Moto mkubwa uliOTOKEA
JANA umesababisha zaidi ya hekta 11 za msitu wa Ngezi HUKO Makangale Wilaya ya Micheweni KISIWANI
Pemba kuUNGUA.
Mkuu wa Msitu huo Abdi Mzee Kitwana amesema kuwa katika eneo la Mkiang'ombe inakisiwa kUWA jumla ya Hekta kumi zimeteketea huku katika eneo la Vumawimbi Hekta zaidi ya mbili za msitu zimeteketea kwa moto .
Amesema kuwa chanzo cha moto huo katika eneo la Mkiang'ombe shehiya ya Tondooni ni wapika ULEVI AINA gongo ambapo wakati wa msitu huo UKIWAKA walikuta mabaki ya VIFAA VinaVYotumika kutengenezea pombe hiyo haramu .
akizungumzia kwa upande wa eneo la Vumawimbi Shehiya ya Makangale Abdi amesema kuwa hekta mbili za miti aina mbali mbali ZIMEUNGUA .
Hata hivyo amewashukuru wananchi wa shehia hizo , wafanyakazi wa msitu pamoja na kikosi cha zima moto ambao walifanya kazi ya ziada kuhakikishwa moto huo hauendelei kuleta madhara ndani ya hifadhi hiyo .
Mkuu huyo wa Msitu amewataka wananchi waOnaishi kATIKA vijiji vinavyozunguka msitu huo kuendelea kushirikiana na wafanyakazi wa msitu ili kuhakikisha hakutokei hujma ya aina yoyote ndani ya hifadhi hiyo.
No comments:
Post a Comment