NAIROBI
KENYA IMESEMA HAITATUMA WANAJESHI
WAKE KATIKA NCHI JIRANI YA SUDAN KUSINI PAMOJA NA KUWA UMOJA WA MATAIFA
UMEIOMBA IFANYE HIVYO.
HAYO YAMEBAINISHWA JANA NA WAZIRI WA
MAMBO YA NJE WA KENYA BI. AMINA MOHAMMAD AMBAYE AMESEMA UMOJA WA MATAIFA UMEITAKA
NAIROBI ITUME ASKARI 5,500 ILI KUZUIA KUENEA VITA SUDAN KUSINI.
AMESEMA SERIKALI YA KENYA ITASAIDIA
KUREJESHA AMANI NCHINI HUMO KWA NJIA ZA KIDIPLOMASIA.
BI. AMINA AMEDOKEZA KUWA BARAZA LA
USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LIMEZIOMBA NCHI KADHAA ZIKIWEMO KENYA NA RWANDA
KUCHANGIA KIKOSI CHA ASKARI 5,500 KATIKA NCHI HIYO ILIYOTUMBUKIA VITANI TOKEA
DESEMBA 15 MWAKA JANA.
AKIJIBU MADAI KUWA UAMUZI WA UGANDA
KUTUMA WANAJESHI WAKE JUBA NI TISHIO KWA MAZUNGUMZO YA AMANI NCHINI HUMO, BI.
AMINA AMESEMA UAMUZI WA KAMPALA KUTUMA ASKARI WAKE JUBA UMEIDHINISHWA NA
SERIKALI YA SUDAN KUSINI PAMOJA NA JUMUIYA YA KIENEO YA IGAD.
WAKATI HUO HUO KATIBU MKUU WA IGAD
MAHBOUB MAALIM AMESEMA MAZUNGUMZO YA UPATANISHI YANAENDELEA VIZURI MJINI ADDIS
ABABA, ETHIOPIA.
UMOJA WA MATAIFA UMETANGAZA KUWA
WATU KARIBU NUSU MILIONI WAMEKIMBIA MAKAZI YAO SUDAN KUSINI KUTOKANA NA
MAPIGANO MAKALI AMBAYO YAMEGEUKA KUWA YA KIKABILA BAINA YA KABILA KUBWA ZAIDI
LA DINKA LA RAIS SALVA KIIR NA KABILA LA NUER LA RIEK MACHAR ANAYEONGOZA UASI.
No comments:
Post a Comment