ZANZIBAR.
JUMLA YA WANAFUNZI 27,222 WAMEFANYA MTIHANI
WA DARASA LA SABA MWAKA JANA.
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA KHABARI
OFISINI KWAKE MAZIZINI WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR ALI
JUMA SHAMUHUNA AMESEMA KUWA JUMLA YA
WANAFUNZI 1334 WA MICHIPUO NA KIPAWA MAALUM DARASA LA SABA
WAMEFAULU.
AMESEMA KUWA UFAULU WA WANAFUNZI WA
MICHEPUO NA KIPAWA MAALUM DARASA LA SABA UMEONGEZEKA IKILINGANISHWA NA
IDADI YA MWAKA JANA.
AMEZITAJA SKULI BORA ZILIZOFANYA VIZURI KWA MWAKA 2013 KWA DARASA LA SABA
KUWA NI MICHAENI B CHAKE CHAKE KISIWANI PEMBA,MITIULAYA WETE PEMBA NA SKULI YA
WAZAZI AMANI.
HATA HIVYO WAZIRI HUYO AMEBAINISHA KUWA WANAFUNZI 91 WAMEFAULU VIPAJI MAALUMU ,AMBAPO UNGUJA NI 52
NA PEMBA 39 SAWA NA ASILIMIA 14 AMBAYO NI NDOGO IKILINGANISHWA NA MWAKA JANA.
AKIBAINISHA SKULI ZILIZOFANYA VIBAYA DARASA LA SABA WAZIRI SHAMUHANA
AMESEMA KUWA NI PAMOJA NA MFURUMATONGA WILAYA YA KASKAZINI A,KANDWI NA PEMBENI
CHAKE CHAKE.
AKITOA MATOKEO YA WANAFUNZI WA KIDATO CHAPILI AMESEMA KUWA JUMLA YA WANAFUNZI 11,483 SAWA NA ASILIMIA 59.4 WAMECHAGULIWA
KUJIUNGA NA KIDATO CHA TATU.
AMESEMA KUWA SKULI ZILIZOA WANAFUNZI BORA KWA DARASA LA KUMI NI SHUNGI CHAKE CHAKE PEMBA,NYERERE NA
MAKOONGENI.
MATOKEO RASMI YANARAJIWA WAKUTOLEWA NA SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR ZBC
WAKATI WOWOTE KUANZIA KESHO.
MNAENDELEA
KUSKILIZA TAARIFA HII YA KHABARI KUTOKA RADIO ADHANA FM MASJID JUMUIYA RAHALEO ZANZIBAR .
No comments:
Post a Comment