

NAYE WAZIRI WA FEDHA BIBI SAADA MKUYA SALUM ALIMSHUKURU MHESHIMIWA RAIS KWA KUWAPA FURSA YA KUKUTANA NAE AMBAPO WAMEWEZA KUJIFUNZA MENGI KUTOKANA NA NAHASA ZAKE WAKATI WA MAZUNGUMZO HAYO.

ALIONGEZA KUWA UJIO WAKE NA TIMU YAKE UMELENGA SIO TU KUJITAMBULISHA BALI PIA KUUHAKIKISHIA UONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUWA WIZARA YAKE ITAENDELEA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANA NA KWA KARIBU WAKATI WOTE.

 

WAZIRI SAADA ALIBAINISHA KUWA ANATAMBUA KUWA WIZARA HIYO INASHUGHULIKIA PIA MASUALA YA MUUNGANO HIVYO ATAHAKIKISHA KUWA KUNAKUWEPO NA USHIRIKIANO WA KARIBU NA UTEKELEZAJI WA HARAKA WA MALENGO YALIYOWEKWA KWA MANUFA YA SERIKALI ZOTE MBILI.

 

MAZUNGUMZO HAYO YALIHUDHURIWA PIA NA KATIBU MKUU KIONGOZI DK. ABDULHAMID YAHYA MZEE, KATIBU MKUU WA WIZARA YA FEDHA YA SERIKALI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. SERVACIUS LIKWELILE, KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA YA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR BWANA OMAR MUSSA, MKURUGENZI WA TAWI LA BENKI KUU YA TANZANIA, ZANZIBAR BWANA NICODEMUS MBOJE NA MENEJA WA UTAWALA NA FEDHA WA TAWI HILO BWANA MANSOUR ABDALLA.

UKOSEFU WA HAKI ZA BINAADAMU MISRI


CAIRO

SHIRIKA LA KUTETEA HAKI ZA BINAADAMU LA AMNESTY INTERNATIONAL LIMEKOSOA VIKALI UKATILI WA VIKOSI VYA USALAMA VYA MISRI DHIDI YA WAANDAMANAJI WANAOMUUNGA MKONO RAIS ALIYEONDOLEWA MADARAKANI MUHAMMAD MORSI.

KATIKA RIPOTI ILIYOTOLEWA JANA JUMATANO KABLA YA MAADHIMISHO YA MWAKA WA TATU WA MAPINDUZI YA WANANCHI MWAKA 2011 YALIYOMUONDOA MADARAKANI DIKTETA HOSNI MUBARAK, AMNESTY IMESEMA WATAWALA WA MISRI WANATUMIA KILA NJIA INAYOWEZEKANA KUWAKANDAMIZA WAPINZANI NA KUKIUKA HAKI ZA BINAADAMU.

MKUU WA AMNESTY INTERNATIONAL MASHARIKI YA KATI NA AFRIKA KASKAZINI HASSIBA HADJ SAHRAOU AMESEMA 'BAADA YA KUPITA MIAKA MITATU, MATAKWA YA 'MAPINDUZI YA JANUARI 25' YA KUTAKA KUHESHIMIWA HAKI ZA BINAADAMU HAYAJAFIKIWA.

WATU KADHAA WALIOONGOZA MAPINDUZI HAYO WAKO KOROKORONI HUKU UKANDAMIZAJI NA UKIUKAJI SHERIA UKIWA JAMBO LA KAWAIDA.' SHIRIKA HILO LA KUTETEA HAKI ZA BINAADAMU LIMEONGEZA KUWA WATU 1,400 WAMEUAWA NA VIKOSI VYA USALAMA KATIKA MACHAFUKO YA KISIASA YALIYOANZA JULAI 3 MWAKA JANA BAADA YA JESHI KUMUONDOA MADARAKANI MORSI.

WAFUASI WA MORSI WAMEKUWA WAKIANDAMANA MARA KWA MARA WAKITAKA AREJESHWE MADARAKANI.

KENYA KUTOTUMA WANAJESHI S. KUSINI


NAIROBI

KENYA IMESEMA HAITATUMA WANAJESHI WAKE KATIKA NCHI JIRANI YA SUDAN KUSINI PAMOJA NA KUWA UMOJA WA MATAIFA UMEIOMBA IFANYE HIVYO.

HAYO YAMEBAINISHWA JANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KENYA BI. AMINA MOHAMMAD AMBAYE AMESEMA UMOJA WA MATAIFA UMEITAKA NAIROBI ITUME ASKARI 5,500 ILI KUZUIA KUENEA VITA SUDAN KUSINI.

AMESEMA SERIKALI YA KENYA ITASAIDIA KUREJESHA AMANI NCHINI HUMO KWA NJIA ZA KIDIPLOMASIA.

BI. AMINA AMEDOKEZA KUWA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LIMEZIOMBA NCHI KADHAA ZIKIWEMO KENYA NA RWANDA KUCHANGIA KIKOSI CHA ASKARI 5,500 KATIKA NCHI HIYO ILIYOTUMBUKIA VITANI TOKEA DESEMBA 15 MWAKA JANA.

AKIJIBU MADAI KUWA UAMUZI WA UGANDA KUTUMA WANAJESHI WAKE JUBA NI TISHIO KWA MAZUNGUMZO YA AMANI NCHINI HUMO, BI. AMINA AMESEMA UAMUZI WA KAMPALA KUTUMA ASKARI WAKE JUBA UMEIDHINISHWA NA SERIKALI YA SUDAN KUSINI PAMOJA NA JUMUIYA YA KIENEO YA IGAD.

WAKATI HUO HUO KATIBU MKUU WA IGAD MAHBOUB MAALIM AMESEMA MAZUNGUMZO YA UPATANISHI YANAENDELEA VIZURI MJINI ADDIS ABABA, ETHIOPIA. 

UMOJA WA MATAIFA UMETANGAZA KUWA WATU KARIBU NUSU MILIONI WAMEKIMBIA MAKAZI YAO SUDAN KUSINI KUTOKANA NA MAPIGANO MAKALI AMBAYO YAMEGEUKA KUWA YA KIKABILA BAINA YA KABILA KUBWA ZAIDI LA DINKA LA RAIS SALVA KIIR NA KABILA LA NUER LA RIEK MACHAR ANAYEONGOZA UASI.

MAKAMO SOUTH


ZANZIBAR                               

 

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMEONDOKA NCHINI LEO KUELEKEA AFRIKA KUSINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI YA KISIASA.

 

AKIWA NCHINI HUMO MAALIM SEIF ATASHIRIKI KATIKA MKUTANO MKUU WA MUUNGANO WA VYAMA VYA KILEBERALI NA DEMOCRAT VINAVYOJUMUISHA BAADHI YA NCHI ZA ULAYA, PACIFIC, AFRIKA NA CARIBBEAN.

 

KATIKA MKUTANO HUO UNAOTARAJIWA KUFANYIKA MJINI CAPETOWN, MAALIM SEIF AKIWA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI CUF, ANATARAJIWA KUPATA FURSA YA KUWASILISHA HOTUBA YAKE KWENYE MKUTANO HUO.