ZANZIBAR.
waziri wa katiba na sheria abuubakar khamis
bakari amesema kuwa afisi ya mufti zanzibar imekuwa ikichukuwa HATUA MBALI
MBALI ZAKUTOA ELIMU KWA MAIMAMU NA MASHEIKH NCHINI ILI KUZUIA MIGOGORO
MISIKITINI.
WAZIRI ABUUBAKAR AMEELEZA HAYO WAKATI
AKIWASILISHA RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA KAMATI YA KATIBA SHERIA NA
UTAWALA YA BARAZA LA WAWAKILISHI KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA KATIKA KIKAO
KINACHOENDELEA HUKO CHUKWANI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.
AMEBAINISHA KUWA HIVI KARIBUNI MAIMAMU 150 WA
UNGUJA NA PEMBA WAMEPEWA MAFUNZO KUHUSU
JINSI YAKUEPUKA MIGOGORO MISIKITINI.
HATA HIVYO WAZIRI HUYO AMEONGEZA KUWA WIKI IJAO BARAZA LA ULAMAA ZANZIBAR
LINATARAJIWA KUKUTANA KUJADILI SABABU ZAKUONGEZEKA KWA MIGOGORO MISIKITINI.
AKIZUNGUMZIA NJIA YAKUONDOA MIGOGORO
MISIKITINI WAZIRI ABUUBAKAR AMESEMA KUWA
NIKUREJEA KWA M/MUNGU NAKUFAHAMU KUWA MISIKITI NI NYUMBA YA M/MUNGU NA SI
VITEGA UCHUMI.
No comments:
Post a Comment