mfanyabiashara maarufu nchini said
seif salami maarufu bin saadun ameporwa jumla ya shilingi milioni 11,500,000 nyumbani kwake rahaleo mjini
zanzibar.
akizungumza na waandishi wa khabari ofisini kwake muemmbe madema kamanda wa
polisi mkoa wa mjini magharibi ndugu mkadam khamis mkadam amesema kuwa mfanyabiashara huyo aliporwa
fedha hizo ambazo alizifunga katika mfuko wa kaki majira ya saa tisa na dakika
55 jioni.
kamanda huyo amewataja majambazi waliopora fedha hizo ambao tayari wanashikiliwa
na jeshi la polisi kuwa ni pamoja
na maulid ali kipara,khamis hajji mkaazi
wa mwera na gangira chalse mshandete msukuma wa dar-es-salaam.
hata hivyo amesema kuwa majambazi
hao waliokamatwa kwa jitihada za polisi na wananchi wa maeneo mbali mbali
walionekana na silaha na risasi kumi na saba.
aidha kamanda mkadam amebainisha
kuwa hadi sasa jumla shilingi milioni 3,900,000 na simu ya mlalamikaji
ameonekana nazo mtuhumiwa wapili.
akizungumza na adhana fm mfashabiashara aliyeporwa fedha hizo ndugu said seif salami amelitaka jeshi la polisi
kuchukuwa hatua kali zakisheria na wahusika kufikishwe mahakamani.
No comments:
Post a Comment